Ni mambo gani ya kuzingatia unaponunua kiwanja au nyumba?

ninyi watu mna matatizo gani mimi nauliza kwaajili ya kujifunza kodi tu inanitoa jasho la meno ndio ntanunua kiwanja? Vilevile yatakayosemwa hapa yanaweza kunisaidia hata miaka ijayo

kwanza kabisa hakikisha mvua zinanyesha pande zote za hiyo nyumba maana kuna nyumba mvua zinaishia uwani tu
 
Maswali muhimu ya kujiuliza;

1)Lengo la kununua kiwanja ni nin?i.
Unanunua kwa ajili ya Makazi binafsi!? Hapa vitu vingi vinaibuka ..Unafamilia!? Mseja!? unataraji kuwa na familia!?

Swali hili litachangia level ya scheme unayoweza kwenda kununua kiwanja au kuishi. Je inazo Huduma za msingi kusupport mfumo wako wa maisha!? Maana hapo ndipo utakapoamkia kila siku na kulala.

Je kwa ajili ya uwekezaji wa kupangisha!? Uwekezaji unaweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu. Katika uwekezaji wa muda mfupi unapaswa ununue maeneo yenye makazi yaliyokwisha kuanza kuiva, eneo unaloweza kujenga na kupangisha au kuuza kiwanja kwa haraka na kwa faida. Kama ni kwa uwekezaji wa muda mrefu nunua green acre site ambazo huwa ni projects pembezoni mwa miji hizi huchukua mpaka miaka 10+ kuanza kushamiri.

2)Je una uharaka kiasi gani na matumizi ya kiwanja unachotaka kununua!? Kama unataka kuhamia haraka, basi nunua kwenye miradi yenye sound implementation plan .. mfano wauzaji wawe na mpango wa kuleta Huduma ..Kama maji, umeme na Barabara, au wanafacilitate uwekezaji katika Huduma Kama Shule na Afya nk. Usinunue tu kiwanja wa sababu kimepimwa kinaweza kikawa mbali na Huduma zikakawia ukajikuta pesa yako imekamatika ilhali unataka kuhamia haraka.

Kwa matumzi mengine Kama Viwanda na Mashamba ya Mjini haijalishi.. mara nyingi hununuliwa kwa ajili ya uwekezaji was muda mrefu.

Baada ya hayo mengine ya kuangalia ni;-

A) Nunua kutoka kwa mmiliki halali wa eneo. Na Kama Ni Dalali ndiye anayehusika na mauzo omba uone nyaraka halali za muuzaji wa eneo hilo.

B) Fanya Malipo yote kupitia Bank, na utunze nakala ya nyaraka zako. Na ndani ya Slip za Bank Andika "Ni kwa manunuzi ya Kiwanja So &So" ni muhimu hata ikotokea ulitapeliwa with this kind of bank transfer unapakuanzia

C) Ukipelekwa uwandani(Site) kuoneshwa Kiwanja chako, Majina ya Vigingi(beacon) (Kama zipo) yaendane na kile kilochoandikwa katika ramani ya upimaji. Yasipoendana hiyo ni red flag kubwa.

D) Kamilisha Transaction yako mbele ya Mwanasheria. Na mara baada ya mauziano usikawie kufanya taratibu za kubadilisha umiliki kupitia ofisi za Ardhi kwa kumuona afisa Ardhi mteule kwa maelezo ya kina.

Kama lengo ni kununua kiwanja kilichopimwa toka kwa mtu anayemiliki.. unaweza kujiridhisha (kwa ushauri fanya hii kwa viwanja vyote) kwa kufika wizarani na kufanya official search. Hii inatolewa na Wizara kwa malipo kidogo.. lakini inakupa detailled info za kiwanja na umiliki.maana unaweza kuuziwa kiwanja Sahihi lakini sio na muuzaji Sahihi.

Kama unanunua eneo lisilopimwa..

Ukishaliona na ukaridhika. Hakikisha lina designated njia kutoka barabara au njia inayotumika kwa Sasa.

Mkishakukubaliana Fanya malipo kwa njia ya Bank.. na makabidhiano yafanyike mbele ya Viongozi wa serikali ya Mtaa. Chonde chonde wasije watu site na makoti yao ukaambiwa hutu Ni mjumbe wa serikali ya Mtaa, huyu mwenyekiti na mini Ndiye Mtendaji na muhuri.. Utaliwa kekundu.

Chukua taarifa za uwandani (Coordinates) nenda nazo Halmashauri wakuangalizie kama Serikali inao mpango na eneo hilo kuwa sehemu salama.. sio unaanza kujenga kumbe uko juu ya bomba la mji au gesi. Gharama zake ni Kati ya 50k-250k kulingana umekutana na Nani na site iko wapi.

Ukisha kuridhika basi fika serikali ya Mtaa, muda wa kazi na ukutane na Viongozi. Waeleze shida yako watakufungua... Maana Kama Kuna mgogoro wao wana nafasi nzuri zaidi ya kukufahamisha.

La mwisho.. if it feels so good to be true.. then it's definitely a scam. Ukihisi umeula kwenye transaction ya Ardhi sehemu hot Basi baba/mama tembea kifua mbele Kama boya maana utakuwa umeliwa ..Sema haujajua tu Bado.

Alamsiki.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Maelezo marefu yaliyoenda shule,nondo tupu umetupia
 
Mungu Awaongoze Ndugu zangu... Watu wanatapeliwa wengine wanaangukia na kupata stroke kwasababu za utapeli wa ardhi ... Kuweni makini sana kiongozi
 
Hapa nitagawa sehemu Tatu nazo ni:-

A) Lengo la kununua kiwanja ni nini? Ni makazi? Ni biashara? Ni nyumba ya Ibada? Ni huduma za kijamii?
Je hapo unapotaka kununua kwa kuzingatia malengo yako na mpangilio wa watu pale utafiti? Huwezi kusababisha kero kwao au kwako kupigiwa kerere?

B) KAMA NI MAKAZI BINAFSI ZINGATIA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII.
Hapa utazingatia kuwa karibu na
1) Taasisi yako ya Dini ,Mfano siyo wewe mkristo ukajenge karibu na Msikiti utajuta kuzaliwa wakianza swala swalaa za usiku na maneno yao ya vitisho na makelele ya misipika yao.Zingatia kuwa karibu na taasisi ya imani yako ya Dini

2) Huduma za Afya,Shule ,Maji .Miundombinu mfano Barabara,n.k

C)ZINGATIA UHALALI wa umiliki
1) Ukishajiridhisha sehemu A hapo juu vipo sawa,Unakuja sasa kujiridhisha uhalali wa anayekuuzia
kiwanja ndiye mmiliki halali?

Kiwanja hakina mgogoro?

Majirani zake pande zote nne uwatafute bila yeye kujua ongea nao ili wakupe ukweli wa nani ndiye mmiliki halali wa hicho kiwanja na mipaka ya kiwanja hicho na Historia ya kiwanja hicho.

- Nenda ofisi za ardhi ukajiridhishe umiliki wa kiwanja ni nani.

Ukijiridhisha hayo,Tafuta kamishina wa viapo kwa kujibu wa sheria makamishina wa viapo ni Mawakili au Hakimu mlipane na kutiliana saini.

ZINGATIA,;- Kabla ya kutiliana au kulipana hakikisha anayekuuzia umejiridhisha pasipo na shaka yoyote kuwa
  • Ndiye mmiliki halali wa kiwanja hicho.
  • Mkewe au mumewe pamoja na watoto wanajua kiwanja hicho amekiuza na wao wawe sehemu ya mashahidi upande wa muuzaji ili kesho na kesho kutwa wasije wakadhulumiana pesa wakaanza kukusumbua kuwa baba yao au mumewe hakuwahi kuuza kiwanja hicho, hii itakusaidia kuepukana na usumbufu huo.Kuna wengine wanauza kwa lengo la kumkomoa mwanandoa mwenzake lakini sheria haitoi kibali hicho. Mali mliyoitafuta wote na mkiuza basi wote muwe mmekubaliana.

Taratibu zingine za kubadili jina utazifuata.

Watendaji au wenyeviti wa serikali za mitaa au vitongoji kisheria hawana mamlaka ya kusimamia mauziano ya ardhi.Wenye mamlaka ni makamishina wa viapo.

Ukitumia wenyeviti ni sawa na yule ambaye katumia mashahidi wa kawaida tu .Mahakamani watatambulika kama mashahidi tu na ushahidi wao ni wa kawaida tu sawa na yule ambaye hakuwa tumia tofauti na ushahidi utakaotolewa na Kamishina wa viapo huo huchukuliwa kwa uzito mkubwa.

Kila la heri
 
Back
Top Bottom