Ni madhara yapi unayoweza kuyapata ukimrudia msichana uliyeachana naye?

MCHEZA KAMARI

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
561
1,000
Wakuu, kuna msichana mmoja niliachana naye baada ya kugundua kuna vitu anavyo ambavyo ni vikwazo kwangu hivyo nisingeweza kuwa na malengo nae ya mbali, hivyo nikamuacha kibaharia bila ugomvi wala nini ila nikakata mawasiliano

Baada ya kukata naye mawasiliano kwa muda kidogo kama mwaka mzima, siku moja alikutana na rafiki yangu mmoja akamuomba namba yangu ya simu, alianza upya kuwasiliana na mimi.

Niliamua kumueleza ukweli kuwa sihitaji tena mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa sina malengo nae hivyo nisingependa kumpotezea muda wake, lakini yule binti kaamua kunilazmisha turudiane hivyo hivyo hata kama sina malengo naye.

Nimewaomba ushauri marafiki wawili mmoja kaniambia nirudiane naye niendelee kula mzgo hivyohivyo, rafik mwingine kaniambia madhara ya kumrudia mwanamke uliyemwambia huna malengo nae ni makubwa sana, unaweza hata kulogwa(limbwata) upoteze uelekeo au akuletee maradhi.

Bado najiuliza madhara nitakayopata ni yapi au faida nitakazo pata ni zipi pindi nikiendelea naye hali ya kua anajua sina malengo naye
GunFire
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,029
2,000
Maadam huna malengo naye wala nawe vyovyote utakavyofanya ni sawa.
 
Chang’oe

Senior Member
Jun 16, 2013
129
500
Kwa mtazamo wangu hapo kuna mawili

1-Anaweza kuwa sasa amezunguka na kuona kuwa wew ulikuwa wathaani sana.hivyo ameamua kurudi akiwa ameyatoa mapungufu yote ambayo alikuwa nayo.Anaweza akawa mke bora kuwahi kutokea.

2-Aliekuwa nae kwa wakati huu amemzingua amemua kupunguza machungu kwa kukufata wew.Atakuwa masikivu kwa kipindi hiki hata kukuaminisha kuwa unaweza kumuamini kwaajiri ya malengo,lakin ukweli ni kuwa anabuy time.

3-Amerudi kukukomesha na kuharibu misingi yako yote uliyoijenga(mahusiano,uchumi na Afya).

Sasa bora aje kwa njia ya 1 lakin akija kwa njia hizi mbili utajuta.

N.B. hapo naona risk ni kubwa kuliko hasara.Kama hauna mpenzi kwa sasa basi unaweza kumpima kati ya hizo 3 amekuja na ipi.Ila kama una mpenzi,yanin kujichafua ikiwa unaweza kupata mapenzi kwa ulienaye?!!.

Note: kama bado unampenda futa uzi huu mtumie nauli.(maana kma umemenda hata ukipewa sababu hazitokuwa na nguvu).
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
3,872
2,000
Ikitoka imetoka, ikirudi pancha.... sijui ndo walimaanisha nini.

Shoka shoka ekashokelaga na yenge.
 
MCHEZA KAMARI

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
561
1,000
Kwa mtazamo wangu hapo kuna mawili

1-Anaweza kuwa sasa amezunguka na kuona kuwa wew ulikuwa wathaani sana.hivyo ameamua kurudi akiwa ameyatoa mapungufu yote ambayo alikuwa nayo.Anaweza akawa mke bora kuwahi kutokea.

2-Aliekuwa nae kwa wakati huu amemzingua amemua kupunguza machungu kwa kukufata wew.Atakuwa masikivu kwa kipindi hiki hata kukuaminisha kuwa unaweza kumuamini kwaajiri ya malengo,lakin ukweli ni kuwa anabuy time.

3-Amerudi kukukomesha na kuharibu misingi yako yote uliyoijenga(mahusiano,uchumi na Afya).

Sasa bora aje kwa njia ya 1 lakin akija kwa njia hizi mbili utajuta.

N.B. hapo naona risk ni kubwa kuliko hasara.Kama hauna mpenzi kwa sasa basi unaweza kumpima kati ya hizo 3 amekuja na ipi.Ila kama una mpenzi,yanin kujichafua ikiwa unaweza kupata mapenzi kwa ulienaye?!!.

Note: kama bado unampenda futa uzi huu mtumie nauli.(maana kma umemenda hata ukipewa sababu hazitokuwa na nguvu).
Ushauri mzuri mkuu ila sijion kama ninamapenzi nae baada ya kuvigundua vikwazo vyakua na malengo nae ni vingi, licha yakua analazmisha niwe nae hivyo hivyo.
Ahsante kwa ushauri mkuu.

GunFire
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom