Ni madhara gani nchi ya Iran itayapata baada ya jeshi lake "IRGC" kuingizwa kwenye orodha ya magaidi na Marekani ??

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,408
Kuna msemo wa kiingereza husema hivi "mpe mbwa wako jina baya, kisha umuue". Mnamo tarehe 8 mwezi huu Raisi wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba jeshi la mapinduzi la Iran, ambalo ni sehemu ya majeshi ya ulinzi na usalama ya Iran kwamba ni magaidi. Marekani hajafanya haya kwa bahati mbaya na wala hajafanya haya kwa lengo la kutishia tu, kuna kitu kimkakati anachotaka kukifanikisha.

Madhara yako mengi sana kiuchumi, kwasababu jeshi la mapinduzi la Iran lina mkono mkubwa sana kwenye uchumi wa Iran na limejipenyeza kwenye taasisi nyeti za nchi. Hivyo kama wameitwa magaidi basi ina maana Marekani italazimika kupambana na taasisi zote za nchi ya Iran ambazo zinahusika moja kwa moja na hilo jeshi.

Upande mwingine ni kwamba nchi nyingi hasa washirika wake watalazimishwa kuchukua hatua hizo dhidi ya taasisi za Iran kwasababu ni za kigaidi. Sasa jambo kubwa ni kwamba kama jeshi la mapinduzi la Iran wameitwa magaidi, taasisi zote kubwa za kiserikali ambazo zitahusika na kulipatia jeshi hilo pesa kwa ajili ya kujiendesha zitaitwa wafadhili wakuu wa ugaidi (Financiers and Sponsors of terrorism).

Bahati mbaya sana hili halitaishia kwenye jeshi la mapinduzi la Iran peke yake, bali litamgusa hadi Ayatollah mwenyewe kwasababu tofauti na vikosi vingine vya majeshi ya Iran: Jeshi la mapinduzi la Iran ndiyo taasisi ya ulinzi yenye nguvu sana nchini Iran, na haiwajibiki kwa Raisi wala Mkuu wa majeshi, bali kwa Ayatollah mwenyewe. Hivyo basi, tusishangae siku za mbeleni Ayatollah na serikali yote ya Iran ikaja kuwekwa kwenye orodha ya magaidi kwasababu jeshi la mapinduzi ni taaisisi ya kiserikali.

Lakini jambo ambalo linaogopesha sana kuliko yote ni kwamba Iran nao wamesema watafanya hivyohivyo kwa Marekani, naam mpaka sasa Iran naye kasema Marekani ni taifa linalofadhili ugaidi: Kiuhalisia Iran kufanya hivyo halina madhara yoyote kiuchumi kwa Marekani, lakini kijeshi na kiulinzi lina madhara makubwa sana.

Mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo inahusika na kusimamia vita kama ile ya Hague ya mwaka 1907 na ile ya Geneva ya mwaka 1949, inasema dhahiri kabisa kwamba wakati wa vita wanajeshi watalazimika kupigana kwa kufuata sheria na endapo wanajeshi wa nchi zinazopigana watakamatwa basi watakuwa ni mateka wa kivita (Prisoners of war) ambao watatakiwa kuheshimiwa na kutofanyiwa madhara yoyote yale. Lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba mikataba ya The Hague ya mwaka 1907 inakataza matumizi ya baadhi ya silaha wakati wa vita.

Sasa jambo la kitaalamu (Question of technicality) hapa ni kwamba siyo kila mpiganaji wa vita anapewa heshima ya mateka wa vita endapo atakamatwa na adui. Raia wa kawaida ambao siyo wanajeshi lakini wamehusika kwenye vita (Franc-tireurs), majasusi (Spies), magaidi (Terrorists) na Waasi (Insurgents) wakikamatwa hawana kinga yoyote ile ya ulinzi kama ambavyo wanayo wanajeshi wa kutoka kwenye majeshi halali ya nchi: Hivyo hawawezi kupewa ulinzi na heshima ya mateka wa vita (Prisoners of war), na watatakiwa kurudishwa kwenye nchi yao punde baada ya vita kuisha.

NB 1: Sasa baada ya lile tangazo la tarehe 8, popote pale ambapo wanajeshi wa vikosi vya IRGC watakutana na wanajeshi wa Marekani watashughulikiwa kama magaidi na watahukumiwa chini ya sheria za Marekani, hivyo hata kama vita itaisha hawataachiliwa huru bali watapelekwa kule Guantanamo Bay.

Iran imezungukwa na vikosi vya majeshi ya Marekani, kutokea Afghanistani upande wa Mashariki, na Iraq kutokea upande wa Magharibi. Hivyo Iran nao wakikamata wanajeshi wa Marekani hawatawehesabia kama wafungwa wa vita bali magaidi na kuwafungia. Tena hili naomba muondoe wasiwasi maana historia inatuambia kwamba Iran hatashindwa kufanya hivi: kama mwaka 1979 kuvamia Ubalozi wa Marekani na kuwateka mabalozi kwa miaka zaidi ya miwili kinyume kabisa na mikataba ya kimataifa inayolinda mabalozi (The Vienna Conventions on Diplomatic and Consular Relations) unadhani watashindwa kuwakamata wanajeshi wa Marekani na kuwafungia kama magaidi ??

NB 2: Gaidi hatambuliki na sheria za vita, hivyo vita dhidi ya ugaidi haihesabiwi kama vita ya kawaida. Sheria hazitawabana kabisa Marekani na Iran, hapa wataruhusiwa kutumia hata zile silaha zilizokatazwa na mikataba ya kivita. Silaha zilizopigwa marufuku kutumika kwenye vita kama Cluster Munitions, Booby Traps, Dum-Dum Bullets, Blinding Laser Weapons, Nerve Gas na nyinginezo ambazo zimegundulika hatuzijui zinaweza kutumika na Marekani wala Iran wasihukumiwe kwa uhalifu wa kivita kwasababu wote wameitana magaidi.

Haya yalitokea Vietnam na Marekani aliua maelfu ya watu, akatumia hadi Napalm Bombs na alikuwa akikamata mateka wa vita anaua. Mwisho wake wavietnam nao walipowakamata wakina John McCain walikiona cha mtema kuni.

NB 3: Mwisho wa haya yote utakuwa ni upi, ?? Maana hata nchi masikini kama Tanzania ambazo zina Urafiki na Iran zinaweza kupigwa mkwara kabisa kutoshirikiana na serikali ya Iran kwasababu inahusika na kuwafadhili magaidi, ambao bahati mbaya sana ni jeshi lake. Mataifa makubwa kama Urusi na Uchina hayawezi kupangiwa na Marekani lakini sisi tunaotegemea wahisani lazima tukanyage kwa umakini sana.


==================================
UPDATES:
JANUARY 7, 2020.

Iranian MPs declare all of US military ‘terrorist entity’ after General Soleimani killing

The US Armed Forces are now regarded as a terrorist organization under an urgent motion by Iranian lawmakers, who earlier branded the assassination of the Quds Force commander “state-sponsored terrorism,” state media report.

Iranian MPs adopted a bill on Tuesday calling “personnel of the Pentagon, all affiliated companies, institutions, agents and commanders” members of a “terrorist entity,”local media reported.

The bill amends and expands previous legislation which gave a similar designation to US Central Command (CENTCOM). Initiated in April of last year, it was a tit-for-tat response to Washington’s blacklisting of the Islamic Revolutionary Guards Corps (IRGC).

Source: Russia Today

Points of concern:
This Afternoon, the Iranian Legislature has reciprocated the American act, by designating the entire US Armed Forces as a terrorist organisation. Down this path, all American military personnel, including top ranking officials are now potential targets without being accorded any protection emanating from the Geneva Conventions on the law of War and it's Additional Protocols.

This means, both Iran and the US can resort to means and methods of Warfare not acceptable under International law and the Community of Nations: This reminds of me of what Cicero said to Quintus "At the times of war, the law falls silent"
 
Kitendo cha marekani kuendelea kuisakama Iran kunaifanya Iran izmidi kujiimalisha kila kukicha na jinsi Iran inavyo imarika ndiyo inakuwa ngumu marekani kuvamia Iran, na kadiri Marekani anavyo chelewa kuivamia na kuiangusha Iran ndivyo Iran inazidi kuwa taifa lilsilo dhibitiwa kivyovyote vile.

Ninawahakikishia Iran ikija kufanikiwa kutengeneza silaha za nyuklia Marekani itapata tabu sasa hapo mashariki ya kati, maana itafanya inavyo taka na hakuna atakaye dhubutu kukoroma. Sasa hivi Iran licha ya kujitutumua lakini ina woga Fulani kwa marekani hilo ni lazima tuwe wakweli .
 
Una uhakika iran hawana silaha hzo?
Kitendo cha marekani kuendelea kuisakama Iran kunaifanya Iran izmidi kujiimalisha kila kukicha na jinsi Iran inavyo imarika ndiyo inakuwa ngumu marekani kuvamia Iran,na kadiri marekani anavyo chelewa kuivamia na kuiangusha Iran ndivyo Iran inazidi kuwa taifa lilsilo dhibitiwa kivyovyote vile.Ninawahakikishia Iran ikija kufanikiwa kutengeneza Silaa za nukilia Marekani itapata tabu sasa hapo mashariki ya kati, maana itafanya inavyo taka na hakuna atakaye dhubutu kukoroma.Sasa hivi Iran licha ya kujitutumua lakini ina woga Fulani kwa marekani hilo ni lazima tuwe wakweli .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina uhakika 90% Iran wana nuclear weapons haki nawaambia maana sio kwa jeuri hiyo yote unataka kunambia wameendelea sana kinyuklia toka miaka mingi ati washindwe kuwa nazo?

Yaani Israel atishie kuvamia Iran na Israel anazo nyuklia halafu Iran akae tu? Iran anazo aisee.
 
Nina uhakika 90% Iran wana nuclear weapons haki nawaambia maana sio kwa jeuri hiyo yote unataka kunambia wameendelea sana kinyuklia toka miaka mingi ati washindwe kuwa nazo?

Yaani Israel atishie kuvamia Iran na Israel anazo nyuklia halafu Iran akae tu? Iran anazo aisee.
Anaweza akawa nazo lakini kwa siri.
 
If they would wangesema wanayo?
Unafikiria kiburi cha irani ni nn??

Sent using Jamii Forums mobile app
Licha ya kwamba haina hizo silaa lakini INA sila
If they would wangesema wanayo?
Unafikiria kiburi cha irani ni nn??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiburi cha Iran kinatokana na uwezo wa makombora alionao kwa sababu kambi zote za marekani zilizoko mashariki ya kati na ulaya zipo kwenye shabaha yake. Kwahiyo viongozi was Iran wanajua kabisa ya kwamba nilazima marekani ijishauli mara mbili linapo kuja suala la kuivamia Iran, lakini pia Iran ina mtandao mkubwa sana wa wapiganaji kwenye nchi mbalimbali hapo mashariki ya kati kwaa hiyo Iran ina uwezo wa kuivuruga Mashariki ya kati yote.
 
Licha ya kwamba haina hizo silaa lakini INA sila

Kiburi cha Iran kinatokana na uwezo wa makombora alionao kwa sababu kambi zote za marekani zilizoko mashariki ya kati na ulaya zipo kwenye shabaha yake. Kwahiyo viongozi was Iran wanajua kabisa ya kwamba nilazima marekani ijishauli mara mbili linapo kuja suala la kuivamia Iran, lakini pia Iran ina mtandao mkubwa sana wa wapiganaji kwenye nchi mbalimbali hapo mashariki ya kati kwaa hiyo Iran ina uwezo wa kuivuruga Mashariki ya kati yote.
Trust me u r missing big picture hapa
Nayo ni nyuklia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran ana siri kubwa sana kuna miaka alikua anarutubisha uraniam kwa siri alipata upinzani sana toka US na Isrel .Pia Israel alihusika sana kwenye mpango kwa kuua wanasayansi ya Iran waliohusika kwenye mpaka wa kurutumisha Uranium kwenye vinu vya nyuklia.

Kuna uwezekano Iran anamiliki silaha za Nyuklia au yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha silaha hizo mana huu kujiamini na kibri si kawaida.
 
Iran ana siri kubwa sana kuna miaka alikua anarutubisha ufaniam kwa siri alipata upinzani sana toka US na Istraeil.ma Israel alihusika sana kwenye mpango kwa kuua wanasayansi ya Iran waliohusika kwenye mpaka wa kurutumisha Uranium kwenye vinu vya nyuklia.
Muna uwezekano Iran anamiliki silaha za Nyuklia au yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha silaha hizo mana huu kujiamini na kibri si kawaida.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom