Ni maisha mazuri na Furaha kila kona ya nchi, Rais Magufuli amefungamanisha Bunge, Mahakama na Falsafa za kuchapa kazi

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Mabadiliko makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli na kuyafungamanisha kwenye mihimili yote mitatu yaani Bunge,Mahakama na Serikali leo yamezaa matunda makubwa kwa Taifa hili na kuleta furaha isiyo na kifani.

Mara ya kwanza wengi walihisi Rais Magufuli anaingilia mihimili mingine wakati ule akijaribu kuifungamanisha falsafa yake ya nidhamu,uwajibikaji na uchapaji kazi katika Bunge na Mahakama.

Mahakama ya leo si ile ya mwaka 2014,Majaji na Mahakimu wanasafiri kwa mabasi kwenda kusikiliza kesi maeneo ambayo yasingefikika kirahisi kwa kutumia mahakama inayotembea"Mobile court".

Ofisi ya DPP au mwendesha mashtaka si ile ya mwaka 2014 ,Tuliowahi pata matatizo tunafahamu hii ofisi ilikuwepo lakini haikuwa na nguvu kama sheria inavyoitaka,Kesi kubwa za mabilioni leo zinasikilizwa kwa muda mfupi.

Mwenye mamlaka ya kuendelea na kesi au kuifuta ni DPP tu kama sheria inavyomtaka tangu zamani ,lakini sasa ni vitendo na mabilioni yanaonekana.

Bunge limegeuka sehemu ya kujiamini na kuendeleza ujamaa na fikra zetu sio kwa vitisho vya mabeberu,Rais Magufuli alilifungamaisha Bunge kufanya kazi wakati wa corona bila hofu kwa kauli yake moja tu tusitishwe na corona ,

Bunge la sasa sio lile la 2014 lililoogopa kupitisha sheria za kubana mabeberu,Sheria kali za madini zimepitishwa na Bunge ambalo limefungamanishwa na falsafa ya hapa kazi tu.

Mambo haya ndio yamepelekea kila mtu kuwa na furaha na Maisha mazuri.

Muda wa kesi kusikilizwa umepungua sana hivyo kuokoa muda wa watu kufanya shughuli za maendeleo kama falsafa ya Rais Magufuli hapa kazi tu.

Sheria za umiliki wa rasilimali zetu zimeweka historia kwa vizazi vijavyo na hivyo kuondoa dhana kuwa hatuwezi badilisha sheria zetu katikati ya makubaliano hata kama sheria zinatuumiza,Kuna mtu alitishia tutashtakiwa MIGA.

Leo kila mtu ameacha kujadili mambo ya siasa bali mjadala umehamia kwenye mambo ya maendeleo hii yote ni kufungamanisha falsafa za JPM za uchapaji kazi.

Miundombinu na ajira zinazopatikana kwa sasa katika miradi hii mikubwa ni matokeo ya falsafa za JPM

Rais Magufuli hajawahi ingilia muhimili wowote ule, Bali falsafa yake ya uwajibikaji na kuchapa kazi ameifungamanisha kwa mihimili yote.

Leo Bunge linachapa kazi, Mahakama inachapa kazi na Serikali chini ya JPM mwenyewe inasonga mbele.
 
Mfumo uliokuwepo haramu uliokuwapo miaka ile ulihalalishwa na wachache waliokua na maslahi binafsi huku wengi wakibaki wanaumia bila kuwa na wa kuwasikia wala kuwapa msaada msaada.

Lakini ngoja waje kupinga
 
Ina walivyokudharau hata kuchangia umeandika pumba tupu , wahi milembe usije ukavua nguo muda si mrefu , yeye mwenyewe unayemsifia anajua hali haiko hivyo unavyosema wewe , anajikaza tu kisabuni kwa aibu alivyovurunda .
 
Waulize wazazi wako wanavyo kuhangaikia kukutafutia mlo wa siku?
 
Mfumo uliokuwepo haramu uliokuwapo miaka ile ulihalalishwa na wachache waliokua na maslahi binafsi huku wengi wakibaki wanaumia bila kuwa na wa kuwasikia wala kuwapa msaadamsaada

Lakini ngoja waje kupinga
Kwani utawala uliokuwepo hayo yakitendeka ulikuwa ni utawala wa chama gani?
 
Safi, uandishi mzuri, unavutia, mpangilio safi wa hoja, mawazo chanya, nk nk nk

#sina cha kujibu zaidi ya kuunga mkono katika hoja hizi nzito.
#jr
 
Mfumo uliokuwepo haramu uliokuwapo miaka ile ulihalalishwa na wachache waliokua na maslahi binafsi huku wengi wakibaki wanaumia bila kuwa na wa kuwasikia wala kuwapa msaadamsaada
Kwa hiyo unataka uwe unapewa msaada? we boya kweli fanya kazi acha wivu wa kijinga!
 
Ina walivyokudharau hata kuchangia umeandika pumba tupu , wahi milembe usije ukavua nguo muda si mrefu , yeye mwenyewe unayemsifia anajua hali haiko hivyo unavyosema wewe , anajikaza tu kisabuni kwa aibu alivyovurunda .
Hakika wewe ni mpumbavu wa Taifa

Kilichoandikwa ni jinsi Mahakama inafanya kazi sasa,Je kuna mahakama inyotembea yaani Mobile court au haipo?

Je, Bunge limepitisha sheria za madini ambazo lissu alisema tutashtakiwa Miga?

JPM ni mwamba hata alipokuwa waziri watu wengine walimponda lakini itabaki daima JPM anapiga kazi

Nina mashaka na level yako ya elimu au ndio zile za Mzumbe na IFM mnaoshindwa kuapa
 
Back
Top Bottom