Ni Magufuli wa kazi ndani ya Serikali na Chama, panga pangua yake haitabiriki

jijiletublog

Member
Jul 23, 2020
31
74
Na Humphrey Shao, Msakuzi, Dar es Salaam

Ikiwa imepita mwezi mmoja tangu Watanzania waweze kumpa ridhaa ya kuongoza tena kwa miaka mitano tena hapa nchini huku mambo yakiwa ni tofauti kwa Rais Donald Trump wa Marekani ambaye wananchi awajampa ridhaa ya kuwa kiongozi kwa awamu ya pili.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amezidi kujipambanua kuwa yeye sio mtu wa kutabirika katika upangaji wa viongozi kwani pale alipoamua kuendelea na kazi na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu vivyo hivyo akafanya kwa kurejesha jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kusema kuwa anatosha hivyo ataendelea naye.

Pengine hiyo isiwe la kustua sana kwani watanzania wengi waliamini sana katika utatu huu kazi katika serikali hii ya awamu ya tano.

Leo Rais Magufuli ameshtua watu kwa kuonyesha kuwa yeye sio mtu wa kutabirika kwa kumteua katibu wa itikadi uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Humphrey Polepole kuwa mmoja wa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Uteuzi wa Polepole umeacha maswali mengi sana kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini kuwa Rais Magufuli ambaye ndio Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa je? Amedhamiria kufanya pangapangua ndani ya chama hicho.

Wangine wamekuwa na maswali kuwa uteuzi wa Polepole ndio mwanzo wa upangaji wa safu ya baraza la Mawaziri au nini? Lakini hakuna ajuaye nini kitatokea.

Kumekuwa na wingu zito katika mitandao ya kijamii nchini mara baada ya uteuzi wa Polepole kwani kila mmoja ajui nini kutafuata mara baada ya teuzi hizi mbili kati ya nafasi kumi za Mh Dkt John Pombe Magufuli.

Lakini ikumbukwe kuwa moja ya neno la msingi aliloengea wakati akiwa nahutubia wakati wa kufungua bunge Dodoma kuwa kila mmoja achape kazi na akasisitiza kwamba atakuwa na mabadiliko makubwa sana lakini ukiona speed umekushinda ni vyema kujitoa.

Ni wazi kwa speed hii ambayo Magufuli ameanza nayo inalengo la kutufikisha katika nchi ya ahadi ambayo imeandikwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Screenshot_20201130-002033.jpg
IMG_20201129_143859.jpg
 

Acha UONGO wewe! Huyo anayejiita Mwendawazimu Watanzania hatukumpa ridhaa na yeye alilijua hilo kabla ya October 28 hivyo akaandaa mikakati akishirikiana na tume FAKE ya uchaguzi na polisiccm ili kufanya udhalimu ikiwemo mauaji ili kupora uchaguzi. Huoni aibu kuja kuandika uongo humu? 😳
 
Moja ya uteuzi makini, kazi iliyofanyika kwa nchi na chama kwa ujumla ni kubwa sana Magufuli ametutoa hapa na ametufikisha kuleeeeeee nina amini kuwa mpaka 2025 tutakuwa mbali zaidi.

Hongera Polepole.
Hongera JPM kwa umakini Mkubwa.
 
Acha UONGO wewe! Huyo anayejiita Mwendawazimu Watanzania hatukumpa ridhaa na yeye alilijua hilo kabla ya October 28 hivyo akaandaa mikakati akishirikiana na tume FAKE ya uchaguzi na polisiccm ili kufanya udhalimu ikiwemo mauaji ili kupora uchaguzi. Huoni aibu kuja kuandika uongo humu? 😳
Na Mungu atatuhukumia watanzani kwa hili...karma yaja!
 
Back
Top Bottom