Ni lini Serikali itawaajiri Watanzania waliosomea fani za mafuta na gesi wanaoozea mtaani huku taifa likiwa na gesi asilia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,315
8,214
Ni lini serikali itawaajiri watanzania waliosomea fani za mafuta na gesi wanaozea mtaani huku taifa likiwa na gesi asilia.

Kuna wakati tunatakiwa kuieleza serikali ukweli katika baadhi ya mambo muhimu kama haya. Tunayo miradi mikubwa miwili ambayo inasubiliwa kwa hamu na watanzania.

Kuna mradi wa LNG na EACOP, hii ni miradi mikubwa inayohusisha uwekezaji mkubwa na inafaida kubwa sana kwa taifa. Kutokana na uwekezaji wake kuwa mkubwa mara nyingi kote duniani miradi hii huchukua muda mrefu sana mpaka kufikia makubaliano ya kuanza kuitekeleza.

Sasa basi wakati tunasubiri hii miradi serikali tuwaangalie watanzania tuliowasomesha fani za mafuta na gesi. Mbona kama wanakaa sana mtaani bila kuajiriwa. Itafika kipindi hata watasahau hayo tuliyowafundisha na kuzeekea kabisa mtaani bila kazi. Kusubiri miradi ya LNG na EACOP ianze ndio wapewe ajira, nawambia watu watazeeka mtaani. Vijana wetu watazeekea mtaani. Serikali inatakiwa ilitazame hili kwa undani sana.

Lipo jambo la msingi la kufanya ili kuweza kuwasaidia watanzania hawa. Ukiangalia ajira zilizotangazwa tangu watanzania hawa waanze kuhitimu masomo yao 2016 hazizidi 15. Ukilinganisha na wanaohitimu masomo yao kila mwaka, utagundua serikali inatakiwa iweke mkono hapo.

Jambo lingine la msingi serikali ibuni miradi mingine iwaajiri hawa watanzania wa fani hizi za mafuta na gesi huku wakiwa wanasubiri hiyo miradi yakimkakati.

Watu walianza kuisikia LNG tangu 2014 this time is 2022, ukihesabu miaka ni mingi imepita. Bado watanzania hawa huwa wanasubiri hiyo miradi ndio waajiriwe.

Tuwaeleze ukweli, serikali wabuni miradi mingine, vijana waajiriwe.
Kuna miradi mingi sana. Mfano kusambaza gesi asilia mikoani kwaajili ya kupikia na kutumia kwenye magari.

Ni lini watanzania wataanza kutumia gesi asilia yao kupikia na, matumizi mengine mfano kwenye magari huko mikoani. Tunasikia tu wanao tumia ni wananchi wa Dar es Salaam. Mikoa mingine ni lini wataanza kutumia gesi asilia ambayo bei yake ni nafuu kuliko hizi gesi za akinaOryx, Mihani na Lake.

Na tunajua gesi asilia ni very cheap. Tungeweza kujenga miundombinu mizuri na kuwahamisisha watanzania, saivi karibia nusu ya watanzania wangekua wanatumia gesi asilia kupikia na kwenye magari yao huku serikali ikivuna mapato kwa wingi.

Ninajua tukisema tunasambaza mabomba Tanzania nzima hii, huu si mradi wa kuumaliza leo. Kusambaza mambomba Tanzania nzima kunahitaji pesa nyingi na muda.

Lakini tukisema tujenge vituo tu peke yake vya kujaza na kusambaza gesi huko mikoani, ni mradi ambao utachukua muda mfupi na watanzania wataanza kutumia na kufaidi matunda ya gesi yao kwa wakati huku serikali itaanza kuingiza mapato kwa wingi.

Kwa hiyo tunaposubiri LNG ambao ni mradi wa muda mrefu fanya yafuatayo:
1. Ajiri vijana wasambaze gesi mikoani.
2. Jenga vituo vya kujaza na kushindilia gesi mikoani.
3. Nunua magari makubwa matenka pakia gesi asilia kwenye matenki kutoka kwenye kituo cha Dar es Salaam peleka kwenye vituo vingine huko mikoani,
4. Then wasambazie wananchi wa mikoani waitumie kupikia na kwenye magari, tupate mapato.
5. Tengeneza mfumo wa mobile CNG station, uza CNG kwa kutumia magari maalumu yatayozunguka mikoa mbalimbali kuwafuata wateja. Magari hayo nayo yatumie gesi.

Hiyo njia ni nzuri badala ya kusubiri tujenge mabomba mpaka humo mikoani ambapo itataka uwekezaji mkubwa na, muda mrefu wa kukamilika. Badala ya tujenge vituo kama kama hivyo vya petrol station humo mikoani kisha tupeleke gesi kwa kutumia magari ya tenka.
 
Hiyo fani ilianzishwa na wafadhili matapeli sio Serikali wakijitia ohh Waataalamu hao hawapo.Baadaye wakaingia mitini bila kuajiri
 
Ilikuwaje hii sijawahi kuisikia kabisa
Mengi alifungua kampuni yake inaitwa Swala Oil and Gas Tanzania PLC hii ni moja ya.kampuni waliopiga yowe kuwa nchi Haina wataalamu wa oil and gas wanapata shida kuendesha shughuli za na kusema Vyuo vikuu waanzishe vitivo vya oil and gas wao wako tayari kufadhili wanafunzi kusoma chuo kikuu mambo ya oil and gas nchini

Ushindani ukawa mkubwa mno kupata hiyo course Chuo kikuu cha Dar es salaam ilikuwa shida .Unatakiwa kuwa na ufaulu wa kutisha wa juu

Kweli ufadhili ulitolewa lakini wanafunzi walipomaliza wakashangaa ajira hamna .The so called wafadhili makampuni ya oil and gas wakatokomea gizani bila kuajiri
 
Mengi alifungua kampuni yake inaitwa Swala Oil and Gas Tanzania PLC hii ni moja ya.kampuni waliopiga yowe kuwa nchi Haina wataalamu wa oil and gas wanapata shida kuendesha shughuli za na kusema Vyuo vikuu waanzishe vitivo vya oil and gas wao tayari kufadhili wanafunzi kusoma chuo kikuu mambo ya oil and gas nchini
Ushindani ukawa mkubwa mno kupata hiyo course Chuo kikuu cha Dar es salaam ilikuwa shida .Unatakiwa kuwa na ufaulu wa kutisha wa juu

Kweli ufadhili ulitolewa lakini wanafunzi walipomaliza wakashangaa ajira hamna .The so called wafadhili makampuni ya oil and gas wakatokomea gizani bila kuajiri
🏃🏃🏃🏃
 
Ni lini serikali itawaajiri watanzania waliosomea fani za mafuta na gesi wanaozea mtaani huku taifa likiwa na gesi asilia.

Kuna wakati tunatakiwa kuieleza serikali ukweli katika baadhi ya mambo muhimu kama haya. Tunayo miradi mikubwa miwili ambayo inasubiliwa kwa hamu na watanzania.

Kuna mradi wa LNG na EACOP, hii ni miradi mikubwa inayohusisha uwekezaji mkubwa na inafaida kubwa sana kwa taifa. Kutokana na uwekezaji wake kuwa mkubwa mara nyingi kote duniani miradi hii huchukua muda mrefu sana mpaka kufikia makubaliano ya kuanza kuitekeleza.

Sasa basi wakati tunasubiri hii miradi serikali tuwaangalie watanzania tuliowasomesha fani za mafuta na gesi. Mbona kama wanakaa sana mtaani bila kuajiriwa. Itafika kipindi hata watasahau hayo tuliyowafundisha na kuzeekea kabisa mtaani bila kazi. Kusubiri miradi ya LNG na EACOP ianze ndio wapewe ajira, nawambia watu watazeeka mtaani. Vijana wetu watazeekea mtaani. Serikali inatakiwa ilitazame hili kwa undani sana.

Lipo jambo la msingi la kufanya ili kuweza kuwasaidia watanzania hawa. Ukiangalia ajira zilizotangazwa tangu watanzania hawa waanze kuhitimu masomo yao 2016 hazizidi 15. Ukilinganisha na wanaohitimu masomo yao kila mwaka, utagundua serikali inatakiwa iweke mkono hapo.

Jambo lingine la msingi serikali ibuni miradi mingine iwaajiri hawa watanzania wa fani hizi za mafuta na gesi huku wakiwa wanasubiri hiyo miradi yakimkakati.

Watu walianza kuisikia LNG tangu 2014 this time is 2022, ukihesabu miaka ni mingi imepita. Bado watanzania hawa huwa wanasubiri hiyo miradi ndio waajiriwe.

Tuwaeleze ukweli, serikali wabuni miradi mingine, vijana waajiriwe.
Kuna miradi mingi sana. Mfano kusambaza gesi asilia mikoani kwaajili ya kupikia na kutumia kwenye magari.

Ni lini watanzania wataanza kutumia gesi asilia yao kupikia na, matumizi mengine mfano kwenye magari huko mikoani. Tunasikia tu wanao tumia ni wananchi wa Dar es Salaam. Mikoa mingine ni lini wataanza kutumia gesi asilia ambayo bei yake ni nafuu kuliko hizi gesi za akinaOryx, Mihani na Lake.

Na tunajua gesi asilia ni very cheap. Tungeweza kujenga miundombinu mizuri na kuwahamisisha watanzania, saivi karibia nusu ya watanzania wangekua wanatumia gesi asilia kupikia na kwenye magari yao huku serikali ikivuna mapato kwa wingi.

Ninajua tukisema tunasambaza mabomba Tanzania nzima hii, huu si mradi wa kuumaliza leo. Kusambaza mambomba Tanzania nzima kunahitaji pesa nyingi na muda.

Lakini tukisema tujenge vituo tu peke yake vya kujaza na kusambaza gesi huko mikoani, ni mradi ambao utachukua muda mfupi na watanzania wataanza kutumia na kufaidi matunda ya gesi yao kwa wakati huku serikali itaanza kuingiza mapato kwa wingi.

Kwa hiyo tunaposubiri LNG ambao ni mradi wa muda mrefu fanya yafuatayo:
1. Ajiri vijana wasambaze gesi mikoani.
2. Jenga vituo vya kujaza na kushindilia gesi mikoani.
3. Nunua magari makubwa matenka pakia gesi asilia kwenye matenki kutoka kwenye kituo cha Dar es Salaam peleka kwenye vituo vingine huko mikoani,
4. Then wasambazie wananchi wa mikoani waitumie kupikia na kwenye magari, tupate mapato.
5. Tengeneza mfumo wa mobile CNG station, uza CNG kwa kutumia magari maalumu yatayozunguka mikoa mbalimbali kuwafuata wateja. Magari hayo nayo yatumie gesi.

Hiyo njia ni nzuri badala ya kusubiri tujenge mabomba mpaka humo mikoani ambapo itataka uwekezaji mkubwa na, muda mrefu wa kukamilika. Badala ya tujenge vituo kama kama hivyo vya petrol station humo mikoani kisha tupeleke gesi kwa kutumia magari ya tenka.
Ajira sio zawadi..

Wakatafute Kazi Nje ya Nchi ambako Gani zao Zina Fursa..

Hata mimi ni Civil Engineer sijaajilowa nakomaa kitaa
 
Hao wanatakiwa waombe kazi za kimataifa i.e Angola, Nigeria etc...😀😀😀
 
Tuelezane ukweli mchungu hapa,watanzania tutaendelea kusubiri sana kama hawa wasomi wetu wa vitabuni bado wanafikiri hivi, wajibu wa serikali ni kuandaa mazingira ya watu wake wajiajiri na wajitegemee,serikali SIO mwajiri!,hapa way forward tulazimishe serikali iondoe ukiritimba wa nchi kutegemea umeme wa Tanesco tu,hawa tanesco wawe ni distributors tu,wazalishaji wa umeme wawe wengi (hawa vijana waliosomea ndio ingekua kazi yao ,kuzalisha umeme na kuwauzia Tanesco).
 
Embu tuone toa neno moja, mtu wa mafuta anaweza kujiajiri wapi.
 
Kama wanashindwa kuwafanya wawekezaji wa bomba la mafuta kutoka uganda kuja Tz EACOP kuwaajiri watz ndio wataweza kuwaajiri wao
 
Back
Top Bottom