Ni marufuku kukusanyika kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu bila kibali cha Polisi

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
4,072
6,235
Sijaielewa hii amri ya Jeshi la Pilosi ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu katika mkoa wa Arusha,
Inaamaana watu hawataruhusiwa kujumuika kwenye shughuli hata za msiba au sherehe.
Pili suala la wananchi kuamua kujumuika ili kuaga miili ya marehemu kwenye eneo la umma ambalo halina hata uzio (uwanja) ni suala ambalo linaitaji kibali cha Polisi, na hivyo kutokuwa nacho ni kosa.
Naamini kabisa wanachi wangeachwa waomboleze na waage miili ya hao marehemu wa kulipukiwa na bomu kusingetokea vurugu yeyote, nadhani kwa mara nyingine tena Jeshi letu la Polisi limetumia nguvu kubwa sana bila sababu ya msingi na bila utashi wowote.
Naamini kabisa wanachi wangeachwa waage na kisha upelelezi wa polisi uendelee na pasingetokea vurugu zilizotokea leo.
Nashuri Jeshi la Polisi liwaachie hao wanachi waliokamatwa kwa kosa la kukukusanyika bila kibali cha Polisi kwa ajili ya kuaga miili ya hao marehemu ili lijijengee hata kidogo heshima yao iliyoshuka sana kwa sasa
 
hii amri ya police inakiuka utamaduni na desturi zetu za kuaga miili ya marehemu
 
Vitambi vikubwa akili ndogo,
maamuzi kwa kutumia vitambi badala ya akili kidogo walizo nazo ndio madhara yake.
 
Busara zinatofautiana kila mtu na busara yake, ujue hata anayekwenda kuzini na mke wa mtu kwake anafikiri ni haki. Niliwahi kumsikia kijana mmoja aliyekwapua mkoba wa mama mmoja akiwaambia watu waliokuwa wanampiga kuwa "kwa nini mnanipiga wakati ni mkoba tu mbona hamna huruma na wenzenu wakati mimi jana nimelala njaa. Polisi wanatumia busara zao za siku zote, na raia wanataka kushiriki kuaga marehemu. Mtu wa tatu asiye polisi au raia wa Arusha anaweza akapima busara hizi mbili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom