Ni mambo gani mwanaume anapaswa kufanyiwa na mpenzi/Mke ili asi Cheat?

nelly nashon

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
242
521
Habari!!

Kumekuwa na tabia kwa wanaume wengi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au kuwacheat wapenziwao!

Wanaume wamekuwa na sababu mbalimbali za kufanya hivyo!!
je, we mwanaume mwenzangu, ni mambo gani tunapaswa kufanyiwa na wapenzi wetu ili tusiwacheat?

Tililikaaaaaa!
 
Habari!!

Kumekuwa na tabia kwa wanaume wengi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au kuwacheat wapenziwao!

Wanaume wamekuwa na sababu mbalimbali za kufanya hivyo!!
je, we mwanaume mwenzangu, ni mambo gani tunapaswa kufanyiwa na wapenzi wetu ili tusiwacheat?

Tililikaaaaaa!

Amubali nioe wanawake kadri nipendavyo
 
Binafsi nikifanyiwa haya naweza ishi milele bila kuchepuka.
1)Kutokuudhiwa/kukasirishwa/kukerwa.
2)Kila nikitaka papuchi nisiletewe sababu au maringo au kucheleweshewa.
3)Nikipewa hiyo naniliu nipewe na ushirikiano sio kudo kama naduu na maiti.
4)Amani upendo vitawale nyumbani. Basi
 
Hivi ndivyo Mwanamke Anatakiwa Kufanya kwa
Mume ili Asitoke Nje Ya Ndoa.
Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo
usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia.
Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya
kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya
kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa
dhati.
Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu
ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako,
utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye,
utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata
wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao
kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii
wameachika na bado wanaranda mtaani.
Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye
uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda,
hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia
utundu na ubunifu wako katika yale ambayo
yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa
pekee kwake.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu
kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza
kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa
leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa
kujidai.
Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza
kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia
hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa
kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya
kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo
lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu
wanawake. Kuna wanawake ambao
wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda
sana na kuwapatia kila wanachohitaji.
Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa
kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi
wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.
Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya
wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini
wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa
waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata
kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi
walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana.
Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana
lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani
siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo
tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa
zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni
kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa
huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza
asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa
kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa
tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa
pambo la nyumba tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume
walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao
walikosa wake sahihi ambao wanaweza
kuwashikilia waume zao.
Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo
zinazooonekana kuwashika waume za watu siku
hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na
wabunifu.
Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya
ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba
ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi
karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe
huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake
huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye
aliona kinyaa kuyafanya.
Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya
kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo
ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe.
Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni
uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini
nasema hivyo.
Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama
mwanaume huyo anampenda amfanyie kila
atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi
kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa,
mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona
kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo
wengine wamekuwa wakiyafanya na
wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.
Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini
kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba,
ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini
tambua bado utakuwa na kazi kwenye
kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi
mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.
Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata
kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa
zake tu lakini mambo ya msingi uwe
unampatilizia.
 
Nyie bwana hata mfanyiwe vipi lazma mtachepuka hiyo ni hulka yenu
Nyie ndiyo mmezidi hata ununuliwe BUGATI lazima uchepuke na hata ugegedwe usiku mzima nikitoka dk 5 na wewe unavusha
 
Back
Top Bottom