Super Charged
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 922
- 1,635
Habari wana JF,
Kuna vitu huwa tunaviona vya kawaida katika jamii lakin kumbe vinaathiri maisha ya baadhi ya watu. Nina mdogo wangu ana umri wa miaka 19 yeye amekuwa akiathiriwa na suala la ufupi. Yani kiufupi anapoteza pesa zake nyingi kutafuta dawa ya kuongeza urefu, mara leo kaagiza kutoka india, mara leo kafanya hivi.
Kiukweli ni kama anapoteza pesa tu, ingali kuna njia dawa aliagiza kutoka mataifa ya nje ikamsaidia kuongeza kama nusu inchi, ni kidogo sana kiukweli. Maisha yake yote yeye yuko na kutafuta urefu. Ana urefu wa futi 5.3 kikawaida ni mfupi mbele ya wanaume warefu lakn pia ni kama yuko average.
Anapenda kucheza baskteball, kwa umaridadi alonao katika huo urefu wake naona unamtosha maana ni hatari katika basketball na ninataman kumuona anafika mbal katika career ake. Huwa tunamwambia achana na urefu miaka 19 bado unaweza refuka mpaka unapofikisha umri wa miaka 21, lakini amekuwa akikataa kwa sababu anajiona kama ameshakuwa mkubwa na hawez refuka tena kwa sababu ana ndevu. Naomba kujuzwa wana JF.
Je, mwisho wa kurefuka ni miaka mingapi, anaweza ongezeka kidogo kwa umri alonao miaka 19.
Kama kuna dawa ya kumfanya aongezeka inches kadhaa zaidi ya hapo naomba mnijulishe pia mbali na surgery maana anachosikia chochote anafanya ni kama kavurugwa hajui kizur wala kibaya, naomba kujuzwa kama kuna dawa au njia nzuri ili nimsaidie dogo.
Changia na wewe katika umri gani uliacha refuka kwa wanaume.
Naomba kusaidiwa maoni wakuu maana huku ndo nyumbani kwetu, maana dogo tunaona suala dogo lakin linaathiri maisha ake kiujumla maana anaona kama ndoto zake hazitatimia hata kama akifanikiwa anaona ataitwa mchezaji mfupi, kingine anachoona kama hataongezeka licha ya kuambiwa ana nafasi mpaka miaka 21, ni yeye alibalehe mapema akiwa na umri wa miaka 16, (kiume).
Naomba msaada wana JF usijibu kwa dhihaka jibu kama mtoa elimu.