Ni lini Serikali itajenga Chuo Kikuu mkoa wa Mwanza?

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
414
877
Kwa kuzingatia umuhimu na ukubwa wa jiji la Mwanza kunatakiwa kuwe na Chuo Kikuu cha Serikali ambacho kitatoa elimu kwa ukanda wote wa Ziwa.

Kulingana na matawi yaliyopo ya vyuo mbalimbali lakini bado hayajakidhi mahitaji na matakwa ya watu wa Mwanza. Kunatakiwa kuwepo na chuo kikuu ambacho main campus itakuwa Mwanza.

Namuomba Rais Magufulu kabla hajatoka Madarakani aache amejenga au ameanzisha ujenzi wa chuo kikuu mkoa wa Mwanza.

Hii itampa heshima na kumbukumbu nzuri sana kwa wananchi wa Mwanza na kanda yote ya ziwa kwa ujumla ukizingatia watu wa kanda hii wanampenda sana.
 
Shida ni Userikali au issue ni kutoa Elimu? SAUTI ipo wapi? Na je, imejaa?

Pia tatizo ni uhaba wa Vyuo au Tatizo ni ukosefu wa Mikopo wa watu kumudu Gharama?
 
Mmmh badala ya chuo ajira muhimu, matawi na vyuo binafsi vinatoa wahitimu wengi na vinatosheleza.
 
Kitajengwa Chato. Mwanza hakuna hata International Airport halafu mnataka UDSM yenu?

Hata hospital ya rufaa ya kanda ya serikali tumejenga Chato. Mwendo ni huo huo na chuo kikuu.
 
Kwa kuzingatia umuhimu na ukubwa wa jiji la Mwanza kunatakiwa kuwe na Chuo Kikuu cha Serikali ambacho kitatoa elimu kwa ukanda wote wa Ziwa.

Kulingana na matawi yaliyopo ya vyuo mbalimbali lakini bado hayajakidhi mahitaji na matakwa ya watu wa Mwanza. Kunatakiwa kuwepo na chuo kikuu ambacho main campus itakuwa Mwanza.

Namuomba Rais Magufulu kabla hajatoka Madarakani aache amejenga au ameanzisha ujenzi wa chuo kikuu mkoa wa Mwanza.

Hii itampa heshima na kumbukumbu nzuri sana kwa wananchi wa Mwanza na kanda yote ya ziwa kwa ujumla ukizingatia watu wa kanda hii wanampenda sana.
Mkuu kwa hali ilivyo nadhani sasa hivi haina budi kwanza serikali iangalie namna ya kupunguza hawa wasomi waliopo mtaani ambao bado hawana ajira. Maana kuzidi kuongeza idadi ya vyuo wakati bado kuna wahitimu wengi wasio na ajira ni kuzidi kuongeza tatizo.
 
Kanda ya ziwa serikali iboreshe chuo cha pansiasi kikubwa iongeze kozi mfano Bachelar ya kufuga chatu na fisi ( B A hyena and python keeping),B A in witch craft, au nakosea!??
 
Kwa kuzingatia umuhimu na ukubwa wa jiji la Mwanza kunatakiwa kuwe na Chuo Kikuu cha Serikali ambacho kitatoa elimu kwa ukanda wote wa Ziwa.

Kulingana na matawi yaliyopo ya vyuo mbalimbali lakini bado hayajakidhi mahitaji na matakwa ya watu wa Mwanza. Kunatakiwa kuwepo na chuo kikuu ambacho main campus itakuwa Mwanza.

Namuomba Rais Magufulu kabla hajatoka Madarakani aache amejenga au ameanzisha ujenzi wa chuo kikuu mkoa wa Mwanza.

Hii itampa heshima na kumbukumbu nzuri sana kwa wananchi wa Mwanza na kanda yote ya ziwa kwa ujumla ukizingatia watu wa kanda hii wanampenda sana.
Imekula kwenu mlizoea kulia lia kama watoto
 
Kanda ya ziwa serikali iboreshe chuo cha pansiasi kikubwa iongeze kozi mfano Bachelar ya kufuga chatu na fisi ( B A hyena and python keeping),B A in witch craft, au nakosea!??
Sawa bhana lakini sikumaanisha utani huu
 
Daraja la busisi haliwatoshi? Kwanini msingejikusanya siku ile ya tar 26 muungane mtoe maombi yenu kwa pamoja? Nyinyi watoto wa mwendazake mbona wasumbufu hivi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom