Ni lini Tanzania itakuwa na umeme wa uhakika, Maji safi na barabara bora!!! Nimechoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lini Tanzania itakuwa na umeme wa uhakika, Maji safi na barabara bora!!! Nimechoka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Feb 12, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Labda mimi nimekaa ugaibuni kwa muda mrefu lakini ndugu zangu naomba niulize bila siasa.

  Ni lini nitapiga simu kwa Wazaziwangu Tanzania nisiambiwe hatuna umeme?, Hatuma maji safi?, Kuna foleni sana??. Chakula kinaharibika kwa sababu ya umeme!, Maji ni ya kununua kwa ndoo!! na barabara si za kueleweka!. Umeme wazaziwangu wanaulipia kabla ya hata kutumia lakini unakatwa!, maji tumevuta peke yetu bila msaada hadi nyumbani sasa ni kwa nini hivi vitu vichache tu serikali haiwezi kufanya. Sasa serikali inafanya nini kama hata maji tu ambayo ni machafu haiwezi kusambaza. Bill za maji tunalipa, viwanja tunalipia ingawa si vya serikali na barabara hatuzioni.
  Sisi tumekuja nje kutafuta maisha tumejitahidi kwa pesa yetu kujisomesha, kujenga, na kusaidia Wazazi wetu Tanzania lakini serikali inaturudisha nyuma na hii inasikitisha sana.
  Kama wewe kweli ni Mtanzania Mzalendo na unapenda Tanzania huwezi kuisifia serikali kwa kazi wanayofanya hata kama ni CCM au Chadema. Mimi sijui tu lakini serikali inanichanganya sana!
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Juzi dada yangu kaniandikia email analia na kusema kua Saloon yake ambayo ndio anayoitegemea kwaaajili ya kuendesha maisha yake ameshindwa kuindesha kwa ukosekanaji wa umeme, then akiniomba nimsaidie jenereta angalau aweze kumudu garama za maisha ya dar, mwisho aliishia kwa kusema kua anashangaa kwanini wa tz wamekua wapole kiasi hicho wanashindwa kuandamana katika swala nyeti kama hilo,

  kiukweli niliumia sana na kuona ni jinsi gani nchi yangu ninayoipenda kwa dhat ikiendeshwa kiuandawazimu na wafanya biashara mafisadi wasiokua na nania njema ya kuleta maendeleo ya kijamii, kielimu na kiuchumi, tanzania bado tunadharauliwa na wenzaetu wa kenya na uganda katika soko la ajira kwani wao ndio wanaongoza kwa kutoa wataalam ktk sekta mbalimbali, sasa sijui sisi tunajivunia lipi? umeme wa shida, maji ya shida, mikopo elimu ya juu shida mpaka baadhi ya dada zetu wanaingia kwenye ukahaba ili waweze kujikimu na wamalize masomo yao.
  inauma sana na sasa yatupasa kuchukua hatua, sisi ambao tupo humu jamvini tunaongea mengi lakini hakuna utekelezaji na matokeo yake mafisadi wanaendelea kula nchi na sisi tunaishia kulalamika pembeni huku wao wanajua hatuna cha kuwafanya.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Spika wa dodoma alisema swali kama hili hutakiwi kuuliza hapa, subiri tamko la waziri! teh
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Siku tutakapoanza kutumia akili zetu. Pia tukiacha ubinafsi, wizi, uzembe na ufisadi...
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Bado sana.................
   
 6. l

  limited JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mimi naona mpaka vongozi wetu waache kufikiria hiviii!! 1+ 2= 12 then we 'll be ok
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa maneno mengine, yote hayo pamoja na kuiongoza CCM madarakani, tena watakaokuja waondoshe huo ubinafsi, wizi, uzembe na ufisadi... Vyenginevyo............. tusitarajie daima.
  Ah! Masikini Tanzania,
   
 8. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  CCM waking'olewa.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Tutakapoamua kukiondoa chama cha mafisadi madarakani
   
 10. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna mada moja ilikua nzuri sana iliwahi kujadili suala kama hili, ilikua inauliza, kuna faida yoyote ya kuwa mtanzania? Thread hii niliipenda sana kwani ilijaribu kuchambua kama kuna faida yoyote ya kuwa mtanzania wakata hali halisi ya maisha haina furaha hata kidogo. Umeme hakuna, Maji safi na salama hakuna, foleni ni kubwa barabarani, huduma za afya ni mbovu, shule watoto wanafeli na mazingira ni mabovu, wizi na uvamizi usiku kwenye nyumba zetu, ufisadi na wizi wa mali za umma pamoja na mengine kadha wa kadha...!

  Kweli ni bora mtu ubebe mabox ulaya walau unauhakika wa maisha pamoja na kwamba sio ya starehe sana kuliko kuishi Tanzania, kero ni nyingi mno...! Kweli sioni faida ya kuwa mtanzania au kujisifia kwamba mimi ni mtanzania kwa hali iliyopo...!
   
 11. n

  nyantella JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
   
Loading...