Ni lini Spika Job Ndugai atajibu tuhuma za yeye na Wabunge kuhongwa Pesa na serikali ya Magufuli ili kupitisha miswada mibovu ya sheria kandamizi?

Hawezi kutoka mwenyewe na kujibu tuhumabila kushurutishwa humu ktika majukwaa ya mitandao ya kijamii
huku ndipo dola yetu wakereketwa ilipo
 
Mh Mbowe katika hotuba yake kwa Taifa pamoja na mambo mengine mengi aliyoyazungumza , pia alizungumza kwa msisitizo sana jinsi Bunge la Tanzania lilivyogeuzwa kuwa Muhuri wa kupitisha Sheria mbovu za ukandamizaji pamoja na kuunga mkono bajeti za serikali zenye makando kando .

Mbowe alitamka bila kumung'unya maneno kwamba Spika na Naibu wake waligeuzwa kuwa Watumishi wa serikali kwa kulazimishwa kuhudhuria kila hafla ya Magufuli , kama haitoshi Mbowe aliendelea kusema Spika na Wabunge wa ccm walihongwa pesa taslimu ili kupitisha bajeti na miswada ya hovyo , huku akisema anao ushahidi wa jambo hilo na akiombwa atauweka hadharani bila shaka yoyote ile .

Sasa swali langu dogo ni hili , ni LINI JOB NDUGAI atajitokeza hadharani kukanusha hili ama kulitolea ufafanuzi ?
Wanabahati wanaongoza watu legelege.
 
Sheria kandamizi huwaathiri wananchi wengi wakawaida. Hivi ni hawahawa wanachi ambao walijitokeza kwa wingi(pengine haijawahi kutokea) kumsindikiza hayati JPM ktk safari yake ya mwisho ndiyo waliogandamizwa na sheria za awamu ya tano? Kama ni kweli kwamba watanzania hawa waliomsikitikia kwa kiwango kile ndiyo wanaogandamizwa na sheria hizo basi tunasafari ndefu sana mkuu.
Unazungumzia wale waliokuwa wanazimia huku wameshikilia mifuko yao mikononi?
 
Sheria kandamizi huwaathiri wananchi wengi wakawaida. Hivi ni hawahawa wanachi ambao walijitokeza kwa wingi(pengine haijawahi kutokea) kumsindikiza hayati JPM ktk safari yake ya mwisho ndiyo waliogandamizwa na sheria za awamu ya tano? Kama ni kweli kwamba watanzania hawa waliomsikitikia kwa kiwango kile ndiyo wanaogandamizwa na sheria hizo basi tunasafari ndefu sana mkuu.

Hata yule mamba mla watu au simba akinaswa na kuuawa, wananchi kwa wingi wao hujitokeza kushuhudia.
 
Nisikiliza ile hotuba ya Mbowe ,aliwachana live kina Ndungai bila chenga.Sasa hivi Ndungai kabakia kujiumauma na kutupia vijembe visivyo na mashiko kwa Mbowe! 🤣
 
Hii nchi ilikuwa imefikia pabaya mno, kikundi cha watu wachache kilikuwa kinafanya kitakayo bila hofu woga wala aibu.... - ukifanya ngweeee kesho nyumbani familia haikuoni.
 
Hii nchi ilikuwa imefikia pabaya mno, kikundi cha watu wachache kilikuwa kinafanya kitakayo bila hofu woga wala aibu.... - ukifanya ngweeee kesho nyumbani familia haikuoni.
Sasa Mungu amewageuzia kibao
 
Back
Top Bottom