Ni maneno gani ya kwanza kuambiwa baada ya kumtongoza mpenzi wako?

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
228
210
Hi everyone in here,

Ukiufungua moyo wangu kwenye ukurasa wa mwanzo kabisa utakutana na maneno ya kingereza "If you love me, I love you" yaani "Kama unanipenda, nakupenda" Haya ndio maneno ya kwanza kuambiwa na Linda mara baada ya kumtongoza. Sikuamini masikio yangu!

Vpi nyie wenzangu mliambiwaje, baada ya kumtongoza uliyenaye sasa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye: sawa nitakupa jibu kesho.
Mimi: haya powa

Kesho

Yeye: Mambo
Mimi: powa jibu langu vipi
Yeye: mi naona tuendelee kuwa marafiki
Mimi: haitowezekana Bora kila mtu afute namba ya mwenzake
Yeye: Amna bana nilikua nakutania
Mimi: kwahiyo inakuaje
Yeye: nimekukubalia
Mimi: upo wapi saiv
Yeye: nipo nyumbani ntaangalia TV
Mimi: baadae njoo
Yeye: sawa

*THE END*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ALinambia "kwa jina la upendo nimekukaribisha moyoni, daima nitakufanya mkazi wakudum wala si mpita njia" THEN AKAENDELEA
"Ikiwa ardhi ya moyo wangu imekubali kukaliwa nawe, mimi ni nani hata niupinge wito wa moyo " then akanikumbatia kwa hisia hata tukajikuta sote tunatokwa machozi bila kutarajia
 
Back
Top Bottom