Ni mambo gani ambayo unadhani yapo ndani ya uwezo wa mbunge wa Tanzania. Na anashindwa kutekeleza jimboni kwake?

Misss Chuga

Senior Member
Oct 6, 2021
181
327
Habari za muda huu wana JF.

Hope ni wazima wote. Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu kwamba ni mambo gani unadhani yapo ndani ya uweza wa wabunge wetu lakini wanashindwa kutekeleza?

Wabunge kama wapeleka kero zetu au shida zetu mbele ya serikali (wawakilishi wetu mbele ya serikali) wamekuwa wakepeleka shida zetu mbalimbali kama inavyotakiwa. Lakini wabunge wetu wamekuwa kimya sana mbunge akiwakilisha kero basi yeye kazi yake imeishia hapo serikali ifanye isifanye kwake yeye mwendo mdundo.

Hoja yangu ni kuwa wabunge hawa wamekuwa wakisubiri serikali kutatua matatizo ya wananchi hata kama ni madogo vipi, ambayo mengine yapo ndani ya uwezo wao kabisa. Tukumbuke hawa watu wanapewa hela nyingi sio mshahara tu, il kuna hela nyingi Kwa ajili ya kuzunguka jimboni kwake.

Unakuta mbunge anashindwa hata kuchukua vijana wawili awaambie wafukue calvati tu maji yapite anasubiri serikali ije ifanye jimboni kwake. Mbunge amekaa miaka mitano bungeni lakini kashindwa kupeleka madawati hata hamsini tu katika shule ya kata.

Sema yako ambayo unadhani yapo ndani ya uwezo wa mbunge lakini anashindwa kutekeleza jimboni kwake.

Karibu!
 
Kero kubwa ya wabunge wetu ni kujiitia miradi iliyotekelezwa na serikali kuu kuwa ni yao na bila wao isingetekelezwa.

Mfano:aliyekuwa mbunge wa tarime vijijini ndg John Heche aliyesema kwenye moja ya mikutano yake kuwa bila yeye kituo cha afya SIRARI kisingejengwa. Wakati ulikuwa mpango wa jpm.
 
Kusupport shughuli za maendeleo ya maeneo yao. Mfano wabunge wajitokeze sana kwenye biashara za watu wa mikoa yao, Bar, Maduka ya nguo na thamani, kupanda Boda, Michezo. Kualika watu majimboni kwao.. yaani wajali vitu vyao. Utaona mambo yatavyoenda.
Alishinda sana Makonda kwa Trick hyo
 
Tuwe siriazi watanzania. Nimejaribu kuwaza mbali kidogo, hv na huko kwa wenzetu duniani hivi unaweza kukuta mbunge anajishughulisha na vikazi vya mwenyekiti wa mtaa kweli. Hakuna chochote cha maana kwa mbunge kama wameshindwa/ ameshindwa kuisimamia serekali. Haiwezekani serekali imetumia matrilion ya pesa vibaya au serekali imeingia mikataba ya kinyonyaji alafu mbunge kalifumbia macho na maisha yanasonga tu. Wabunge wa wenzetu wako siriazi kwenye ishu kama hizo za kuisimamia serekali sio hawa wakwetu
 
Habari za muda huu wana JF.

Hope ni wazima wote. Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu kwamba ni mambo gani unadhani yapo ndani ya uweza wa wabunge wetu lakini wanashindwa kutekeleza?

Wabunge kama wapeleka kero zetu au shida zetu mbele ya serikali (wawakilishi wetu mbele ya serikali) wamekuwa wakepeleka shida zetu mbalimbali kama inavyotakiwa. Lakini wabunge wetu wamekuwa kimya sana mbunge akiwakilisha kero basi yeye kazi yake imeishia hapo serikali ifanye isifanye kwake yeye mwendo mdundo.

Hoja yangu ni kuwa wabunge hawa wamekuwa wakisubiri serikali kutatua matatizo ya wananchi hata kama ni madogo vipi, ambayo mengine yapo ndani ya uwezo wao kabisa. Tukumbuke hawa watu wanapewa hela nyingi sio mshahara tu, il kuna hela nyingi Kwa ajili ya kuzunguka jimboni kwake.

Unakuta mbunge anashindwa hata kuchukua vijana wawili awaambie wafukue calvati tu maji yapite anasubiri serikali ije ifanye jimboni kwake. Mbunge amekaa miaka mitano bungeni lakini kashindwa kupeleka madawati hata hamsini tu katika shule ya kata.

Sema yako ambayo unadhani yapo ndani ya uwezo wa mbunge lakini anashindwa kutekeleza jimboni kwake.

Karibu!
Wajibu wa mbunge kwa mujibu katiba ni upi na job description yake katika jimbo ni nini? Dhana ya uwakilishi inaleta wajibu upi wa mbunge jimboni kwake?

Kazi ya katibu wa mbunge ni ipi?
 
Back
Top Bottom