Ni lipi gari maalumu kwa serikali ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lipi gari maalumu kwa serikali ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MSIPI, Mar 1, 2012.

 1. M

  MSIPI Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu, wadau nimekuwa nikiitizama Nchi yetu kwa muda mrefu na kuutafakari uelekeo wetu na kushindwa hata kuamua kwa vitu vidogo kabisa. Hebu fikiria hadi leo hii, Tanzania na ikiwa ni hivi majuzi tu, tumetoka kusheherekea nusu karne ya kuutumikia uhuru wetu, lakini bado tumeshindwa hata mambo madogo kabisa. Mathalani wadau hadi leo hii ni lipi hasa gari linalotumika hasa na serikali yetu, yaani ukipita barabarani basi uwe na urahisi wa kutambua kwamba hili ni gari la serikali na hili ni aina ya gari la mtu binafsi.

  Hata sasa tembea huko mitaani utaona Hyundai, Toyota Landcruiser ya aina yeyote,Corolla, Landlover,Mitsubishi, Rav 4 na nyingine za aina mbalimbali zikiwa zote zinatumika na serikali yetu. Tunashindwa kweli kuwa na sera au muongozo wa kusema kwamba magari ya serikali ni haya! Hayumkini katika kipindi kifupi kijacho sasa serikali yetu itatumia Hammer na Vogue. Waziri Mh. Dk John Pembe Magufuli waziri mwenye dhamana uko wapi.

  Wadau tuijadili hiyo, mwenye majibu please!
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Hadi Bajaj za Serikali zipo...
   
 3. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanatumia pia Benz, Ford,BMW nk
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  magari ya serikali utayatambua kwa plate number zake..zimeandikwa STK,STH,STJ, etc..SM,SU,etc etc etc
   
 5. i

  iMind JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Kwa nini unataka kuwe na gari maalumu. Itasaidia nini kwa mfano serikali ikitumia gari aina fulani pekee. Nafikiri wakati mwingine mnapenda kuilaumu serikali hata kwa vitu ambavyo havina maana. Katika hizi zama za utandawazi, biashara huria, na ushindani unaweza kweli ukachagua gari aina moja au mbili zitumike na entire Govt? Ukumbuke kuwa pia taasisi na Idara tofauti za Serikali zina mahitaji tofauti ya magari kulingana na mazingira na kazi zao. Ndugu yangu kajipange, hoja yako haina mshiko.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Utandawazi mkuu ndio unatumaliza ikiwa ni pamoja na sheria za manunuzi za kitandawazi!
   
 7. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 734
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  mhh! Kwan nchi nyingine zina gar maalum za serikali? Njia ya kulitambua gar la serikali ni kwa kuangalia namba
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbuka kuwa serekali inapokuwa na gari za aina moja hata matunzo yake ni rahisi.
   
 9. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja alitaka serikali iwe na specific types of vehicles kulingana na mazingira ya kazi, mahala pa kazi, cheo cha mtu na umuhimu wake. Tuna weza kuamua rais atumie benz na landcruiser v8. Mwaziri wote landcriser tu, wabunge na wakuu wa mikoa na wilaya wapewe landlover mpya TDI kwa urahisi wa kukagua maendeleo. Na watumishi wengine wapewe magari kulingana na mazingira ya kazi na umuhimu wa mtumishi na cheo chake ilimradi tubane matumizi ya serikali.
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mimi huwa sioni kama ni maamuzi ya busara wakubwa wa serikali kutumia magari makubwa kama V8 katika jiji kama Dsm! Zinunuliwe gari ndogo kwa matumizi ya mijini.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe unataka waheshimiwa sana watembelee bettle? hapana bana, mbona majiji makubwa kama New York kuna macardilac, ma Hammer, GMC, N:K?
   
 12. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Na yale yanayotolewa kama msaada je? Au wahisani wapewe condition ya magari watakayotoa! Mbona familia moja baba ana BMW, mama ana Harrier na mtoto ana CRV?
   
 13. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Umeishasema majiji makubwa kwa hiyo si Tanzania,halafu ebu nitajie kiongozi mmoja uliyewahi kumuona katika msafara wake akitokea katika hizo HUMMER,GMC,CARDILAC?
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Tatizo liko hapa..magari mengi ni ya msaada na mikopo kutoka nchi mbali mbali..kama unavyojua tena, Japan wakitupa msaada wa magari watatoa TOYOTA, uingereza watatoa LANDROVER, FORD, etc, India wanatupa MAHINDRA au TATA..
  kifupi taifa legelege lenye viongozi legelege halipati fursa ya kuchagua moja!
   
 15. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya ndiyo yaleyaleee, "Vazi la Taifa"
   
 16. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Umiona babuuu

  Hapo sasa sijui tunataka nini.......bora angesema yanayotumika ni ghali na mzigo kwa serikali
   
Loading...