Ni lini Watanzania wataelewa kwamba shida sio Mbunge wala Diwani bali ni Mfumo wa hovyo

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,461
8,669
Kuna watu wanaamini kwamba Charles Kimei ataibadilisha Vunjo, sasa imani yao inaegemea kwamba jamaa alikuwa CRDB, na wanaamini pesa alizovuna CRDB zitaenda kuibadilisha Vunjo.

Haya ni mawazo a kijinga sana na ya kupuuzi yanayo wazwa na watu wenye uelewa finyu sana. MO alikuwa na pesa mbona singida bado ni masikini? Rostam alifanya nini Igunga si alikuwa na pesa?

Shida sio pesa shida ni mifumo mibovu na nchi kuto kuwa na vipa umbele vinavyo lenga watu wa chini.

Jimbo hata likilosa mbunge si kuna Mkuu wa wilaya? Mkurugenzi wa wilaya si yupo? Mwenyekiti wa Halimashauro si yupo? Mkuu wa mkoa si yupo? Hao unazani wanashindwa kulea maendeleo mpaka mbunge?

Acheni kushabikia ujinga, Charles Kimei hatachukua pesa zake za mafao CRDB akawaletee watu maendeleo na sio jukumu lake bali la Serikali.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom