Ni lini viongozi wa afrika watakuwa wanaachia madaraka bila kulazimishwa na umma?

backer

Member
Dec 22, 2010
86
8
Inasikitisha sana kuona kuwa viongozi wengi wa afrika wamekuwa makupe wa madaraka, wakishaonja ikulu tu, inakuwa kama sumu sijui hasari? mimi hata sielewi, tena wengine wanasingizia kuwa walipigania uhuru, sasa kama ulipigania uhuru kwa nini usitoke kwa heshima kama nyerere na mandera? ilianza kwa mugabe, ikaja kwa mwai emilio kibaki, ikaenda kwa gbagbo ikatoa athari zake tunisia kwa ben sasa inalilia kwa mubarak, je? baada ya hapo inkwenda wapi? this is the wind of change,. ukikataa kwenda na upepo huu utapelekwa hata kwa nguvu na upepo huu.:bump:
 
Ni lini waafrika wataheshimu taratibu zao? walizoziweka wenyewe..ni swali nzuri nalo
 
Kwa Tanzania hatuna tatizo hilo, ila badala yake ni chama hicho hicho hakitaki kuachia madaraka -- ni ujanja tu mwingine. Hapa kwetu viongozi (marais) wanaachia madaraka ukifika muda wao lakini kulindana madhambi yao kwa hali ya juu ndiyo kunafanya chama hicho hicho kuendelea kukaa madarakani.

Hata hivyo inafurahisha kuona hilo limeshashtukiwa na CCM hana maiosha marefu -- huko huko kulindana ndiyo kutaiangusha.
 
Back
Top Bottom