Ni maamuzi gani unapaswa kuchukua pale role model wako anapobadili msimamo?

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Habari wanajamvi, hope mu wazima wa afya.

Kuna Jambo nahitaji kuwekwa sawa, kama kichwa cha habari kinavyojieleza

Je, ni maamuzi gani unapaswa kuchukua pale role model wako anapobadili msimamo wake.

Maana ni wazi kila mtu duniani kote ana mtu anaye muinspire,hamasisha kwa mambo kadha wa kadha iwe

Uongozi,mavazi, haircuts, airdressing, na lifestyle mbalimbali.

Inawezekana unamuiga mtu kwa staili yake ya kuongoza, lakini ghafla akabadili utaratibu ambao ni vigumu kwako yaani upo njiapanda

Au unahamasika na maisha ya mtumishi fulani wa Mungu, lakini anabadilika na kuwa mlevi wa kutupwa

Au unavutiwa lifestyle ya msanii au muigizaji flani iwe Bongo au Ulaya yaani mtu amekufanya uingie kwenye hiyo tasnia lakini baadaye anautangazia umma kwamba.

Alichokuwa anakifanya ni haramu au dhambi, je ni hatua zipi unatakiwa uchukue,na wewe upo kwenye mtandao huo?

Sina maana, huwezi bila yeye maana ni mtu ambaye unaiga tu principle zake hata hakujui.

NB:my role model kwa hapa bongo ni mzee Edward Lowassa usiulize kwanini,japo suala la yeye kuhamia upinzani aliniacha kwenye mataa

Ughaibuni ni Abraham Lincoln mmoja wa walio kuwa presidents wa USA.

Corona ipo na inaua, chukua tahadhari
 
Binafsi sina role model mmoja.

Ila kuna mambo role model akifanya, na bullshit directly.
 
Sasa kwa mfano mimi Lucky Dube atabadili vipi msimamo wake wakati ni marehemu?

Nawashauri vijana pendeni kuwa na maroli modo ambao ni marehemu tayari.

Kuwa na lorimodo ambae hajafa unaweza kushangaa akabadili msimamo kuwa shoga. Sijui na wewe utabadili au vipi 😀😀
 
Back
Top Bottom