Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
492
1,000
Ni mabadiliko sahihi yanayoenda kuboresha utendaji wa kazi ndani ya mikoa yao na serikalini kwa ujumla

Mheshimiwa mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, mara kadhaa amekuwa ni mtu wa kutoa kauli tata sana kwa lugha nyepesi ni mropokaji, kwa nafasi yake kama mkuu wa mkoa sio busara sana kuwa mropokaji

Kwa upande wa Mheshimiwa Ally Salum Hapi, alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Tabora huku mama yake mzazi ni mtumishi kwenye moja ya halmashauri ndani ya mkoa wa Tabora

Yaani, mtoto alikuwa ni bosi wa mama yake mzazi(kama binadamu kungeweza kuwa na changamoto kidogo)

Hii inanikumbusha awamu ya tatu ya hayati Rais Benjamin Mkapa, alipomteua Dr. Asha Rose Migiro kuwa waziri wa maendeleo ya wanawake, jinsia na watoto na wakati huo huo akamteua mama Mwantumu Malale kuwa katibu mkuu kwenye wizara hiyo hiyo (maendeleo ya wanawake, jinsia na watoto)

Mheshimiwa Dkt. Asha Rose Migiro na mama Mwantumu Malale nni mtu na dada yake kabisa, Mwantumu ni mkubwa na Dr Asha Rose ni mdogo, yaani mdogo alikuwa bosi wa dada yake

Mheshimiwa Mkapa alipogundua hilo, alimuamisha mama Mwantumu haraka sana kutoka kwenye wizara hiyo

Kwa upande wa Dkt. Batilda Buruhani, yeye ni mwanasiasa aliyekuwa mbunge na pia waziri kwenye serikali ya awamu ya nne

Alipoteuliwa kuwa katibu tawala wa mkoa (Regional Administrative Secretary) nafasi ya utumishi wa umma kwa mwanasiasa haikuwa nzuri sana

Ila sasa kwenda kuwa mkuu wa mkoa (political post) ni sahihi kabisa, kwa sababu mkuu wa mkoa ni nafasi ya kisiasa

Ni mabadiliko yenye tija kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom