Ni mambo yepi ya msingi ya kuzingatia wakati wa kutunga Katiba?

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,129
2,000
Habarini za wakati huu waungwana.

Kwanza kabisa nichukue nafasi kukupa pole ya msiba mzito uliokupata Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Msiba wa kuondokewa na Baba yako kipenzi. Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Nikirejea Kwenye mada tajwa kama ilivyo jieleza kwenye kichwa cha uzi huu.

Nahitaji kujua pia kuufahamisha Umma wa watanzania mambo ya kuzingatia wakati wa kutunga katiba ya nchi.

Nimefikia hatua ya kuandika uzi huu mara baada ya kuona kwamba wanasiasa wengi wanapenda kuwepo na katiba mpya. Lakini ukiwauliza ni mambo gani ungependa yawemo kwenye katiba yetu.

Wengi wanashindwa kutoa maoni yao jinsi wanavyo elewa wao bali watakupa tu mfano wa mambo yaliyomo kwenye katiba za nchi zilizo endelea. Wakidhani kwamba mambo hayo yakiwekwa na kwenye katiba yetu mambo yatakuwa mswano.

Nahitaji kujua, toa mchango wako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom