Ni mambo gani wenza wanaweza kufanya wawapo fungate?

Uttarra

JF-Expert Member
Jan 5, 2019
458
1,000
Nani alisema fungate ni kwa ajili ya kunyanduana?

Kuna kujuana zaidi hasa mkiwa bored unajua uvumilivu, tashtiti na decision making ya mwenzio.

Kuna kujua ndoto/ mipango ya baadae ya kila mmoja na kureconcile jinsi ya kutimiza ndoto zenu kwa usawa ikitokea mna ndoto tofauti.

Kuna kusoma vitabu, kucheza, kula, kunywa na kupanga mipango mingine ikiwapo lini mpate watoto, watoto wangapi etc.
 

grand millenial

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
1,855
2,000
Hello guys!
Hivi ni mambo gani yanaweza kufanywa na wenza wakiwa fungate ili wasiwe bored? Maana hii ya kunyanduana tuuu kwa two weeks naona kabisa ni mtihani.
Inakuwa mtihani kwa sababu mlishaonja kabla ya kuingia ndani ya ndoa so hapo kila mtu kamchoka mwenzake kabla hata two weeks hazijaisha anyways no offence.

Ila fungate sio lazima mkae tu sehemu moja mnaweza kufanya vitu vya tofauti tu maana hizo 2 weeks mnakuwa free zaidi kama mfuko uko vizuri mnaweza kufanya utalii wa ndani pia tembeleeni zanzibar, mbuga za wanyama chukueni na kibali kabisa muwinde hata swala tu.

Pandeni hata mlima kilimanjaro, tembeleeni maeneo ya ki historia au hata maeneo ambayo mnajua kabisa kufika huko ni ndoto (sisemei nje ya nchi ila kama mfuko upo good pia mnaweza kwenda).

Na kama yoote hayo yaneshindikana mnaweza kutumia muda wenu wa free pia mkiwa huko kwa hotel kuongelea future yenu zaidi na mipango mingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom