Supervision
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 265
- 203
Hey jambo watanzania wenzangu!
Ebwana nimefuatilia habari mbalimbali na mijadala mingi mikali nimegundua kumba raisi kuna mambo machache tu akiyafanya malalamiko yatapungua.Mambo hayo ni kama yafuatayo:
1.Kuachilia ajira zile ambazo hazieleweki zitatoka lini?
2.Kupandisha wafanyakazi madaraja na kuachia uhamisho
3.Kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali.
Hili la tatu ni muhimu na linaweza kuchangia uwepo wa pesa kurudi mtaani kwasababu,'
Kuna wafanyakazi wa serikali kila sehemu mjini na vijijini.Kama kijiji kinawafanyakazj 20 ama 30 yaani hapo manesi,mabwanashamba na walimu kila mtu anapata mshahara mkononi siyo chini ya laki sita maana yake ukizidisha mara 30 unakuwa na siyo chini ya milioni kumi na tano.
Watu hawa watachangia kuongeza mzunguko wa pesa kwa kununua bidhaa vijijini na mijini na hata kuanzisha vimiradi ama kujenga nyumba ama kufanya shughuli za kilimo hivyo kuongeza upatikanaji wa pesa hata kwa watu wa chini.
Akimaliza kufanya haya atakuwa amepunguza malalamiko na kuongeza pesa kuzunguka mtaani na hata kuongeza kodi kwa taifa.
Zaidizaidi yatabaki maswala ya kisiasa lakini kwa wananchi wengi pesa itakuwa imerudi na kuhitaji tu maswala machache kama vile kilimo,kusimamia ununuzi wa mazao ili wananchi wanufaike,ukusanyaji mzuri wa mapato na kuziba mirijanya kinyonyaji.
Ni vitu hivi na vingine vidogo sana akivifanya malalamiko yatapungua na wananchi kupiga makofi