Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 116,495
- 215,349
Mh Mbowe katika hotuba yake kwa Taifa pamoja na mambo mengine mengi aliyoyazungumza, pia alizungumza kwa msisitizo sana jinsi Bunge la Tanzania lilivyogeuzwa kuwa Muhuri wa kupitisha Sheria mbovu za ukandamizaji pamoja na kuunga mkono bajeti za serikali zenye makando kando.
Mbowe alitamka bila kumung'unya maneno kwamba Spika na Naibu wake waligeuzwa kuwa Watumishi wa serikali kwa kulazimishwa kuhudhuria kila hafla ya Magufuli , kama haitoshi Mbowe aliendelea kusema Spika na Wabunge wa CCM walihongwa pesa taslimu ili kupitisha bajeti na miswada ya hovyo , huku akisema anao ushahidi wa jambo hilo na akiombwa atauweka hadharani bila shaka yoyote ile
Sasa swali langu dogo ni hili, ni LINI JOB NDUGAI atajitokeza hadharani kukanusha hili ama kulitolea ufafanuzi?