Ni maeneo gani kwa Morogoro mjini ni mazuri, tulivu na salama kwa kuishi?

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,716
3,233
Wakuu, Habari zenu nyote.

Nimehamishiwa Moro kikazi, bado sijaripoti na vile JF ni jumuiya ya watu wengi naomba kupata msaada wa kufahamu maeneo mazuri na salama ya kuishi kwa mkoa wa Morogoro.

Nina familia hivyo nahitaji maeneo ya mazingira salama kwa vile mda mwingi majukumu yangu yananilazimu kusafri.

Hiyo sehemu iwe na maji ya uhakika na yasiwe maeneo yenye vibaka.
 
Kihonda magorofani na Airport, Kwingine kuliko tulia huna hela ya kukufanya uishi.
Wewe umejuaje hana hela?

Hivi watu wa jf tukiwa nyuma ya keyboard tunapata wapi huu ujuaji wa maisha ya watu, Ukiwa wewe huna hela unadhani wengine wote hawana?

Yeye kauliza maeneo wewe mwambie, yeye mwenyewe ataenda kujipima.
 
Wewe umejuaje hana hela?
Ndo ulichokiona?

Hivi watu wa jf tukiwa nyuma ya keyboard tunapata wapi huu ujuaji wa maisha ya watu, Ukiwa wewe huna hela unadhani wengine wote hawana?
Nauliza tena ndio ulichokiona?

Yeye kauliza maeneo wewe mwambie, yeye mwenyewe ataenda kujipima.
Kwa hiyo sijamjibu?
Ahahahaha naona maneno yangu ya hana hela ya kuishi maeneo mengine tulivu tofauti na Kihonda na Airport yamekuchoma sana na umeyageuza kuwa mada hadi umesahau kuwa nimeshajibu swali.
.
yani wewe ni mwepesi sana kukutoa kwenye mstari
 
SUA

BIGWA

AREA 5

FOREST
(juu juu kule sio huku chini mwanzoni)

KIHONDA

JORDAN CHUO
(ule mtaa wenye hicho chuo siukumbuki jina)
 
Japo sijajua uwezo wake kifedha lakini Forest hill pale ni pazito na hata uwezekano wa kupata house for rent ni mgumu kidogo..otherwise ni sehemu nzuri sana...pametulia mno ..kuna uwanja wa golf pia karibu na moro hotel...nyumba za kishua ...miti mingi na upepo mzuri...pia rami mwanzo mwisho. Usalama ni mkubwa zaidi ukikompea na kihonda
 
Unaifahamu vyema Bigwa mkuu?
Zaidi ya kupafahamu, nimewahi kuweka stationery huko.
ushamba mwingiii watu wa nanenane, misufini, kigurunyembe wote huko ndo kama kasehemu kao kakuchil.
.
Makanisa huko ndo nyumbani kwao japo kuna nyumba kali sana nafahamiana na Maulid ujenzi mtu mmoja maarufu mazingira hayo.
Siwezi kuishi kwenye watu wafupi wengi na washamba washamba
 
Wewe umejuaje hana hela?

Hivi watu wa jf tukiwa nyuma ya keyboard tunapata wapi huu ujuaji wa maisha ya watu, Ukiwa wewe huna hela unadhani wengine wote hawana?

Yeye kauliza maeneo wewe mwambie, yeye mwenyewe ataenda kujipima.
Hana hela huyo,angekuwa na pesa asingebwabwaja humu JF,mfano,ulimuona wapi Dewji anapiga mikelele.
 
Zaidi ya kupafahamu, nimewahi kuweka stationery huko.
ushamba mwingiii watu wa nanenane, misufini, kigurunyembe wote huko ndo kama kasehemu kao kakuchil.
.
Makanisa huko ndo nyumbani kwao japo kuna nyumba kali sana nafahamiana na Maulid ujenzi mtu mmoja maarufu mazingira hayo.
Siwezi kuishi kwenye watu wafupi wengi na washamba washamba
Huo ni mtazamo wako mkuu.! Ila Bigwa ni miongoni mwa sehemu tulivu zisizokuwa na kelele
 
Mitaaa ya Morogoro hotel kule..
Wakuu, Habari zenu nyote.

Nimehamishiwa Moro kikazi, bado sijaripoti na vile JF ni jumuiya ya watu wengi naomba kupata msaada ya kufahamu maeneo mazuri na salama ya kuishi kwa mkoa wa Morogoro.

Nina familia hivyo nahitaji maeneo ya mazingira salama kwa vile mda mwingi majukumu yangu yananilazimu kusafri.

Hiyo sehemu iwe na maji ya uhakika na yasiwe maeneo yenye vibaka.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom