Ni lugha gani ipewe kipaumbele Tanzania kati ya kiswahili na kiingereza

dsibora

New Member
Oct 6, 2011
3
0
Ndungu wanajamii.
mie bado sijaelewa sera yetu ya elimu kuhusu utumiaji wa lugha mbili za kiswahili na kiingereza hivi kwa changamoto za dunia ya leo,za utandawazi na soko huria ni lugha gani itatusaidia kuandaa jamii itakayokuwa tayari kuzikabili?
 
Kiingereza.
...hivi interview za Halmashauri na taasisi za serikari huwa zinafanyika kwa lugha gani vile!?
 
Kusema ukweli kiingereza ni mzigo, tuifanye kuwa lugha ya kigeni itakayofundishwa kwa viwango vya juu ili itufae kimataifa, lakini matumizi ya ndani, elimu n.k. Tutumie kiswahili.
 
mimi naona lugha nzuri yakutumiwa na watanzania iwe kichagga kwani ni luhga ya wakwe zangu.
 
wa ndg.hebu tuache masihara!kiswahili ni noma!ukienda nje ya nchi unatia aibu!zee zee nyng!!kingereza bomba!hamuon wakenya na waganda wanakata mbuga?ukienda USA unamkuta mkenya driver taxi,mbongo mh utata
 
Jibu ni Kiswahili.

Ukiangalia nchi nyingi duniani,tena zilizo na urafiki wa karibu na waengereza hazitumii kiengereza na zinz mafanikio makubwa sana, Angalia nchi za scandnavia,(sweden,kiswedesh,/denmark;Kidenish/Norge,Kinorge na Finland,)hizi nchi pamoja na muungano wao bado kila mmoja anazungumza lugha yake na sikiengereza.

Lakini pia nchi hizi zinaidadi ndogo sana ya watu,Pia ukiangalia holand ni nchi yenye mafanikio lakini haiongei kiengereza pia ina watu si zaidi ya 5mil.

Sijui watanzania munafikiria nini Kutaka tukiache kiswahili turukie kiengereza .

yuko mchangiaji mmoja hapo amesema kua Tubakie na kiswahili lakini tutilie mkozo kwenye Kiengereza ili tukijue kiengereza kama lugha ya pili na ya mawasiliano ya nje tu inatosha.
 
maoni mazuri,lakini mie nadhani hao unaowasema waliweka misingi tangu awali sie tunazungumzia wakati huu ambao maendeeo yetu yanahitaji mahusiano zaidi na mataifa mengine mfano katika elimu ni machapisho mangapi yaliyo katika kiswahil,tatizo hapa ni kubaki kuwa ndumila kuwili huku tunasema kiswahili kinatufaa tunapoingia katika uhalisia wa uchumi shindani watz tunapwaya,mfano omba kazi hudhuria interview ongea broken uone,watasema mtu mwenyewe hata hawezi kujieleza bora tungeamu lugha ipi ipiewe kipaumbele kuliiko kuwa kati
 
mimi naona lugha nzuri yakutumiwa na watanzania iwe kichagga kwani ni luhga ya wakwe zangu.

mkuu mbona umeongeza lugha nyingine badala ya kujadili kiingereza na kiswahili. Unasumbuliwa na chembechembe za ukabili. Asante nyerere kutuunganisha wa Tz kwa lugha ya kiswahili.
 
wa ndg.hebu tuache masihara!kiswahili ni noma!ukienda nje ya nchi unatia aibu!zee zee nyng!!kingereza bomba!hamuon wakenya na waganda wanakata mbuga?ukienda USA unamkuta mkenya driver taxi,mbongo mh utata
Usituzingue hapa kwani lazima tukafanye kazi ulaya
tuna madini kuliko Kongo inayosifiwa wao wajifunze
lugha yetu ili waje kutudhulumu vizuri maana viongozi
wetu ni kama wale wa "Mfalme JUHA" Tanzanite, Uranium,
dhahabu, Almasi, Silver, Chuma....... Tena wakiendelea
si ajabu ukakuta tunapata madini kama Shinyanganite,
Dodomanite..... n.k. Sio tukawe madereva tax ulaya.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom