Ni maridhiano na siasa za ustaarabu tu?

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,962
1,687
Inanishangaza sana kuona chama cha upinzani nilichokuwa nakiheshim(cuf) kimechakachuliwa.Hivi ilani na malengo ya cuf kama chama cha siasa yameshafikiwa?CUF ilisajiliwa ili ilete maridhiano na siasa za ustaarabu?Kama ndio, basi ni busara ikatangaza rasmi kuwa imeshafanikiwa malengo na sasa ni tawi la CCM.Imekuwa ni mtindo sasa kila mtu wa CUF anapozungumza bungeni anatafuta namna ya kuungwa mkono na wabunge wa ccm kwa kutamka maneno ya maridhiano na siasa za ustaarabu.CCM imefanikiwa kuifanya cuf iwe chama cha kijinga,sijui kwa nini!Hata pale haki inapokiukwa,CUF ili kuhalalisha watakuja na maridhiano na siasa za ustaarabu.Kama hayo hayakuwa malengo pekee,kwa nini sasa CUF imeacha malengo yake yote kwa mwananchi na kuishia kwanye maridhiano na ustaarabu?Nawashauri hayo maneno yenu ya kijinga yabakie hukohuko kwenye serikali ya umoja wa kitaifa msituletee huku kwa sababu huku hatuna hiyo serikali ya umoja wa kitaifa!Huku kuna chama kandamizi kinachomnyonya mwananchi na mwananchi anahitaji kupiganiwa mpaka mwisho.Sasa maridhiano na siasa za ustaarabu vinatoka wapi?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom