Ni lini uganda italipa fidia ya vita vya kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lini uganda italipa fidia ya vita vya kagera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Aug 20, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Ni lini Uganda italipa fidia ya vita vya Kagera pamoja na mahusiano mabaya kati ya Tanzania na Uganda kwenye miaka ya mwanzoni ya 70 hasa baada ya Tanzania kuamua kumpa hifadhi ya kisiasa rais aliyepinduliwa Milton Obote.

  Mzozo huo uliingia hatua nyingine baada ya majeshi ya Uganda yakiongozwa na Idd Amin Dada yalipovuka mpaka na kuua raia,kufanya uharibifu wa mali kama kuharibu kiwanda cha sukari,kuvunja daraja na kuitangaza Kagera kuwa sehemu ya uganda.

  Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere iliingia vitani ili kukomboa sehemu ya nchi yetu na pia iliamua kuingia hadi Uganda na kumng'oa Idd Amin madarakani.

  Baada ya vita, Uganda ilitakiwa kulipa gharama zilizotokana na uharibifu wa mali na upotevu wa maisha uliofanywa na majeshi ya Uganda yalipovamia Tanzania.

  Baada ya vita mbali na baadhi ya askari wetu kupoteza maisha,wengine walipata vilema na wengine kupata maradhi kama matatizo ya akili hali hii haikuwaathiri wao tu bali iliziathiri hata familia zao,jambo lakusikitisha wengi wa askari hao hawakulipwa fidia na hata familia zao nazo zimeishi maisha duni hadi sasa.

  Katikati ya miaka ya 2000 tulisikia kauli ya rais Museveni akiiomba serikali ya Tanzania ilifute deni lilitokana na vita vya Kagera lakini kwa bahati mbaya sikusikia kauli yoyte toka serikali ya Tanzania kama wamekubaliana naye au la.

  Ingawa binafsi sikubaliani na ombi hilo labda wajadiliane kuhusu riba iliyotokana na deni hilo,
  nina hakika serikali ya Uganda inaweza hatakupunguza deni hilo kwa kulipa kidogokidogo kwani chini ya utawala wa rais Museveni tumeshuhudia matumizi makubwa ya kijeshi ikiwamo kushuhudia ikishirikiana na majeshi ya Rwanda kuvamia Kongo.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kabla sijachangia kwa kirefu zaidi napenda kujua, Kwani tunadai bei gani,
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu mkowa wa kagere ni mali ya waganda sisi wa tz 2napaswa kuwarudishia

  ngoja nikapate kisusio mmeku
   
 4. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who has to pay who is a million Dollar question. There was no agreement for paying the cost of the war. Idd Amin Dada claimed Kagera to be part of Uganda. We fought the war of course and paid a huge price in terms of human life, economic amongst others and I am sure we have not recovered todate.

  I stand to be corrected it's was eighteen months but that turned out to be 33 years. Ugandans also paid a huge price and I dont know who is gona pay them anyway. We shouldn't dig graves let us forget the past and build a new East Africa of course with lessons.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  And this is the correction;
  iddi invaded tz, that's why uganda must pay for their stupid president.
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mbona hiyo pesa ilishalipwa kitambo tu toka 2007 ilikuwa kama $ 67 million...! Soma hapa http://allafrica.com/stories/200704110882.html[/PHP]
   
 7. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,533
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  Majibu ya nyongeza zaidi:

  Tanzania: 1978 Amin's War: Tanzania Receives Service Charges
  June 28, 2000

  Dar Es Salaam — The government of Uganda has paid Tanzania about 9.6 million US dollars as part of service charges and equipment supplied to the former during the war to oust dictator Id Amin Dada from that country.

  The amount paid, according to the treasury, is part of 64.39 million US dollars already verified. The Deputy Finance Minister, Abdisalaam Issa Khatib has said Tanzania was supposed to be paid 123.2 million US dollars, according to agreement signed by the two neighboring states on September 23, 1998.

  Source: http://allafrica.com/stories/200006280103.html
   
 8. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pesa ilishalipwa siku nyingi..

  Jamani kabla ya kuanzisha threads ni bora kufanya research kwanza, jambo hili lilishajadiliwa sana humu...:hat:
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  (Mbona hiyo pesa ilishalipwa kitambo tu toka 2007 ilikuwa kama $ 67 million...! Soma hapa http://allafrica.com/stories/200704110882.html)
  Nashukuru kwa kunijulisha ila tu nimepost baada ya kusikia malalamiko ya askari wengi ambao walitelekezwa na pia kama serikali imeshalipwa ilipaswa kutoa maelezo hizo pesa zimetumikaje na nani walikuwa walengwa kwani zaidi ya askari kuna wananchi wa mkoa wa kagera ambao waliathirika kwa kiasi kikubwa na vita hivyo.pia inawezekana ililipwa lakini ikaishia mikononi mwa wajanja wachache kwani hakuna taarifa yoyote iliyoletwa bungeni kuonyesha matumizi ya pesa hivyo
  hata hivyo nashukuru kwa kunipanua mawazo na nitaendelea kufanya research kujua kama hizo pesa zilipolipwa ziliingia kwenye mfuko gani na zilifanya nini
  tuko hapa kuelimishana
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mashahidi wakuu wote wamefariki ,nafikiria i disimisi !
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  na Pesa zilishaliwa zote hahahaha bila kurejesha hali ya uchumi kama ule kabla ya Vita
   
Loading...