Ni mara ngapi umemfanya afurahi yule umpendaye?

Baba Kapompo

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
1,344
462
Siku moja asubuhi mke wa MTZ-huru alimwambia mmewe kuwa alihitaji fedha anunue chanuo mpya ya kuchania nywele zake ambazo ni ndefu sana na alipenda zikue zaidi.

Fuledi alimwambia mkewe kuwa hana hela kwani ameshindwa hata kununua mkanda mpya na kioo cha saa yake ya mkononi iliyoharibika.

Mke wa MTZ-huru hakuomba zaidi ila akamwelewa mmewe.
MTZ-huru akaenda kibaruani na wakati jioni anarudi akapitia kwa fundi saa na kuiuza ile saa yake kwa bei ya chini sana na kupitia dukani kununua chanuo nzuri mpya.

Aliporudi akiwa amejiandaa kumpa chanuo mkewe alishangaa kumwona mkewe kanyoa nywele na mkononi kashika saa mpya ya kumpa mmewe.

Kumbe na mke alikata zile nywele ndefu na kuuza kwenye kampuni ndogo ambayo hurutubisha nywele na kuziuza kama nywele nyingie bandia ziuzwavyo.

Kila mtu machozi yalimtoka sio kwa uchungu ila kwa kufurahishwa na hatua ya kila mmoja aliyoichukua kumfanya mwenzake afurahi.

Funzo: Mapenzi sio kitu cha ajabu, kupendwa ni kitu cha faraja ila kupendwa na kujaliwa na unayempenda ni jambo la muhimu zaidi.

Hebu jaribu kufikiri ni mara ngapi umemfanya afurahi yule umpendaye katika nyakati zote yaani kwa shida na raha?
 
Kweli kabisa : Kupendwa na kujaliwa na unae mpenda ni raha sana. Mara nyingi sana nimemfanya nimpendae ajione wa tofauti. Nayy ametambua na ananijali zaidi.
 
Siku moja asubuhi mke wa MTZ-huru alimwambia mmewe kuwa alihitaji fedha anunue chanuo mpya ya kuchania nywele zake ambazo ni ndefu sana na alipenda zikue zaidi.

Fuledi alimwambia mkewe kuwa hana hela kwani ameshindwa hata kununua mkanda mpya na kioo cha saa yake ya mkononi iliyoharibika.

Mke wa MTZ-huru hakuomba zaidi ila akamwelewa mmewe.
MTZ-huru akaenda kibaruani na wakati jioni anarudi akapitia kwa fundi saa na kuiuza ile saa yake kwa bei ya chini sana na kupitia dukani kununua chanuo nzuri mpya.

Aliporudi akiwa amejiandaa kumpa chanuo mkewe alishangaa kumwona mkewe kanyoa nywele na mkononi kashika saa mpya ya kumpa mmewe.

Kumbe na mke alikata zile nywele ndefu na kuuza kwenye kampuni ndogo ambayo hurutubisha nywele na kuziuza kama nywele nyingie bandia ziuzwavyo.

Kila mtu machozi yalimtoka sio kwa uchungu ila kwa kufurahishwa na hatua ya kila mmoja aliyoichukua kumfanya mwenzake afurahi.

Funzo: Mapenzi sio kitu cha ajabu, kupendwa ni kitu cha faraja ila kupendwa na kujaliwa na unayempenda ni jambo la muhimu zaidi.

Hebu jaribu kufikiri ni mara ngapi umemfanya afurahi yule umpendaye katika nyakati zote yaani kwa shida na raha?

AVATAR YAKO TUUU MIMI NAISHANGAA

mada yako nzuri ni muhimu kjitoa kwa yule tunayempenda
 
Back
Top Bottom