Ni Lipi Lengo Kuu la CCM? Kuendelea Kutawala au Kutuondoa Katika Umasikini?

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,132
Wadau

Katika kipindi cha week moja tumekuwa katika msukosuko wa kuwasema au kuwataja mawaziri ambao wanashtumiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kukwapua mali za nchi yetu. Haya yamekuwa yakitokea kwa viongozi kadhaa ndani ya serikali na chama tawala (CCM).

Vikao vya ndani ya CCM tunasikia vinafanyika mara kwa mara na hivi karibuni kulikuwa na vikao wa wabunge kutoka CCM. Wengi hatujui haswa yanayojadiliwa katika hivyo vikao zaidi ya habari za hapa na pale ambazo hama tunazipata humu kwenye jamvi (JF) au vyombo vingine vya habari.

Swali linalonijia mara kwa mara ni Je katika hivyo vikao CCM wanajadili jinsi ya kuendelea kutawala au jinsi ya kumkomboa Mtanzania wa kawaida katika hali ngumu ya maisha inayomkabili? Viongozi wanaoshtumiwa kuwaletea watanzania hali ngumu ya maisha bado wanaendelea na vyeo vyao na hata wabunge wanaojaribu kuwakemea wanatishiwa maisha yao. Je CCM inafanya hivyo kwa manufaa ya Mtanzania au mwana CCM (aliye na cheo).

Enyi wana CCM, tuambieni mbiu yenu kuu ni Kuendelea kutawala au Kumkomboa Mtanzania katika hali ngumu ya maisha?
 
Huna pointi CCM ni chama chenye dola kamili, si vyama vya msimu kama CDM
 
Lengo lao ni kuendelea kutawala.

Kama lengo lao kuendelea kutawala wakati Watanzania tunaendelea kufa kwa kukosa madawa hospital, vigari vyetu vinakatika spring kila siku kwenye mashimo barabarani, kula milo miwili anasa, inabidi tumipe lipi bora. Kuendelea kuwa na CCM au kuangalia plan B
 
Kama lengo lao kuendelea kutawala wakati Watanzania tunaendelea kufa kwa kukosa madawa hospital, vigari vyetu vinakatika spring kila siku kwenye mashimo barabarani, kula milo miwili anasa, inabidi tumipe lipi bora. Kuendelea kuwa na CCM au kuangalia plan B

Plan B ni kuhama nchi mkuu kwa.maana piga ua hivi vyama vya msimu nu ngumu kushika dola
 
Back
Top Bottom