Ni mabadiliko gani ambayo ungependa kuyaona katika kipindi kijacho cha miaka 5? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mabadiliko gani ambayo ungependa kuyaona katika kipindi kijacho cha miaka 5?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyani Ngabu, Jul 28, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, ungependa kuona mabadiliko gani ya kweli kutoka kwenye serikali mpya itakayoundwa? Mimi binafsi ningependa kuona mabadiliko mengi lakini nitaanza na hili la mawaziri kuwa wabunge.

  Sina uhakika katiba inasemaje kuhusu hili jambo lakini kwa mtazamo wangu mimi naona ni utaratibu usio na akili. Ubunge ni kazi ambayo ni 'full time'. Vile vile uwaziri ni kazi ambayo ni 'full time'. Hivi mtu unawezaje kweli kufanya kazi zote hizo mbili kwa ufanisi? Kwa hali ya nchi yetu kazi ya ubunge si lelemama. Ni kazi ambayo inayohitaji muda, nguvu, na juhudi za mbunge kwa wakati wote.

  Uwaziri na wenyewe si mchezo wa watoto wadogo. Leo uko huku kesho uko kule, keshokutwa umeenda sijui wapi kusaini mikataba, mwezi ujao umehudhuria sijui mkutano gani. Sasa waziri aliye mbunge atapata wapi muda wa kufanya kazi jimboni kwake?

  Ili kuleta na kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa serikali yetu na wawakilishi wetu bungeni, mimi ningependelea, iwe Dkt. Slaa au Kikwete, yeyote yule kati yao atakayeshinda kiti cha uraisi atumie nafasi yake hiyo kwa mujibu wa sheria kutuletea mabadiliko ya kweli ambayo tutayaona kwa macho yetu na mojawapo ni hili la uwaziri na ubunge. Kama raisi hana nguvu za kisheria za kubadilisha utaratibu huu basi atumie 'bully pulpit' ya taasisi ya uraisi na kushawishi kuondolewa kwa utaratibu huu.
   
 2. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mie ningependa baraza la mawaziri lipunguzwe.
  2. Misafara ya nje ya nchi waende wale wahusika tu sio msururu mrefu wa watu.
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono kuhusu mbunge asipewe kazi ya uwaziri, pili napenda kuona serikari ikiwa na mawaziri wachache kadri iwezekanvyo, kuwe na magari maalumu ya serikari siyo haya mashangingi yanayotutia umasikini, ukubwa wa bunge pia upungue, maana tunawabunge karibu sawa na USA ambayo ina watu zaidi ya 270,000,000 wakati sisi tuko tu 42,000,000 na tu masikini wa kutupwa, mikataba yote ya madini ifutwe, waarabu kule Loliondo waondoke nk
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Acha CHUKI BINAFSI
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi ningependa sana misele ya nje isipigwe saaaaaaaaana maana wenzetu jirani hapo wapigi pigi misele na wanatupiga bao kimaendeleo wanazidi kupaa cha msingi nikukomaa hapa hapa home mitaji mbona tunayo kwa nn tusikomae.
  Alafu atakae boronga kwenye kitengo flani anapaswa kutemwa sio kumpleka kule nako anaboronga tena unamrudisha huku nako anavurunda hii ya kubebana iwe mwisho.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  We DDT ndo dawa yako pekee ya kukupoteza.
   
 7. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mimi ningependa kuona serikali ikiacha kugharimia magari ya wabunge (na mengine mengi tu ya watendaji wa serikali). Kwa mawaziri, wakuu wa mikoa sawa, wengine wote no. Serikali inatumia mabilioni ya pesa kwenye gharama za mafuta na uendeshaji wa magari haya (mengi ya kifahari) wakati nchi ni maskini.
   
 8. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Malengo ya dhati na ya kueleweka (sio mapambio kama ya kilimo kwanza) yapewe kipaumbele cha kweli na usimamizi wa kweli ufanyike.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kubwa ni kuona mafisadi wote wananyongwa na RA anarudishwa kwao mashariki ya kati!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono kwa hili. Katiba yetu inasema kuwa Waziri ni lazima awe mbunge lakini naamini hilo nui kosa. Kimsingi, moja ya kazi kubwa za Bunge ni kuisimamia serikali inapotekeleza majukumu yake. Kazi hii hufanywa na wabunge.
  Kwa kumfanya Mbunge kuwa waziri maana yake ni kumwondoa kutoka kwenye kazi ya kuisimamia serikali mpaka kuwa mtekelezaji wa majukumu ya serikali. Haiwezekani tena kwa mtu huyu kuisimamia serikali kwa sababu yeye mwenyewe ndiye mwenye wajibu wa kutekeleza majumkumu ambayo anatakiwa ayasimamie.
  Lakini pia, Mbunge anafanya kazi ya kuwawakilisha wananchi wake. Unapomchagua kuwa waziri, ina maana unamwondolea kwa kiasi kikubwa jukumu hilo kwa sababu muda mwingi atautumia kufanya kazi za serikali.
  Nadhani kuna haja ya kwua na mfumo mwingine utakaophakikisha kuwa hakuna mwingiliano wa kimaslahi baina ya bunge na serikali
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  First 100 days:-
  1. Mifisadi wote wanafikishwa mbele ya sheria na kuua kabisa mtandao na vyombo vyote vilivyokuwa affiriated with. Freeze account na confiscate mali zao hadi hukumu zitakapo tolewa.
  2. Miiko na maadili ya Azimio la Arusha yanarudishwa na taasisi zake kuwa huru.
  3. Katiba inafanyiwa marekebisho makubwa kuhusiana na Uchaguzi kufuta vyama utitiri visivyokuwa na Itikadi na kutangaza dira ya Taifa ambayo itikadi za vyama zitabase mtazamo wa falsafa zao.
  4. Kuunda baraza la senators ambalo ndilo litakuwa juu ya maamuzi yote ya mapendekezo ya bills za Kitaifa.. Hawa watateuliwa au kuchaguliwa kwa kuzingatia mustakabali wa Taifa (dira)..
  5.Kupunguza madaraka ya rais ktk majukumu yake, kama kuteuwa majaji, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, taasisi na mashirika ya Umma pasipo kupitishwa na Senate.
  6. Kuwepo na Uchaguzi mdogo (kikatiba) kila baada ya miaka miwili (kura za maoni) kwa wawakilishi na watendaji waliochaguliwa ikiwa wameshindwa kufikisha maendeleo kwa wananchi kama walivyoahidi.
  7. Suluhisho la kudumu kuhusiana na Muungano wetu.
  8. Mpango wa muda mrefu wa kiuchumi unaozingatia zaidi maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania na sio missionaries au misaada. Maslahi ya Taifa yatalindwa na Watanzania hivyo nguvu ya uwekezaji iwe mikononi mwa wazawa na wageni watakaribishwa tu ktk kukuza uzalishaji nchini na sio kuuza mali zao kama tunavyoona Wachina wa Kariakoo.

  Na mengine mengi ambayo ni sera za mrengo wa kulia kwa sababu hatuwezi kugawana Umaskini isipokuwa kukuza uchumi uliopo kwanza tuvuke bar ya umaskini..
   
 12. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tume ya uchaguzi iwe huru, hakuna mtu kuteuliwa na rais, PCCB iwe huru hakuna mtu kuteuliwa na rais bunge pekee liteue boss wake, Jamani elimu karibu 50% ya watz hawana elimu hivyo ni muhimu kupunguza gap, jamani hizi international school hazifai, zinajenga matabaka, kwa nini tusiwe na mfumo mmoja wa elimu kuliko kuwa na watu wengine akina kayumba wengine akina Elly.

  Jamani, kunahaja ya kumega kidogo ubepari, kumega kidogo usocialism, harafu tukawa na mfumo wetu wa kuiendesha badala ya sasa full ubepari ambao hata marekani kwenyewe unawashinda.

  Tuendelee kutaja.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mimi ningependa kuona mabadiliko ya katiba yakifanyika.Tanzania inahitaji katiba mpya si katiba viraka kama wanavyofanya sasa.

  Mabadiliko ya katiba amabyo ningependa yafanyike mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 ni kama ifuatavyo.

  [1] Kupunguza madaraka ya Rais wa JMT.Rais wa Tanzania ana madaraka makubwa kupita kiasi,suali hili liliwahi kutamkwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl J K Nyerere sikumbuki hasa alikuwa akihutubia wapi lakini alisema kwamba tukimchagua Rais dikteta katiba yetu itamlinda au Rais akiamua kuwa dikteta vipo vifungu vingi vya katiba ambavyo vingemlinda.

  Rais wa Tanzania ni mwajiri mkuu wa wafanyakazi wote wa serekali ingawa haitaji kura zao,Rais amepewa madaraka ya kufanya uteuzi wa baraza la mawaziri kwa kushauriana na waziri mkuu.kuteua mkuu wa majeshi ya ulinzi [JWTZ] bila kuthibitishwa na chombo chochote.Mkuu wa jeshi la polisi,wakuu wa mkoa yote Tanzania bara,wakuu wa wilaya wote Tanzania bara,Jaji mkuu na majaji wote wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu,Makatibu wakuu wote wa mawizara Tanzania bara,makatibu tawala wote Tanzania bara,Makamishna wa tume ya uchaguzi,Mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali,mwanasheria mkuu wa serekali na wakuu wote unaowajua bila kuthibitishwa au kupigiwa kura na chimbo chochote.Haya madaraka ni makubwa sana kumlimbikizia mtu mmoja tena bila ya kuwa na chombo chochote cha kuhoji teuzi za Rais.Marekani Obama akifanya uteuzi wa wakuu eg mwanasheria mkuu lazima athibitishwe na baraza la seneti.Bila shaka wamarekani wanajua Rais wao ni mwanadamu wa kawaida anaweza kufanya uteuzi kwa pendeleo au kwa maslahi yake binafsi.Tanzania tumeshuhudia mara kwa mara marais wetu tangu enzi za Mwl Nyerere mpaka zama za Muungwana wakiteuliwa watu kwasababu tu kujuana au kulindana.

  Ningependa katiba yetu ikifuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao hawana kazi za kufanya zaidi ya kufuja fedha kidogo za walipa kodi.Ningependa kuona teuzi zote za wakuu mbali mbali zikithibitishwa na bunge ili kuepuka watu wa hovyo kuendelea kuwamo katika safu za uongozi.Ningependa kuona baraza la mawaziri linakuwa dogo sana ikiwezekana mawaziri wasiozidi kumi na tano,si lazima kuwepo na manaibu waziri katika kila wizara.

  Ningependa kuona safari za viongozi zikipunguzwa maradufu,kazi zingine zifanywe na mabalozi walioko huko ughaibuni.

  Ningependa kuona Tanzania ikichukua tahadhari kubwa kuelekea shirikisho la EAC kwasababu nchi zote wanachama zina matatizo ambayo yanaweza kuhamishiwa Tanzania.

  Ningependa kuona Tanzania ikiacha kuuza ardhi kwa nchi zenye ukosefu wa ardhi eg kenya,Korea,nchi za kiarabu na nk.

  Ningependa kuona Tanzania ikipitisha sheria ya kifo/kifungo cha maisha kwa wahujumu uchumi na mafisadi,hili si jambo geni wenzetu wachina wamefanya hivyo ndio maana China imepiga hatua kubwa kiuchumi.
  Mwisho mabadiliko haya hayawezi kufanywa na Muungwana na chama chake hata siku moja labda Dr Slaa kidogoooo anaweza kujaribu.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mimi ningependa kuona SIASA SAFI NA UONGOZI BORA IN REALITY..
  1. Uwanja wa ushindani uwe sawa, vyama vyote viweze kushiriki sawasawa,
  2. Vyama vya siasa viwe na ukweli na siyo kudanganya wananchi- hii ina maana vyama vyote kikiwemo tawala viweke maslahai ya wananchi wote mbele na siyo matakwa na maslahi ya " wenye chama chao"
  3. Nafasi za uongozi zizunguke - ukiritimba kwenye uwaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi uondoke.Nafasi za kitaalamu ziwe za mikataba.Performance based na siyo vinginevyo
  4. Non- performancers waondolewe mara moja bila kuoneana aibu
  5. Kuwepo na Diversity kwa maana halisi katika uongozi na fursa mbalimbali - balance in terms of dini/imani za watu, makabila, umri, jinsi, etc
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Well..

  Mabadiliko ya Katiba hayatofanyika - siyo sera ya CCM (hii inajibu hoja zote za mawaziri, n.k n.k)
  Ufisadi utaendelea kuwepo kwa "zaidi" - kila mashine inahitaji nishati yake kuiendesha

  Kwa kuchagua kile kile (CCM) matokeo yatakuwa yale yale (tuliyokwisha yaona). Anayefikiria kuwa atapata fotauti hana msingi wa kufikiria hivyo.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  My friend...you have finally come around! Where have you been in all these years?
   
 17. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  1) Serikali iache kununua samani kutoka nje - Iweke mazingira mazuri kwa watengenezaji wadogo wa samani kama Loan guarantee scheme kwa ajili ya mashine za kisasa na mafunzo. Inasikitisha kuona mpaka ofisi ndogo za halmashauri zinanunua samani kutoka Dubai

  2) Matumizi ya serikali na mikataba ziwe kwenye public domain - Ufisadi mwingi umechangiwa na usiri mkubwa wa serikali kama ujenzi wa Twin towers. Kujaribu kupunguza hilo tatizo Serikali ifanye mambo yake kwa uwazi zaidi e.g safari na matibabu ya nje nchi, mikataba.

  3) Kuvutia wawekezaji kwenda mikoani - kuwapa tax break.
   
 18. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ningependa turudi nyuma kwanza back to the basics, apatikane mtu mwenye busara na uzalendo wa Nyerere tumpe nchi kwa mantiki ya kuirudisha nchi mikonomi mwa watanzania na kuwaunganisha upya through true democracy, expensively investing in education and distributing the powers of authority in other sectors such as the police force and the judiciary.

  Apewe nchi for the next twenty years or so if possible awe ruthless na vision ya kutuacha tunapoweza jitegemea kifikra, taifa alijengwi na wachache bali michango ya wengi kama CCM inaenda kushinda this tells us the mental state of average Tanzanian. We havent matured as an independent nation na tunarudisha 'ubwana mkubwa' through political elites. Kibaya zaidi these bozzos dont make the effort to learn on what they aspire to become, yaani JK anapita kwa 99% of party support either watu njaa, waoga au hatujali maslahi ya wengine.
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  NN ameuliza swali zuri na wengi tunajua nini tungependa. Lakini i can assure you things will get worse, usanii kwa sana nothing will move on.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  WomenOfsubstance,
  Duh! hiyo number 5 kidogo inanipa mashakamakubwa kwni tukianza hivyo kutakuwa na mashaka makubwa ktk kutazama uwezo wa mhusika. Zaidi ya hapo mengine yote bomba..
   
Loading...