Halafu unaweza kulipa hata 100,000 kwa mwezi hadi umalize then unapewa hati.Ooh sawa
Laki.Teh pacha unamaanisha milioni moja au laki?
Bila kupepesa machoOoh hii laki hata wewe pacha unaweza kuninunulia. Utashindwa kunilipia laki kwa mwezi kweli?
ninyi watu mna matatizo gani mimi nauliza kwaajili ya kujifunza kodi tu inanitoa jasho la meno ndio ntanunua kiwanja? Vilevile yatakayosemwa hapa yanaweza kunisaidia hata miaka ijayo
Maelezo marefu yaliyoenda shule,nondo tupu umetupiaMaswali muhimu ya kujiuliza;
1)Lengo la kununua kiwanja ni nin?i.
Unanunua kwa ajili ya Makazi binafsi!? Hapa vitu vingi vinaibuka ..Unafamilia!? Mseja!? unataraji kuwa na familia!?
Swali hili litachangia level ya scheme unayoweza kwenda kununua kiwanja au kuishi. Je inazo Huduma za msingi kusupport mfumo wako wa maisha!? Maana hapo ndipo utakapoamkia kila siku na kulala.
Je kwa ajili ya uwekezaji wa kupangisha!? Uwekezaji unaweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu. Katika uwekezaji wa muda mfupi unapaswa ununue maeneo yenye makazi yaliyokwisha kuanza kuiva, eneo unaloweza kujenga na kupangisha au kuuza kiwanja kwa haraka na kwa faida. Kama ni kwa uwekezaji wa muda mrefu nunua green acre site ambazo huwa ni projects pembezoni mwa miji hizi huchukua mpaka miaka 10+ kuanza kushamiri.
2)Je una uharaka kiasi gani na matumizi ya kiwanja unachotaka kununua!? Kama unataka kuhamia haraka, basi nunua kwenye miradi yenye sound implementation plan .. mfano wauzaji wawe na mpango wa kuleta Huduma ..Kama maji, umeme na Barabara, au wanafacilitate uwekezaji katika Huduma Kama Shule na Afya nk. Usinunue tu kiwanja wa sababu kimepimwa kinaweza kikawa mbali na Huduma zikakawia ukajikuta pesa yako imekamatika ilhali unataka kuhamia haraka.
Kwa matumzi mengine Kama Viwanda na Mashamba ya Mjini haijalishi.. mara nyingi hununuliwa kwa ajili ya uwekezaji was muda mrefu.
Baada ya hayo mengine ya kuangalia ni;-
A) Nunua kutoka kwa mmiliki halali wa eneo. Na Kama Ni Dalali ndiye anayehusika na mauzo omba uone nyaraka halali za muuzaji wa eneo hilo.
B) Fanya Malipo yote kupitia Bank, na utunze nakala ya nyaraka zako. Na ndani ya Slip za Bank Andika "Ni kwa manunuzi ya Kiwanja So &So" ni muhimu hata ikotokea ulitapeliwa with this kind of bank transfer unapakuanzia
C) Ukipelekwa uwandani(Site) kuoneshwa Kiwanja chako, Majina ya Vigingi(beacon) (Kama zipo) yaendane na kile kilochoandikwa katika ramani ya upimaji. Yasipoendana hiyo ni red flag kubwa.
D) Kamilisha Transaction yako mbele ya Mwanasheria. Na mara baada ya mauziano usikawie kufanya taratibu za kubadilisha umiliki kupitia ofisi za Ardhi kwa kumuona afisa Ardhi mteule kwa maelezo ya kina.
Kama lengo ni kununua kiwanja kilichopimwa toka kwa mtu anayemiliki.. unaweza kujiridhisha (kwa ushauri fanya hii kwa viwanja vyote) kwa kufika wizarani na kufanya official search. Hii inatolewa na Wizara kwa malipo kidogo.. lakini inakupa detailled info za kiwanja na umiliki.maana unaweza kuuziwa kiwanja Sahihi lakini sio na muuzaji Sahihi.
Kama unanunua eneo lisilopimwa..
Ukishaliona na ukaridhika. Hakikisha lina designated njia kutoka barabara au njia inayotumika kwa Sasa.
Mkishakukubaliana Fanya malipo kwa njia ya Bank.. na makabidhiano yafanyike mbele ya Viongozi wa serikali ya Mtaa. Chonde chonde wasije watu site na makoti yao ukaambiwa hutu Ni mjumbe wa serikali ya Mtaa, huyu mwenyekiti na mini Ndiye Mtendaji na muhuri.. Utaliwa kekundu.
Chukua taarifa za uwandani (Coordinates) nenda nazo Halmashauri wakuangalizie kama Serikali inao mpango na eneo hilo kuwa sehemu salama.. sio unaanza kujenga kumbe uko juu ya bomba la mji au gesi. Gharama zake ni Kati ya 50k-250k kulingana umekutana na Nani na site iko wapi.
Ukisha kuridhika basi fika serikali ya Mtaa, muda wa kazi na ukutane na Viongozi. Waeleze shida yako watakufungua... Maana Kama Kuna mgogoro wao wana nafasi nzuri zaidi ya kukufahamisha.
La mwisho.. if it feels so good to be true.. then it's definitely a scam. Ukihisi umeula kwenye transaction ya Ardhi sehemu hot Basi baba/mama tembea kifua mbele Kama boya maana utakuwa umeliwa ..Sema haujajua tu Bado.
Alamsiki.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mungu Awaongoze Ndugu zangu... Watu wanatapeliwa wengine wanaangukia na kupata stroke kwasababu za utapeli wa ardhi ... Kuweni makini sana kiongoziMaelezo marefu yaliyoenda shule,nondo tupu umetupia