Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,408
Miaka kadhaa nyuma elimu ilinitenganisha na familia yangu. Shule niliyotakiwa kusoma ilikuwa mbali sana na nyumbani kwetu (Ile shule wazee walikuwa wanaipenda kiasi kwamba waliamini ile ndio pekee inayonifaa kitaaluma). Ni mwendo wa masaa 18 kwa bus kutoka mkoa niliokuwepo (Nyumbani) kwenda kule ambako nilitakiwa nikasome (pia wapo ndugu).
Hii ilionesha dhahiri kuwa isingekuwa rahisi hata kurudi nyumbani mara kwa mara wakati wa likizo kwani ni mda ambao ilitakiwa niutumie kwa tuition na kupumzika. Ilibidi kukubali uhalisia kuwa sasa naenda mbali na nyumbani na nitakaa kwa dada yake baba. Kabla ya hapo niliwahi kuonana nae mara 2 tu maishani (kiufupi hatufahamiani kwa 98%).
Maisha mapya katika makazi mapya yalianza. Nakumbuka kuna kipindi kama miaka 2 mfululizo tulipitia changamoto kubwa sana ya kimaisha mimi na shangazi. Mlo mmoja kwa siku ndio ilikuwa bajeti yetu, chai na ubwabwa ilikuwa ni misamiati tu ambayo tuliishia kusikia harufu kwa majirani. Bajeti ya sh. 1000 kwa siku ilikuwa inatutosha kabisa mimi na shangazi yangu. Yalikuwa ni maisha chini ya nusu dollar kwa siku.
Sio kwamba shangazi alikuwa ananitesa, HAPANA!, bali upepo wa maisha ulibadilika tu. Sio kwamba wazazi wangu au ndugu zetu wengine kwenye ule mkoa walikuwa hawapo tayari kusaidia, HAPANA!, ila shangazi tu hakuwa tayari na siku zote alinisisitiza kupambana na kila hali na kutopenda kulia liashida mara kwa mara kwa watu wengine. Shangazi alinifundisha somo la maisha na hadi leo linaniongoza. Kuna kipindi shangazi alikuwa analala njaa ili mimi "mtoto' nile kile kidogo alichojaaliwa kesho niwe na nguvu za darasani. Kiufupi malezi/maisha yangu ya miaka 5 kwa shangazi yalijaa upendo wa hali ya juu na furaha tele.
Huyu ndiye shangazi yangu wa dhahabu, mama yangu wa pili baada ya mama yangu mzazi. Nashukurur sasa nimekuwa na ninajitegemea. Siku zote nimekuwa najitahidi kushea kidogo ninachokipata na shangazi yangu. Najua siwezi mlipa wema wake ila siku zote namuomba Mungu anijalie mafanikio ili nije nimlipe japo nusu tu.
Kuna muda nikisikia manyanyaso wanayopata wengine wanaoishi na ndugu zao (mfano Dada, shangazi, mamdogo, shemeji au wifi n.k), huwa naumia sana na nazidi kumshukuru Mungu kwa kunibariki mlezi wa thamani.
Ni kweli, nakiri kuwa upendo wangu kwa shangazi hauwezi kuzidi upendo nilionao kwa wazazi wangu na ndugu zangu wa damu. Ila thamani yake kwangu ni kama ile ya mama na mwana. She is my second Mother!
Dear Aunt, thank you for the precious scene you played in my life series.