Ni mabomu, risasi uchaguzi Bububu, CCM kufutwa? CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mabomu, risasi uchaguzi Bububu, CCM kufutwa? CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 18, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), akiwa amemshikilia mmoja wa wananchi
  kwa madai ya kuleta vurugu wakati wa upigaji kura Jimbo la Bububu,
  Zanzibar jana huku naye akiwaonyesha watu wengine


  Matokeo ya Uchaguzi

  1. Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Ibrahim Makungu, alipata kura 3,371.
  2. mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Issa Khamis Issa, alipata kura 3,204
  3. mgombea wa Chama cha ADC, Zuhra Bakari Mohamed, akiambulia kura 45.
  4. Jahazi Asilia (7),
  5. AFC (6),
  6. SAU (4),
  7. ccr- Mageuzi (3)
  8. NRA kimepata kura moja.


  • Mwandishi mwingine Channel Ten apigwa
  • Mgombea CCM ashinda, CUF chapinga

  Risasi za moto, uharibifu wa mali, kupigwa mwandishi wa Channel Ten Zanzibar, ni miongoni mwa mambo yaliyotawala katika zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu uliofanyika jana mjini Zanzibar. Uchaguzi huo mdogo ulifanyika kuziba nafasi iliyokuwa wazi baada ya kufariki dunia kwa Mwakilishi wa zamani wa jimbo hilo, Salum Amour Mtondoo, Februari, mwaka huu. Vurugu zilianza kutokea mapema baada ya kufunguliwa vituo saa 1:00 asubuhi, ambapo katika kituo cha Beitrasi, risasi za moto zilipigwa na watu waliokuwa wamevaa nguo za kiraia, na kufunika nyuso zao kwa vitambaa vyeusi na vyeupe wakiwa katika gari aina ya Toyota Pick Up. Watu hao waliteremka kabla ya gari kusimama na kurusha risasi tatu hewani na kusababisha watu kukimbia hovyo.

  Askari hao walifika katika eneo hilo saa 7:00 mchana na kutawanya kundi la watu waliokuwa wamekaa upande wa pili wa mlango mkuu wa vituo vya wapiga kura, wakifuatilia watu wanaoingia na kutoka waliopakiwa kwenye magari wakiwa chini ya uangalizi wa askari wa vikosi vya SMZ. Watu kama hao pia walitawanywa katika kituo cha Bububu baada ya kuibuka watu waliokuwa wakiyapekua magari na kuwahakiki waliokuwemo kabla ya kuelekea katika vituo vya wapiga kura, jambo ambalo lilisababisha watu wengi kushindwa kwenda kupiga kura kwa utaratibu wa kusafirishwa kwenye magari maalum.

  Wakizungumza na NIPASHE, baadhi ya watu waliokuwa nje ya vituo wakizuia watu kwa kuwatuhumu kuwa ni mamluki, walisema kwamba haiwezekani mkazi halali wa jimbo apelekwe kwa magari wakati vituo vipo mita chache kutoka maeneo wanayoishi. "Hawa wanaokuja ndani ya magari hatuamini kama ni wakaazi wa Bububu, ndiyo maana tunazuia magari kuingia katika vituo vya wapiga kura na watu," alisema Rashid Juma, mkazi wa Beitrasi.

  Wakati waandishi wakitoka katika kituo cha Beitrasi kuelekea Bububu, walikuta gari eneo la Kibweni likivunjwa vioo kwa kutumia mawe na magongo kisha kuendeshwa na kuligonga katika vikuta vilivyopo pembezoni mwa barabara kabla ya kurudi nyuma mbio na kuligonga gari la abiria. Gari hilo aina ya Toyota Vitz lenye namba za usajili Z 979 DR, lilifanyiwa uharibifu mkubwa mkabala na Ikulu ndogo ya Kibweni, ambapo Mwandishi wa Channel Ten Zanzibar, Munir Zacharia, aliegesha gari lake pembeni na kushuka kupiga picha, lakini ghafla alivamiwa na kundi la vijana waliokuwa wamekusanyika nje ya tawi la CCM na kuanza kumpiga ngumi na kumjeruhi mdomo na sehemu ya bega.

  "Mnyang'anyeni kamera, apigwe, hapana mwacheni, toa kaseti hiyo, futa mkanda huo," zilisikika sauti za vijana hao kabla ya askari Polisi waliokuwa katika gari PT 1449, kufika eneo hilo na kumwokoa mwandishi huyo kisha wakampakia katika gari lao na kuondoka naye. Askari hao baadaye walilichukua gari la mwandishi huyo aina ya Toyota Spacio lenye namba za usajili Z 623 DR na kumuondoa katika eneo la tukio kwa usalama wake. Juni 2, mwaka huu, mwandishi mwingine wa kituo hicho cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliuawa kwa kupigwa bomu akiwa kazini katika kijiji cha Nyololo Wilaya Mufindi mkoani Iringa.

  Akizungumza na NIPASHE, Zacharia alisema kamera imeharibiwa, pochi imeibiwa na kupigwa ngumi mdomoni na mabegani. Alisema alikwenda kuripoti kituo cha Polisi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za matibabu. "Nashindwa kuelewa kwa nini wananipiga wakati natekeleza majukumu yangu, hilo ni tukio baya katika misingi ya demokrasia na utawala bora," alisema Zacharia.

  Msimamizi wa Uchaguzi katika kituo cha Beitrasi, Abdullah Bakari Khamis, alisema zoezi hilo lilianza saa 1:00 asubuhi ambapo makundi ya watu yalijitokeza mapema na kupiga kura, lakini wakati wa mchana vituo vingi vilikuwa vitupu, ama vikiwa na wapiga kura mmoja mmoja. Alisema kituo hicho kilikuwa na vyumba vya wapiga kura wanane na hakukuwa na matatizo yoyote hadi mchana mbali na matukio yaliyokuwa yakijitokeza katika lango kuu la kuingilia kwa kusheheni askari wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wakiwa na silaha za moto kuimarisha ulinzi eneo hilo.

  Msimamizi wa kituo cha Bububu, Maalim Mussa, alisema hadi mchana zoezi lilikuwa linaendelea vizuri na watu walianza kujitokeza tangu saa 1:00 asubuhi kituoni hapo. Hata hivyo, alisema majina ya wapiga kura yalibandikwa vituoni wiki moja kabla ya uchaguzi huo, lakini wananchi wengi hawakujitokeza kuyasoma ili kuhakiki na kujua wamepangiwa chumba namba ngapi. Kutokana na mparaganyiko huo, maafisa wa uchaguzi waliwasaidia kusoma majina yao na kutambua vyumba walivyopangiwa na kuhakikisha watu wote wanapiga kura kama ilivyopangwa.

  Matukio hayo yanatokana na mchuano mkali kati ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Makungu na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Issa Khamis Issa, kila upande ukipigania ushindi ambapo wafuasi wa wagombea hao walikuwa na mivutano mikubwa hasa katika suala la wapiga kura halali na wale wanaopakiwa katika magari maalum na kufikishwa katika vituo vya kupiga kura.

  Mwangalizi mmoja wa uchaguzi kutoka CCM, Thuwayba Kisasi, alilaani kitendo cha makundi ya watu kuzuia watu wengine kwenda kupiga kura wakati siyo makarani wa uchaguzi wala mawakala wa vyama na kuongeza kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa chimbuko la vurugu.

  Mwangalizi wa uchaguzi kutoka CUF, Habib Mohamed Mnyaa, alisema kuna michezo michafu ambayo imetia doa zoezi la uchaguzi huo ikiwemo mtu halali kuingia katika kituo na kukuta jina lake limeshatumika kupigwa kura na watu wasiojulikana. Hata hivyo, Mnyaaa ambaye ni Mbunge wa Mkanyageni, alisema jambo la kujiuliza inakuwaje mtu aingie katika kituo cha wapiga kura akiwa na kitambulisho ambacho hakina picha yake na kufanikiwa kupiga kura.

  Mgombea wa ADC, Zuhura Bakari Mohamed, alisema atakuwa mzito kuyatambua matokeo kutokana na mkasa alioshuhudia kuwa unakwenda kinyume na taratibu za uchaguzi. Alisema saa 6:20 yaliingia magari matatu ya vikosi vya ulinzi na usalama yenye namba za usajili 2609 JW 97, 20606 JW 97 na KVZ 109 ambayo yalikuwa yamepakia watu wasiopungua 30 na kutoweka baada ya kukamilisha kazi ya kupiga kura katika kituo hicho.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohamed, hakuwa tayari kuzungumzia matukio ya vurugu likiwemo la kupigwa kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten. "Niache nina kazi mkononi," alisema Kamanda Mohamed, baada ya kupokea simu yake ya kiganjani kisha kuikata.

  Kuhusu kuimarishwa askari wa vikosi wakiwa na silaha za moto katika milango mikuu ya kupitia wapiga kura, katika kituo cha Beitrasi na Bububu, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari, alikataa kuzungumza chochote kwa maelezo kuwa waandishi ni mashuhuda wa matukio hayo.

  Abubakar ambaye alikuwepo katika vituo vya kupigia kura akiwa kama Mwangalizi kutoka CUF, alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kutakiwa kuelezea misingi ya demokrasia na utawala bora katika uchaguzi. "Nimekwambia sitaki kuzungumza au hufahamu Kiswahili nikueleze kwa Kiingereza?," Alihoji waziri huyo aliyekuwa akitoka msikitini uliopo kituo cha kupigia kura cha Beitrasi eneo la Chuo Kikuu cha Ualimu cha Nkrumah.

  Wakati zoezi hilo lilipokuwa likielekea ukingoni, vurugu ziliendelea kutawala katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, ambapo matairi ya magari yalichomwa moto barabarani na mawe makubwa kutumika kufunga njia karibu na kituo kikuu cha Polisi cha Bububu. Aidha, risasi za moto nazo zilirindima katika maeneo mbalimbali, kujaribu kuwatawanya watu waliokuwa karibu na vituo wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi huo na kuzuia magari yaliyopakia watu katika maeneo ya vituo vya kupigia kura.

  Hata hivyo, wakati wagombea wa vyma vingine wamekubali matokeo hayo, CUF wameyapinga kwa madai kwamba taratibu kadhaa za uchaguzi zilikiukwa.
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  ITV walikuwa wakionyesha habari kama summary ya wiki, wakati mbowe anaongea kuhusu Tendwa na TBC basi habari ikapatikana kuhusu CCM kuleta fujo.What a wonderful coincidence.Tendwa katendwa na kutendeka, katupiwa mpira sasa ni vipi ataucheza?CDM watamuuliza kila kukicha yeye ndie ajitete na kuitetea CCM in public na kuthibitisha madai ya CDM.SIku ya kufa CCM mamluki wote huteleza na kupwaya.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Ndilo ninalojiuliza, maana Chadema ingeshiriki uchaguzi huu lawama zote zingeelekezwa kwa Mbowe na Slaa. Mungu ndiye anayeongoza mageuzi nchini, kwani sijapata picha Chadema walivyoamua kutoshiriki na sikujua hoja yao, lakini leo naona kosa lenye heri lilivyowakwepesha na mbinu chafu za serikali na CCM.

  Tendwa analitolea kauli gani tukio la vurugu za uchaguzi huko visiwani ambako Chadema wanaodaiwa kuwa waleta vurugu hawakujihisisha na uchaguzi huo? Hata kama ni ugomvi ndani ya nyumba kati ya mume na mke, lakini wagombanapo mafahari wawili nyika huumia.
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tendwa ndio wazee walioishiwa sifa za kuwa viongozi ndani ya nchi ni bora kupumzika na kuachia vijana wanaweza leta mabadiliko
   
 5. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,771
  Likes Received: 2,673
  Trophy Points: 280
  Hii yaweza kuwa ni majaribio ya mbinu mpya ya ukuvuruga matokeo, pakia watu kwenye magari peleka kwenye kituo cha uchaguzi hakikisha anapigia kura mgombea wa chama kinachotalazimisha kushinda.

  Kwa hiyo mtindo wa kulinda kura haufui dafu hapa. Designers wa mbinu za kulinda kura rudini Designing room, kazi mpya imeletwa.

  Kwa matukio haya kimbunga cha machafuko yasiyo na kikomo kinakuja miaka michache ijayo.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mimi nachukulia watu wanaoelezea siasa za Tanzania katika mifano ya ndoa, mke mume, dada, kaka kama watu wasioelewa/ wasio weledi wa siasa.
  Je ni Tanzania tu ndio kuna hizi ndoa?

  Naelewa ni utamaduni wetu mbovu au mazoea ya kuona kina mama( mama zetu) ni dhaifu katika mahusiano ya kindoa. Utamaduni wa kiafrika wa kudharau mwanamke. Sasa hilo linapoingia katika siasa pia basi uelewe, wahusika wana uelewa finyu wa siasa, mikakati ya kisiasa na hali halisi za kisiasa katika jamii husika kwa wakati huo.

  Hivi Cameroon ameolewa na nani kule UK? Au Cameroon amemuoa nani ?

  Link mumemke link mkemume

  Mugabe ameolewa na Morgan Tsvangirai? au MDC imeolewa na ZANU PF?

  Link ndoa

  Huu naona ni udhaifu na ushabiki wa "kipuuzi". Pia ni kuonesha kuwa hatuko makini.

  Je ikitokea siku na huku bara tukaihitaji hiyo ndoa, tutakuwa na uwezo wa kuramba matapishi yetu?
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  CCM katika uchaguzi huru na wa haki hawawezi kushinda!!!

  Kuna watu hawaelewi dhana ya chama dola kwa Tanzania ni CCM tu imejipa hadhi hiyo.
  Tume za uchaguzi kama zilivyo leo ni vyombo vya kuisimika CCM madarakani. Polisi ndio mlinzi wa CCM, TISS, Tendwa...yaani CCM wamejiwekeo mfumo ambao unawahakikishia kuwa "wanashinda kwa kishindo" na sio kuchaguliwa kwa kura.

  Ndio pale inapokuwa muhimu kwa vyama vya upinzani kushirikiana( hapa sizungumzii kuungana). Kuna mambo mengi wanayoweza kuyafanya pamoja ili kutandika mfumo sawia kwa vyama vya siasa.

  Ni wazi,tutaingia katika machafuko kama utaratibu huu wa kihuni utaendelea pia tutegemee CCM wataendelea kuvitendea vyama vyengine mizengwe. na kung'ang'ania madaraka ya shamba la bibi.
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sasa tutajua mwisho wa ndoa ya CCM na CUF. Maana kwa kuchezewa mchezo huu mchafu huenda watastuka ingawa ni vigumu kutokana na CUF mwenyewe kupewa umakamu wa rais ingawa he is but a white elephant. Sana sana anaambulia makombo na sifa za kipuuzi. Nadhani mwamjua jamaa mwenye madevu na tamaa hakuna duniani.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,419
  Likes Received: 81,466
  Trophy Points: 280
  Hizi ni mvua za rasharasha tu...Tusubiri kivumbi kinakuja 2015...Nchi itawaka moto.

  Quote:
  "I am no Cassandra, but, mark my word, people will die."

  ~Jenerali Ulimwengu
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo Katibu Mkuu wa CUF supu za serikalini zimemliwaza na kumlewesha kabisa, hana nafasi ya kukipigania chama chake, ni Lipumba anahangaika pekee.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukisikia ndoa za mkeka ndo hizi, kwani mioyo haikukutana kwa dhati, ila shinikizo ndilo lililowalazimisha kukaa pale mkekani. Aliyewashinikiza ana bado nafasi ya kuwapatanisha?
  Mwafaka ni kitendawili, hatujui waliafikiana nini na imekwuaje leo matokeo ya uchaguzi wanaanza kukorofishana katika ndoa yao.
  Je, ni halali waliofanya mwafaka kisiasa kushtakiana kuhusu kuzidiana kete katika upigaji kura?
   
Loading...