Ni Mafanikio yapi ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya za Awamu ya Nne? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Mafanikio yapi ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya za Awamu ya Nne?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 13, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ni miaka minne sasa tangu tupewe kibwagizo kipya cha kisiasa cha Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya.

  Je tumepata mafanikio gani kwa kauli mbiu hiyo?Je hali yetu ya Kisiasa, Uchumi, Kijamii na Kiutendaji zimepata maendeleo tangu tulipoachana na Sera za Uwazi za Mkapa?

  Sikuwahi kusikia maana halisi ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya. Sikumbuki kupewa mnyumbulisho wa kusema Ari, Kasi na Nguvu Mpya zilikuwa ziwekwe wapi na kufanya nini.

  Lakini mategemeo yangu kutokana na kauli hiyo ni kuwa Ari, Kasi n aNguvu ilikuwa ni msukumo mpya wa kuleta maendeleo Tanzania ambao umejaa Ufanisi, Umakini na Uajibikaji.

  Kwa nchi maskini kama Tanzania, mategemeo yangu ilikuwa ni kuwa Serikali hii ya awamu ya nne, ilikuwa ije na mbinu mpya za kumwezesha Mtanzania aongeze juhudi na maarifa katika uzalishaji mali, kupunguza matumizi na kero ambazo zinadumaza na kuweka kizingiti kwenye kusukuma kwetu gurudumu la maendeleo na kuwa na mfumo bora wa uongozi ambao unang'ara kwa Uwajibikaji, Ufanisi na Umakini.

  Najiuliza kwa kutumia vitendea kazi vichache tuu, je kwa miaka hii minne ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya, je Tanzania tumepiga hatua gani katika yafuatayo;
  • Je Uchumi wa Tanzania, pato letu kama Taifa na Mtanzania vimeongezeka na kukua kwa kiasi gani? na katika nyanja gani?
  • Je Mtanzania amepiga hatua ngapi mbele kuachana na Umasikini na kuwa na uwezo wa kujitegemea? Ama amepiga hatua gani mbele kufuta Ujinga na Maradhi?
  • Je Bajeti ya Maendeleo imekua na kuongezeka kwa kiwango gani?
  • Je Bajeti ya Matumizi imepungua kwa kiasi gani?
  • Je deni letu la ndani na la nje limepunguzwa kwa kiasi gani? kama limeongezeka ni sababu gani zilizosababisha likaongezeka? na ni mbinu gani zinatumika kuhakikisha deni linapungua?
  • Je uwiano wa mauzo nje ya nchi na uagizaji bidhaa umepungua na kurekebishwa kwa kiasi gani?
  • Je ni kwa kiasi gani tumepunguza Utegemezi wa misaada na mikopo ili kujiendesha?
  • Je ni mbinu gani zinapangwa kujijenga na kuwa Taifa linalojitosheleza na kuwa na Bajeti ambayo asilimia 80 au zaidi ni kutokana na uchumi wetu na pato la ndani na si mikopo au misaada?
  • Je Kilimo, Ufugaji na Uvuvi vimekua kwa kiasi gani?
  • Je Taifa letu limeongeza akiba ya chakula kukabiliana na njaa na ukame kwa kiasi gani?
  • Je hifadhi ya mazao na usindikaji wa vyakula kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kumeongezeka kwa kiasi gani?
  • Je mazao yetu ya biashara, yameongezeka uzalishaji na ubora kwa kiasi gani na mauzo yake yameongezeka kwa kiasi gani?
  • Je umwagiliaji na ukulima wa kisasa umeongezeka kwa kiasi gani?
  • Je viwanda vyetu vimeongeza uzalishaji kwa kiasi gani?
  • Je tumeweza kwa kiasi gani kuondokana na kuwa wazalishaji wa mali ghafi na kuzigeuza kuwa bidhaa kamili kupitia viwanda vyetu?
  • Je ajira ngapi zimepatikana kutokana na mfumo mpya wa uzalishaji mali?
  • Je Sekta za elimu na afya zimekuwa kwa kiasi gani na mafanikio yake ni yapi?
  • Je vifo kutokana na maradhi kama Malaria, Kipindupindu, Ukimwi, kifua kikuu na watoto wadogo vimepungua kwa kiasi gani?
  • Je lishe na chakula bora zimeongezeka kwa kiasi gani na afya za watoto na wazee zimeongezeka kwa ubora wa kiasi gani?
  • Je ni wahitimu wangapi kutoka katika vyuo vyetu vyote wamepata ajira na wanafanya kazi walizosomea?
  • Je tumeongeza Madaktari, Wauguzi na Watu wa Maabara wangapi?
  • Je Ufanisi, Umakini, Uwajibikaji na Uadilifu umeongezeka kiasi gani serikalini?
  • Je ni kwa asilimia gani mipango ya maendeleo ya Taifa ya MKUKUTA, MKURUBITA na mingineyo imepiga hatua mbele na kuleta mafanikio?
  • Je Serikali imepiga hatua gani ya kuongeza ufanisi kwa kutumia Teknolojia?
  • Je Serikali imefanya juhudi gani kupunguza matumizi holela ya fedha na kudhibiti uvunjaji wa kanuni za mahesabu na utendaji kama ilivyobainishwa na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu?
  • Je uhalifu umepungua kwa kiasi gani? na ni uhalifu wa namna gani?
  • Je ni juhudi gani zimefanyika kujenga mfumo wa Utawala Bora wenye demokrasia ya kweli ambayo ni shirikishi?
  • Je masuala ya kisiasa kama Muungano, Katiba mpya na tume huru za Uchaguzi, zimefanyiwa kazi kwa kiasi gani na matokeo yake ni yapi?
  • Je ni barabara, madaraja, mifereji na vivuko vingapi ngapi vimejengwa na kuongezwa urefu ili kuboresha shughuli za Uchukuzi na Mawasiliano
  • Je huduma za Reli, Bandari na Ndege kama shughuli za Uchukuzi, zimeongezeka kwa kiasi gani na zimechangia vipi kupanuka na kukua kwa maendeleo ya Taifa letu?
  Nafikiri ni muhimu kwa sisi kama Taifa kuipima Serikali yetu na kuwapima viongozi na wawakilishi wetu (wabunge) kwa vigezo vya matokeo ya kazi na si ahadi au kauli mbiu wanazozitoa. Inapaswa tupime vitendo na matokeo na si kuishia kuwa ni programu kwenye makaratasi, majarida na hotuba.

  Ndiyo naana nauliza je ni mafanikio gani hasa yanayopimika kwa vitendo na matokeo tunaweza kusema yamepatikana kutokana na kauli mbiu ya ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya kutoka kwa Uongozi wa Awamu ya Nne chini ya Mheshimiwa Rais Kikwete?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev. Kishoka heshima yako Mkuu. Kwa maoni yangu kauli mbiu ile ilikuwa ni usanii tu wa kuhakikisha Kikwete anasafisha njia yake ya kuingia Ikulu huku akibebwa na mafisadi kwa kutupa Watanzania matumaini makubwa kutoka Serikali ya awamu ya nne na wengine kuthubutu kutamka kwamba 'sasa tumepata mkombozi wetu' na wengine kusema "Kikwete ni chaguo la Mungu".

  Baada ya kukaa madarakani kwa miaka minne sasa kuna ushahidi wa kutosha kwamba Kikwete hajaweza kukamilisha kutimiza hata kauli yake moja aliyoitoa katika kampeni za uchaguzi wa 2005 bali amekuwa mbabaishaji tu ambaye hastahili kuendelea kuwepo madatakani kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  BAK,

  Je tunapima kauli mbiu hiyo na Kikwete pekee kama Rais au ni Serikali ya awamu ya nne ambayo ni ya CCM ikijumuisha na Bunge lake?

  Maana nakumbuka Wabunge wa CCM walikuwa wakiimba mapambio na kaswida za Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya.

  Iweje tumpime yeye pekee na si Serikali yake nzima na Wabunge wake au kwa kifupi Utendaji wa Serikali ya CCM?
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Haya Maswali ndio Jk angebidi aulizwe juu ndugu yangu Kishoka, Lakini kutokana na uwezo wa wetu tulishindwa kufanya hivyo, Hizo ndio kama Nguzo za kufanya kazi kwa Jk na Serikali yake, Kwa miaka yote tumeona huo mwimbo wao ukipungua kusikika machoni wa Watanzania. Kuna haja sisi Kama Taifa kujitafakari na kujiuliza maswali haya kila siku na kufanya uamuzi sahihi. Lakini kwa siasa kama hizi hatuwezi kufika hata kidogo mkuu,
  Taifa lenye maendeleo watu wake wanakuwa na wajibu wa kuzingatioa yote uliyoyasema hapo juu na sio vingine, Lenganisha na Mikakati yao, Mara MKUKUTA, Mara ILANI, Mara Vision ya 2015, sasa tufanye nini tuache lipi??
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mafanikio huyaoni ? Fika bandarini na TRL utaona na kujua CCM imefanya nini .
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Duuh, sio mchezo. Huku kulindana kwa wakubwa huku ipo siku kutatutokea puani. TRL ni siko la kufa ambalo halisikii dawa
  Kama ndio mafanikio hayo basi Kikwete kazi anayo.Tena itakuwa kubwa kuliko ya Mkapa
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Rev, I hope you remember the famous quote from US president Harry Truman, "The bucks stops here"

  Kikwete ndiye Kiongozi wa "Chama Twawala" madudu yote yanayofanyika ndani ya Chama hicho, Serikali na Bunge yanasababishwa na uongozi wake dhaifu na woga ambao nadhani unasababishwa na kuwa karibu mno na mafisadi waliombeba kuingia Ikulu 2005.

  Kwa hiyo kama kiongozi wa chama, Kikwete angweza kabisa kuukemea usanii mkubwa na ufisadi unaofanywa ndani ya chama twawala, serikali na bunge lakini ameamua kufumbia macho maovu yote ndani ya Taasisi hizo pamoja na kuwa kama Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama ana madaraka makubwa ambayo hayatumii.

  Kwa hiyo pamoja na kuipima serikali, Bunge na utendaji wa Ziiziim kwa maoni yangu hakuna mwingine yeyote anayestahili lawama za juu zaidi ya Kikwete kwa yote ambayo yanalalamikiwa na Watanzania. The buck should stop somewhere.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  • Je Uchumi wa Tanzania, pato letu kama Taifa na Mtanzania vimeongezeka na kukua kwa kiasi gani? na katika nyanja gani?
  • Je Mtanzania amepiga hatua ngapi mbele kuachana na Umasikini na kuwa na uwezo wa kujitegemea? Ama amepiga hatua gani mbele kufuta Ujinga na Maradhi?
  • Je Bajeti ya Maendeleo imekua na kuongezeka kwa kiwango gani?
  • Je Bajeti ya Matumizi imepungua kwa kiasi gani?
  • Je deni letu la ndani na la nje limepunguzwa kwa kiasi gani? kama limeongezeka ni sababu gani zilizosababisha likaongezeka? na ni mbinu gani zinatumika kuhakikisha deni linapungua?
  • Je uwiano wa mauzo nje ya nchi na uagizaji bidhaa umepungua na kurekebishwa kwa kiasi gani?
  • Je ni kwa kiasi gani tumepunguza Utegemezi wa misaada na mikopo ili kujiendesha?
  • Je ni mbinu gani zinapangwa kujijenga na kuwa Taifa linalojitosheleza na kuwa na Bajeti ambayo asilimia 80 au zaidi ni kutokana na uchumi wetu na pato la ndani na si mikopo au misaada?
  • Je Kilimo, Ufugaji na Uvuvi vimekua kwa kiasi gani?
  • Je Taifa letu limeongeza akiba ya chakula kukabiliana na njaa na ukame kwa kiasi gani?
  • Je hifadhi ya mazao na usindikaji wa vyakula kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kumeongezeka kwa kiasi gani?
  • Je mazao yetu ya biashara, yameongezeka uzalishaji na ubora kwa kiasi gani na mauzo yake yameongezeka kwa kiasi gani?
  • Je umwagiliaji na ukulima wa kisasa umeongezeka kwa kiasi gani?
  • Je viwanda vyetu vimeongeza uzalishaji kwa kiasi gani?
  • Je tumeweza kwa kiasi gani kuondokana na kuwa wazalishaji wa mali ghafi na kuzigeuza kuwa bidhaa kamili kupitia viwanda vyetu?
  • Je ajira ngapi zimepatikana kutokana na mfumo mpya wa uzalishaji mali?
  • Je Sekta za elimu na afya zimekuwa kwa kiasi gani na mafanikio yake ni yapi?
  • Je vifo kutokana na maradhi kama Malaria, Kipindupindu, Ukimwi, kifua kikuu na watoto wadogo vimepungua kwa kiasi gani?
  • Je lishe na chakula bora zimeongezeka kwa kiasi gani na afya za watoto na wazee zimeongezeka kwa ubora wa kiasi gani?
  • Je ni wahitimu wangapi kutoka katika vyuo vyetu vyote wamepata ajira na wanafanya kazi walizosomea?
  • Je tumeongeza Madaktari, Wauguzi na Watu wa Maabara wangapi?
  • Je Ufanisi, Umakini, Uwajibikaji na Uadilifu umeongezeka kiasi gani serikalini?
  • Je ni kwa asilimia gani mipango ya maendeleo ya Taifa ya MKUKUTA, MKURUBITA na mingineyo imepiga hatua mbele na kuleta mafanikio?
  • Je Serikali imepiga hatua gani ya kuongeza ufanisi kwa kutumia Teknolojia?
  • Je Serikali imefanya juhudi gani kupunguza matumizi holela ya fedha na kudhibiti uvunjaji wa kanuni za mahesabu na utendaji kama ilivyobainishwa na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu?
  • Je uhalifu umepungua kwa kiasi gani? na ni uhalifu wa namna gani?
  • Je ni juhudi gani zimefanyika kujenga mfumo wa Utawala Bora wenye demokrasia ya kweli ambayo ni shirikishi?
  • Je masuala ya kisiasa kama Muungano, Katiba mpya na tume huru za Uchaguzi, zimefanyiwa kazi kwa kiasi gani na matokeo yake ni yapi?
  • Je ni barabara, madaraja, mifereji na vivuko vingapi ngapi vimejengwa na kuongezwa urefu ili kuboresha shughuli za Uchukuzi na Mawasiliano
  • Je huduma za Reli, Bandari na Ndege kama shughuli za Uchukuzi, zimeongezeka kwa kiasi gani na zimechangia vipi kupanuka na kukua kwa maendeleo ya Taifa letu?
  Mkuu Ukisoma bajeti ya mwaka 2008/2009 bila shaka utapata majibu mengi sana..na nadhani ni muhimu tuiweke hali ya Tanzania ilivyokuwa mwaka 2005 alipochukua madaraka na kutumia takwimu zake kulinganisha na hizi zilizopo..

  Binafsi naamini kuna hatua zimepigwa sawa na siafu anayetembea juu ya mpira..akizunguka pale pale. Kwa lugha hiyo huwezi kumwambia mtaalam wala kiongozi kwamba tumekuwa tukizunguka palepale..Na sababu kubwa ni kwamba upeo wetu pamoja na elimuz zetu ni sawa na siafu..
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  BAK,

  Muundo wa Serikali yetu na Katiba hata Katiba ya CCM, inatoa maelezo kuwa kuna mwenye uwezo wa kumdhibiti Rais au Mwenyekiti wa CCM.

  Kama yeye ni legelege kuna mwenye uwezo kumdhibiti na kumgangamalisha, nao ni CC, NEC na BUnge.

  Je wao ni mguu pande ili lawama ziende kwake mwenyewe? Ndio anawajibika kwa kiasi kikubwa, lakini si yeye pekee!
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Rev. K

  Nimemsikia JK akijitenga mbali kabisa na baathi ya ahadi zilizokuwemo kwenye ilani yaUchaguzi ya CCM ya 2005. Kama sikosei baadhi ya mambo aliyoyakwepa ni Mahakama ya Kdhi na Shule za Kata...

  Sasa iwapo tumemruhu yeye kujitenga na ile Ilani ya Uchaguzi sijui ni kwa vipi tutaweza kumuuliza haya maswali...!!!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Rev nadhani umekuwa ukifuatilia vikao mbali mbali vya kamati kuu na halmashauri kuu ya Chama na kuona usanii mkubwa ulionyeshwa na vyombo hivi muhimu sana ndani ya chama. Kama kungekuwa na mtu ndani ya vyombo hivyo viwili unadhani wangeruhusu usanii mkubwa uliofanyika ndani ya vyombo hivyo viwili uliosababisha Spika wa Bunge na wale wapiganaji dhidi ya mafisadi wasulubiwe kiasi kile katika vikao vya hivi karibuni na hatimaye kuunda kamati nyingine ya kisanii ya akina Mwinyi, Msekwa na Kinana? Rev nadhani unajua pia madaraka makubwa aliyokuwa nayo Kikwete ka Rais wa Tanzania je, ni nani katika vyombo hivyo muhimu ndani ya chama ataweza kumdhibiti Kikwete? Tumeona jinsi mafisadi walivyotaka kumfukuzisha chama Spika ili wamweke fisadi mwenzao pia tumeona jinsi mafisadi ndani ya CC na NEC wanavyojitahidi kila kukicha kutala kumsafisha fisadi Mkapa pamoja na ushahidi wa kutosha dhidi yake.

  Kwa kifupi mafisadi ndani ya chama wameshika 'utamu' na Kikwete kwa kuwaogopa mafisadi ndani ya chama amewapa nguvu kubwa hata kuweza kutishia uhai ya wale wanaopiga vita. Kwa hiyo bado kwa maoni yangu wa kulaumiwa hapa ni Kikwete kwa kuwa Kiongozi muoga na dhaifu kutokana na kuwa karibu mno na mafisadi.

  Nadhani unakumbuka ile kauli ya Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi kwamba mafisadi ni matajiri wakubwa mno na kama wakikamatwa nchi itawaka moto. Rev, unakubaliana na kauli hii kuhusiana na mafisadi? Mimi sikubaliani nayo hata kidogo.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Toka bunge lipitishe bajeti ya kifisadi nilikata tamaa,ufisadi kama mti,dawa ni kuuong'olea mbali na mizizi yake,sijui kwanini ni pagumu hapo kuelewa.Ndio cost ni kubwa kwasababu itabidi tuanze from scratch,lakini ndo dawa yenyewe,kama vile kuitibu kansa ambapo sometimes kiungo muhimu inabidi kikatiliwe mbali,ndivyo itakavyokuwa kwenye kuumaliza ufisadi kwani bila kuwafyekea mbali hakuna solution,huwezi kuchanganya halafu still iwe normal,ni kama nyongo ikishapasuka kuku haliki.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  YbYb, huu ndiyo usanii per se wa Kikwete. Wakati zile ilani ya uchaguzi inakuwa formulated Kikwete aliiona na si ajabu alishiriki katika vikao vya kuipitisha kama Rais na Mwenyekiti mtarajiwa. Leo miaka minne baadaye anajirusha kimanga kama metre milioni kwa sababu anaona tu zimeleta kelele kubwa katika kona mbali mbali za nchi yetu. Alikuwa wapi wakati ilani ya uchaguzi wa 2005 inatungwa na kupitishwa? Alikuwa wapi 2006, 2007 na 2008? Sasa anaona tunaelekea katika uchaguzi wa 2010 anataka kujisafisha ile yeye aonekane hakuhusika kabisa na kutunga au kuipitisha ilani ya uchaguzi wa 2005.

  Basi atwambie Watanzania ni nani waliohusika kuitunga na kuipitisha ilani ya uchaguzi wa 2005 pia atwambie yeye kama Rais na Mwenyekiti mtarajiwa hakuiona kabisa ilani ile? Je, kama aliiona ilani ile ya uchaguzi, je aliziona hizi kasoro ambazo anaziona miaka minne baadaye!?
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Rev Kishoka
  Mpaka sasa hakuna kitu chochote substantial kinachoweza kuoneshwa kuwa ni mafanikio ya serikali ya awamu ya nne. Kama vipi ni vidogo sana. Huwezi kulinganisha hata kidogo na utawala wa Mkapa. Mafanikio yote ya utawala wa Mkapa sasa yanakuwa eroded. Hii sio siri tena kwa mtanzania yoyote
   
 15. K

  Kijunjwe Senior Member

  #15
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hotuba ya kwanza ya JMK katika bunge ilinipa matumaini kiasi ukilinganisha na mwenendo wake kabla ya kupewa jukumu la kuongoza nchi. Kauri yake ya kufuata mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya 3, nilidhani atajitahidi kukumbatia njia zilizo kuu za maendeleo kama zilivyobainishwa na kuanza kupewa muelekeo na BWM. Nilitegemea uendelezaji wa miuondombinu mfano reli, bandari na barabara. Lakini ajabu na kweli, miradi yote mikubwa inakufa bila kuleta mabadiriko yaliyotarajiwa, mfano kasi ya ujenzi wa barabara, uboreshaji wa mashirika ya umma kwa kile wakiitacho privatization.

  Kwa mwendo uliopo kuwakumbusha sisiem juu ya kauri mbiu hiyo ni kuwachokoza kama sio kuwatusi. Kijacho kwa sasa ni Kilimo kwanza, then watatafuta connection na Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya (= ANGUKA) na kuwaongopea Wadanganyika na Wazanzibara.

  Kwa mwenendo wa utekelezaji wa ANGUKA majibu ya maswali ya REV ni vigumu kupata.
   
 16. w

  wasp JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unataka kujua mafanikio ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya kawaulize wabunge. Wao kipato chao kimekwenda juu bila kufanya jambo lolote la maana. Lakini kwa walalahoi imekuwa ni balaa kwa sababu ya ufinyu wa bajeti.
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tunaambiwa kuwa Mkapa aliacha Surplus, sasa hivi tuko kwenye Deficit, je CCM waliounda Ilani ya Uchaguzi 2005 wanafanya nini kuratibu utekelezaji wa Ilani hiyo?
   
 18. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  UFISADI MTUPU. ni Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya katika kulinda mafisadi.
   
 19. C

  Captainjames New Member

  #19
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  James Njenga Ng'ang'a.
  P.O Box 33086 Ngara,
  Code: 00600
  Nairobi.
  Tel: 0723-501585, Email:jjamesnjenga@yahoo.com

  To The Human Resources Manager
  CWS/JVA
  P. O. Box 14176
  00800 Westlands
  Nairobi, Kenya
  Email: hr @ jvakenya.org

  Dear Sir/Madam

  Ref: Application for Emproyement

  I am 27 years of age, Highly experienced in Eco-Tourism, Forest Conservation And Community Based First Aid cum driver/ Marketer; I am a member of Kenya Red Cross Society with over 5½ years experience,

  I have proven my abilities, to maintain high standards while meeting strict deadlines with minimal supervision. I have been able to manage Tourism and Community first aiding record with great integrity and professionalism.

  I hereby apply for employment, in presence of a vacancy, in your institution.

  I have attached my curriculum vitae to this mail.

  I promise to work hard to meet your standards of work.

  Thank you for your consideration.
   
 20. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  What? employment?
   
Loading...