Ni lini watanzania tutapata viongozi wazalendo?

amba.nkya

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
446
131
Ili watanzania tuweze kupata maendeleo na hatimaye kuifikia ndoto ya ‘Maisha bora kwa kila mtanzania’, tunahitajika utashi wa kisiasa kwa viongozi wetu. Utashi kwa maana ya uongozi unaongozwa kwa misingi ya uzalendo wenye kujali usawa na kuweka mbele maslahi ya wananchi. Inasikitisha sana kuona viongozi wengi wanapokuwa madarakani kufanya mambo ama kwa kujisahahu au kwa makusudi kabisa tofauti na matarajio ya wananchi.
Mfano ni pale viongozi wenye dhamana kubwa kutokuwa waadirifu kwa kutoa maamuzi yasiyo na tija kwa nchi na wanapopinga bila aibu wala woga na kuwa ving’ang’anizi wa jambo lisilo na maslahi kwa taifa kama vile hawaoni madhara makubwa yatakayotokea kwa wananchi (Richmond, EPA, Dowans, IPTL, kuzuia maandamano ya amani na kuua raia wasio na hatia, nk, nk, nk ).
Aidha, kwa kutumia kodi zetu, viongozi wengi wa serikali chini ya CCM wanapata fursa ya kusafiri nchi za nje zenye kuonyesha maendeleo sio tu Ulaya na Amerika bali hata pia nchi za wenzetu wa Afrika tukiwa na imani ya kwenda pia kujifunza huko jinsi nchi husika zilivyopiga hatua za maendeleo, lakini kinyume chake wanarudi kama watarii. Tamaa na ubinafsi ndio hulka za viongozi wetu wenye kujali maslahi yao binafsi, watoto wao, wajukuu wao, na maswahiba wao.

Je, tutafika? Ni lini watanzania tutapata viongozi wazalendo?

Tujadili…………………….!!!
 
Back
Top Bottom