Ni makosa gani yanaitwa KUHUJUMU UCHUMI?

RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,966
2,019
Miaka ya nyuma maneno 'hujumu uchumi' yalitumika sana. Watu walishtakiwa kwa kuhujumu uchumi, nadhani kulikua hakuna dhamana.
Mbona siku hizi sisikii mtu akishtakiwa kwa hujuma dhidi ya uchumi wetu dhaifu? Sheria ile bado ipo? Kama mtu amesababishia taifa hasara kubwa sana, kisheria hawezi kuwa amehujumu uchumi?
Ni kwanini kesi ya Mhalu isiwe ya kuhumu uchumi?
 
Sheria hiyo bado ipo ndio maana mtu akikamatwa na nyaya za simu au umeme hata za thamani ya milioni moja HAKUNA dhamana.
Usishangae ROYA
 
Hii mbona hatusikii wakihukumiwa hawa wahindi?

Si wanakula nao ndio maana husikii chochote?
Huwezi kata tawi ambalo umekalia, unless uwe kama Abunuwasi. Tutakaokamatwa ni mimi na wewe ambao tumechelewa kulipia grocery na maduka yetu.
Vigogo wa TRA na Wahindi ni "Kopo na Mfuniko"
Be informed
 
Enzi zile za miaka ya 83-84,neno hili lilisikika sana katika masikio ya watanzania,wakati wa PM sokoine. Siku hizi ni nadra sana kusikia.Suala la BOT,Buzwagi haya yote ni kuhujumu uchumi,muulize Patel Jeetu kama kampuni zake zinalipa kodi,anahujumu uchumi huyu. Ukisikia kesi ya kuhujumu uchumi itakuwqa ni kutoka tanga na inahusu wizi wa nyaya ya simu za TTCL,yanayotokea pale bandarini???? thubutu siyasemi,ila nayo yanahujumu uchumi,kama wataka kyaona,agiza gari yako ifike bongo utayaona
 
nafikiri tunahitaji kujua maana paana ya kosa la kuhujumu uchumi. ila kwa idimi aliyesema kuwa kutolipa kodi ni kuhujumu uchumi amekosea. kutokulipa kodi ni kosa la jinai lakini si kosa la kuhujumu uchumi.

nitatoa maana pana zaidi baada ya kufanya utafiti maana no research no right to speak!!!
 
nafikiri tunahitaji kujua maana paana ya kosa la kuhujumu uchumi. ila kwa idimi aliyesema kuwa kutolipa kodi ni kuhujumu uchumi amekosea. kutokulipa kodi ni kosa la jinai lakini si kosa la kuhujumu uchumi.

nitatoa maana pana zaidi baada ya kufanya utafiti maana no research no right to speak!!!

Leta elimu mdau...
 
Back
Top Bottom