Ni MAENDELEO AU SIASA?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Naona kuna hoja ya kujibu hapa.
Katika mfumo wa vyama vingi, kila kinachofanywa ambacho awali kilifanywa kwa maendeleo ya nchi na wana nchi, sasa hufanywa kwa malengo ya kisiasa.

Najiuliza,
Mbona ujenzi wa barabara,
Ujenzi wa shule,
Ujenzi wa vituo vya afya,
Kuanzishwa kwa SACCOS,
Ujenzi wa viwanda vidogo,
n.k?
unahusishwa na juhudi za chama fulani kuleta maendeleo?

Je ni maendeleo au ni siasa au ni chama fulani?

Wachambuzi semeni.
 
Makyao,

Tatizo moja ni kwamba tumeingia katika mfumo wa vyama vingi bila kuelewa vyema vyama vingi vina wajibu gani kisiasa. Vyama vya siasa vimekuwa vikiwaza zaidi ni jinsi gani vinaweza kuingia kushika madaraka ya nchi bila kuzingatia maana nzima ya mfumo wa vyama vingi. Matokeo yake vimekuwa vikiona njia ya mkato ya katika kufikia azma ya kushika uongozi wa nchi ni kutumia ama kubebea bango shughuli za maendeleo na kujinadi kwamba vyama vyao vikipewa dhamana ya uongozi ndivyo vyenye uwezo wa kuleta maendeleo hayo na kusahau kwamba maendeleo yanapaswa kuletwa na wananchi wenyewe kwa utashi na muongozi wa Serikali.

Tatizo jingine ni mmomonyoko wa maadili miongoini kwa viongozi wa vyama vya siasa na hata wananchi/wanachama wa vyama hivyo kwa ujumla. Vyama vya siasa kuanza kujipigia debe kwa kuorodhesha masuala ya maendeleo ni kudhihirisha jinsi ambavyo vyama vimekuwa na watu/viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa tayari kusema uongo na ulaghai mwingi ili wafanikiwe kupata wanachotaka.

Ujenzi wa barabara,
Ujenzi wa shule,

Ujenzi wa vituo vya afya,
Kuanzishwa kwa SACCOS,
Ujenzi wa viwanda vidogo,
n.k

ni kazi na shughuli za maendeleo ambazo zinapaswa kufanywa na Serikali ikishirikiana na wananchi kwa ujumla na si jukumu la chama ama vyama vya siasa. Zipo Serikali za kijeshi ambazo mapinduzi yake yaliweza kufanywa kwa manufaa ya umma. Serikali hizo zimeweza kuendeleza shughuli za maendeleo ya nchi bila kuwepo siasa ya aina yoyote ndani yake na bila kuwepo vyama vya siasa. Kwa maana hiyo basi hakuna sababu yoyote ya msingi ya kutaka kuhusisha propaganda za chama fulani katika kutafuta ama kuleta maendeleo nchini. Maendeleo hayaletwi na siasa/propaganda za vyama bali huletwa na juhudi za Serikali iliyo madarakani ikishirikisha wananchi kwa ujumla.
 
Boramaisha,
Haya mawazo yako yangalipaswa kuandikiwa kitabu.Yamejaa falsafa kubwa.
Naamini wachambuzi watayambua na kuleta hoja zao.
Iko kazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom