Uchaguzi 2020 Ni Maajabu: CCM inajua kuna wagombea wamepita kwa kutoa Rushwa ila TAKUKURU hawajamkamata hata mmoja nchi nzima

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Inachekesha Sana kwamba Kama nchi tuna chombo Cha kupambana na Rushwa Ila Hadi Leo tunavyoongea Hakuna mtia Nia wa chama chochote aliyepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kugawa Rushwa ingawa Rushwa imetembea wazi wazi

Cha kushangaza zaidi CCM Wana taarifa za baadhi ya wagombea kupitishwa kwa kutoa Rushwa Ila TAKUKURU hawana hizo taarifa kwani Kati ya walioongoza kura za maoni Hakuna aliyepo mahakamani kwa kesi ya rushwa
 
Inachekesha Sana kwamba Kama nchi tuna chombo Cha kupambana na Rushwa Ila Hadi Leo tunavyoongea Hakuna mtia Nia wa chama chochote aliyepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kugawa Rushwa ingawa Rushwa imetembea wazi wazi.

Maafisa wa Takukuru nasikia huko kanda ya ziwa wote wameagiza magari mapya baada tu ya kura za maoni kupata wagombea wa CCM
 
Inachekesha Sana kwamba Kama nchi tuna chombo Cha kupambana na Rushwa Ila Hadi Leo tunavyoongea Hakuna mtia Nia wa chama chochote aliyepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kugawa Rushwa ingawa Rushwa imetembea wazi wazi.
Cha kushangaza zaidi CCM Wana taarifa za baadhi ya wagombea kupitishwa kwa kutoa Rushwa Ila TAKUKURU hawana hizo taarifa kwani Kati ya walioongoza kura za maoni Hakuna aliyepo mahakamani kwa kesi ya rushwa
Walipogeuka kuiita RUSHWA TAKRIMA JE HAMKUJUA kuwa WAMEIRASMISHA...
 
Taasisi nyingi nchi hii zipo kwa ajili ya wapinzani tu.
Msahafu wa Wakristo unasema kuwa siku moja wayahudi walimleta kwa Yesu mwanamke aliyekamatwa laivu akizini. Nadhani mwanamume alifanikiwa kuwapiga chenga. Wakataka maoni ya Yesu maana adhabu yake ilikuwa kuuwawa kwa kupigwa mawe. Yesu akawaambia "Yeyote asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga mwanamke huyu mawe." Wakasepa mmoja baada ya mwingine. Ndugu yangu mmoja anafanya kazi Takukuru. Aliniambia, "Nani alikudanganya kuwa sisi hatutaki pesa? Zikija upande wangu ni riziki Mola kanipa!" Na kweli. Jamaa ana majumba na magari kadhaa!!! Nani amkamate nani! Hakuna mwema kati yao wote wameoza.
 
Dr. Walter Rodney ktk kitabu chake ... How Europe Underdeveloped Africa ... anasema (kwa tafsiri ya kiswahili) ... Ukiona mhudumu wa Ofisi anaiba rimu ya karatasi, usijisumbue, siyo yeye; Na ukitaka kudhibiti wizi na kuimarisha maadili kazini, panda juu kwa Katibu Mkuu wa Wizara kwani huko ndiyo kuna uozo mkubwa ... Hakuna Mtumishi mwajiriwa anayeweza kufanya vizuri au vibaya isipokuwa amemwona wa juu yake (Boss) anafanya.
Inasemekana, (mie binafsi sina ushahidi kwani sijawahi pata tatizo na Takukuru) Takukuru inaongoza kwa ku-promote rushwa Nchini.
Habari ndiyo hiyo.
Ni vigumu sana kwa rushwa kukomeshwa ktk Nchi nyingi za Africa kwa sababu Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zipo zinastawi na kufaidika na mifumo ya rushwa. Bila rushwa haziwezi kushinda tenda, chaguzi mbalimbali n.k. Bila rushwa haziwezi kutawala watu. Bila rushwa haziwezi kufanya biashara. Ni rushwa, ni rushwa tu kila mahali.
Anyway, kitu ambacho watu wengi hatukielewi ni kuwa rushwa ni mfumo wa kiroho unaoratibiwa na kuendeshwa na shetani mwenyewe ktk ulimwengu wa roho. Takukuru, Tiss, Polisi n.k. hawawezi kamwe kukomesha rushwa. Bwana Yesu Kristo mwenyewe ndiye anaweza kukomesha rushwa kwa njia ya kuwaweka watumishi wake waadilifu ktk Taasisi hizi. Watu wenye hofu ya Mungu. Watu waliojikana na wameubeba msalaba wao. Watu wasioipenda dunia kwa sababu wanajua Wao ni wageni wapitaji tu hapa Duniani. Wanaamini kuwa utauwa na kuridhika ni faida. Wanajua kuwa hapa Duniani walikuja uchi na wataondoka wakiwa uchi. Kwao kwa milele ni mbinguni alipo Bwana Yesu. Watu wanaompinga na kumkemea shetani na wanamkataa pamoja na mambo yake yote. Wakristo wakiookoka kweli kweli.
 
Sasa wamkamate nani wamuache nani?....hapa kitakachotokea ni kuenguliwa kwa wale wasiohitajika na Wakubwa kwa kisingizio cha rushwa ili hali asilimia 90 wametoa rushwa.

Na utakuta hata wale walioambulia kura 0 kuna miongoni wao ambao waliojaribu kujitutumua na vijisent vyao vya mboga masikini ya Mungu.

CCM wabuni tu mbinu nyingine ya kupitisha Wagombea wao maana hii iliyopo rushwa haidhibitiki.
 
Kuanzia juu hadi kwa wajumbe wote wanajuana kwa vilemba vyao kama wapembaView attachment 1532468
We Kigogo Warioba ni shida!!
Kwa hiyo CCM ni taasisi ya rushwa, hakuna wakuwazuia!!
TAKUKURU wapo kama figue head, wanaangalia tuu!!
Watanzania ni maskini hawawezi kukataa fedha hiyo ni fact!!
Ila tuwaombe Wapiga kura fedha wachukue wasiwapigie kura mayabithi wa Lumumba!!
 
Wa
Inachekesha Sana kwamba Kama nchi tuna chombo Cha kupambana na Rushwa Ila Hadi Leo tunavyoongea Hakuna mtia Nia wa chama chochote aliyepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kugawa Rushwa ingawa Rushwa imetembea wazi wazi

Cha kushangaza zaidi CCM Wana taarifa za baadhi ya wagombea kupitishwa kwa kutoa Rushwa Ila TAKUKURU hawana hizo taarifa kwani Kati ya walioongoza kura za maoni Hakuna aliyepo mahakamani kwa kesi ya rushwa
Wanatekeleza Sera namba moja ya CCM Mpya yaani Rushwa ambayo hadi serikali yenyewe ni mtoaji.Kwa bahati mbaya,TAKUKURU wanawasaka watoa rushwa bila kushughulikia pia wapokeaji na mawakala wao.Mifumo ya fedha chafu/haramu(Money Floundering) haiwezi kubaini mzunguko/miamala ya fedha walizofanya wagombea/wajumbe hawawezi kuvibaini?
Nawaza kuwa Engineers wa Rushwa wapo CCM Mpya na wanatumika kuwazuia TAKUKURU kufanya kazi yao.
Tuikatae CCM hata kwa ukumbatiaji wa Rushwa za wazi wazi katika michakato ya uchaguzi.Rushwa ya CCM Mpya haifichiki kama Pembe la Ng'ombe.Ukimpa uongozi aliyetoa Rushwa tegemea arejeshe alichopoteza na faida kabla ya kuwatumikia waliomchagua.
Rushwa nyingine iliyofichika ni mishahara,marupurupu,posho na fursa Huru ya kujineemesha iliyopo kwenye siasa.Wanajipangia vinono kwa kazi rahisi na kukandamiza ajira zingine kama Ualimu,Udaktari,Uinjinia,Uafisa Ugani nk kwa kuwapa malipo duni na kusababisha Watanzania kuacha taaluma zao kukimbilia Green Pastures kwenye siasa.Hali hii pia ni Rushwa kwa sababu inavuruga ufanisi wa Wanataaluma,wanageuka washangiliaji badala ya kusimamia Taaluma.
 
Wote wameoza kwa Rushw
Sasa wamkamate nani wamuache nani?....hapa kitakachotokea ni kuenguliwa kwa wale wasiohitajika na Wakubwa kwa kisingizio cha rushwa ili hali asilimia 90 wametoa rushwa.

Na utakuta hata wale walioambulia kura 0 kuna miongoni wao ambao waliojaribu kujitutumua na vijisent vyao vya mboga masikini ya Mungu.

CCM wabuni tu mbinu nyingine ya kupitisha Wagombea wao maana hii iliyopo rushwa haidhibitiki.
Wote wameoza kwa Rushwa,kuanzia Top to Bottom.Wakifuatiliwa kikamilifu,wataingia hatiani kuanzia wagombea hadi wajumbe.Mahakama ya Mafisadi na Magereza yangejaa Kijani/Njano/Nyeusi.
 
Inachekesha Sana kwamba Kama nchi tuna chombo Cha kupambana na Rushwa Ila Hadi Leo tunavyoongea Hakuna mtia Nia wa chama chochote aliyepelekwa mahakamani kwa tuhuma za kugawa Rushwa ingawa Rushwa imetembea wazi wazi

Cha kushangaza zaidi CCM Wana taarifa za baadhi ya wagombea kupitishwa kwa kutoa Rushwa Ila TAKUKURU hawana hizo taarifa kwani Kati ya walioongoza kura za maoni Hakuna aliyepo mahakamani kwa kesi ya rushwa
TAKUKURU wameteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM pia mgombea wa CCM, hivyo TAKUKURU haiwezi kuwakamata wenzao.
 
Dr. Walter Rodney ktk kitabu chake ... How Europe Underdeveloped Africa ... anasema (kwa tafsiri ya kiswahili) ... Ukiona mhudumu wa Ofisi anaiba rimu ya karatasi, usijisumbue, siyo yeye; Na ukitaka kudhibiti wizi na kuimarisha maadili kazini, panda juu kwa Katibu Mkuu wa Wizara kwani huko ndiyo kuna uozo mkubwa ... Hakuna Mtumishi mwajiriwa anayeweza kufanya vizuri au vibaya isipokuwa amemwona wa juu yake (Boss) anafanya.
Inasemekana, (mie binafsi sina ushahidi kwani sijawahi pata tatizo na Takukuru) Takukuru inaongoza kwa ku-promote rushwa Nchini.
Habari ndiyo hiyo.
Ni vigumu sana kwa rushwa kukomeshwa ktk Nchi nyingi za Africa kwa sababu Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zipo zinastawi na kufaidika na mifumo ya rushwa. Bila rushwa haziwezi kushinda tenda, chaguzi mbalimbali n.k. Bila rushwa haziwezi kutawala watu. Bila rushwa haziwezi kufanya biashara. Ni rushwa, ni rushwa tu kila mahali.
Anyway, kitu ambacho watu wengi hatukielewi ni kuwa rushwa ni mfumo wa kiroho unaoratibiwa na kuendeshwa na shetani mwenyewe ktk ulimwengu wa roho. Takukuru, Tiss, Polisi n.k. hawawezi kamwe kukomesha rushwa. Bwana Yesu Kristo mwenyewe ndiye anaweza kukomesha rushwa kwa njia ya kuwaweka watumishi wake waadilifu ktk Taasisi hizi. Watu wenye hofu ya Mungu. Watu waliojikana na wameubeba msalaba wao. Watu wasioipenda dunia kwa sababu wanajua Wao ni wageni wapitaji tu hapa Duniani. Wanaamini kuwa utauwa na kuridhika ni faida. Wanajua kuwa hapa Duniani walikuja uchi na wataondoka wakiwa uchi. Kwao kwa milele ni mbinguni alipo Bwana Yesu. Watu wanaompinga na kumkemea shetani na wanamkataa pamoja na mambo yake yote. Wakristo wakiookoka kweli kweli.
Kama mwenyekiti ananunua jogoo kwa laki wakati anajua bei ya soko ni elfu 10 ndio kujihusisha kwake na rushwa huko
 
Mkuu VYEMELO ,Mungu akubariki sana sana na kongole kwa mchango bora kabisa asubuhi hii ya Jumatatu.
Nimebarikiwa sana na maandishi yako. Endelea vivyo hivyo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom