Ni mashaka matupu kwa utawala huu wa awamu ya nne na bunge lake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mashaka matupu kwa utawala huu wa awamu ya nne na bunge lake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Dec 31, 2011.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nijuavyo mimi kwa akili yangu binafsi kazi kubwa ya bunge ni kuisimamia serikali,lakini kwa nchi yetu bunge limekuwa ni kijiwe kama vilivyo vijiwe vingine vya kupiga soga na kuziacha palepale bila kupata ufumbuzi wa tatizo lenyewe.Ni mara ngapi serikali yetu inakaidi mapendekezo halali yanayotambuliwa na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,ilihali wabunge wetu wakihongwa mapesa kwa visingizio vya posho za vikao(sitting allowance).Ni upuzi mtupu ikiwa wawakilishi wa wananchi wanapuuzwa kwa ajili ya udhaifu wao kwa kuongezewa posho.Sipendi kuamini kama kelele zote zile zilikuwa ni funika kombe mwanaharamu apite.

  Kitendo cha serikali kupuuza mapendekezo ya bunge ni kuonyesha dhahiri bunge letu halina meno,na ni sehemu ya kupiga story huku wakitumia kodi za walalahoi bila faida kwa uwakilishi wao.Tulipowachagua na kula viapo vyenu ambavyo viliahidi kuitii na kuiheshimu katiba ya Jamhuri ya mmuungano wa Tanzania ni unafiki mtupu.Mara mangapi bunge linaonyesha udhaifu wake ikiwa ni pamoja na kuvunja vipengele vya katiba kwa kushindwa kuiwajibisha serikali mara inaposhindwa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na bunge kwa niaba ya wananchi?Usaliti huu mwisho wake nini kwa mustakabali wa nchi yetu.


  Sisi sote ni mashahidi kwa jinsi tukio la Luhanjo lilivyochukua kasi,tena wabunge wakiongea kwa jaziba bila kumungÂ’unya maneno, lakini leo hii nini hatima ya Luhanjo.anastaafu kwa heshima kubwa kwa kulivua bunge nguo na kuliacha uchi mbele ya kadamnasi.Uko wapi uzalendo na uaminifu tuliowatunukia kwa kuwapa nafasi ya kuwakilisha mawazo yetu bila kuchumia matumbo yenu.Sitaki kuamini ni ndoto au ni kweli lakini ninanchokisubiri kwa hamu kubwa ni wabunge na bunge lenyewe kama mhimili wa pili wa dola kutoa maamuzi magumu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais. Matukio ya kudhalilishwa kwa bunge letu tukufu huku wananchi tukiamini ndiyo chombo pekee cha kututetea maslahi ya wanyonge mimi ninasema ni uzandiki na unduminakuwili uliopita kiwango.Matukio haya hayakuanza leo,sisi bado ni waathirika wa hali ngumu ya uchumi uliotokana na mapendekezo ya bunge yaliyoshindwa kuteekelezwa kwa kuwakumbatia waliotufikisha hapa kutokana na umeme wa magumashi usio natija uliopelekea nchi kuingia gizani na uchumi wa nchi kushuka kwa kasi kubwa.Tumeona Mwanyika anastaafu tena kwa staili ya waacheni wazee wapumzike,leo hii mwacheni mzee Luhanjo apumzike!hii ni fedheha kwa chombo kilichoaminika kama bunge.Ni bora kama chombo hiki kimeshindwa,wabunge wake wote bila kujali itikadi zao wajiuzulu,huu ni ushauri wa bure tena mtajijengea heshima na kuonyesha nini maana ya utawala bora.


  Mwisho,Napata sana mashaka kwa serikali iliyoko madarakani kama kweli inajua nini inafanya madarakani.Mgawanyo wa madaraka mbona unakiukwa na sisi wananchi tunaangalia bila kusema lolote!Serikali legelege siku zote huipeleka nchi kizani.Hujichukulia madaraka yote na kujifanya yenyewe ndiyo refari,mchezaji,kamisaa na mtazamaji.Kitendo cha serikali kutia pamba masikioni na kupuuza mapendekezo ya bunge ni udhallishaji mkubwa si kwa bunge tu bali na watu waliolisimika bunge hilo(wananchi).Umangimeza huu wa serikali una kikomo chake,ipo siku isiyo na jina wenye nchi tutafanya maamuzi magumu yanayoshindwa kufikiwa na bunge hili legelege na hakika hatutarudi nyuma mpaka kieleweke.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasubiri kuona Bunge la January hii 2012 litasema nini kabla ya kuchangia hoja yako. Ahsante
   
 3. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Pengine mwaka huu 2012 utakuwa wa mabadiliko makubwa kwa bunge Tz. Wataanza kujitambua wao ni nani na kazi yao ni nini.
   
 4. M

  Middle JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hakuna jipya lolote,serikali ipo juu ya bunge siku izi,hakuna mbunge hata mmoja anayebisha.
   
 5. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Funika kombe mwana haramu apite!
   
Loading...