Ni mapema sana kutenganisha misingi ya Chama na Serikali

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,762
27,841
MAONI YANGU:
Serikali iliyopo na Serikali zote zilizotangulia zimetokana na Chama nikimaanisha Chama Cha Mapinduzi na hapo awali TANU.
Ukipitia kwa undani misingi iliyounda Serikali yetu imetoholewa kutoka katika misingi iliyounda Chama.
Hivyo sio jambo rahisi au la siku moja au la tamko moja kuitengnisha.

Kutenganisha mihimili hii ni process na sio jambo la kukurupuka.
leo hii ukiongelea maadili ya mtumishi wa Serikali yanashabihiana kwa asilimia zaidi ya 90 na maadili ya kiongozi wa CCM.

Tunapoamua ghafla mihimili hii itengane na kuachia loophole ni kama tunataka maadili ya vyama pinzani ndio yawe maadili ya Serikali, tukumbuke kuna vyama vinakubaliana na ushoga au ubepari n.k.

hivyo ni vyema kauli ya makamu Mwenywkiti mpya ikaeleweka kwa context sahihi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,192
17,136
Bo, mada hii inapingana na ile nyingine uliyoweka wewe?

Vipi nini kimekuchanganya kiasi chote hiki?

Unazungumzia serikali na chama kana kwamba ni nchi ya chama kimoja cha siasa?

Serikali inatakiwa iwepo kuwatumikia waTanzania wote wakati wote hata pale panapokuwa siyo ya CCM. CCM inatakiwa iondoke, serikali bado itaendelea chini ya chama kingine cha siasa, au hata kama ni chini ya utawala wa jeshi, ikilazimu kuwa hivyo.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,762
27,841
Bo, mada hii inapingana na ile nyingine uliyoweka wewe?
Vipi nini kimekuchanganya kiasi chote hiki?
....
Kiasili huwezi kuitenga CCM na Serikali kwani baada ya Uhuru philosophy na muundo wa Serikali ulitegemea Elites na resources nyingi za Chama.

Huko mbeleni tena mbeleni sana ndio tunaweza kuja kufanya hivyo.Ila pia usishangae huko mbeleni Chama na Serikali vikaunganishwa zaidi (rejea Uchina).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom