Ni lini Serikali itaanza kuwekeza kwenye viwanja vya michezo vya kisasa?

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
394
710
Salaam.

Kwa wale wanaofuatalia AFCON kule Cameroon watakubaliana na mimi kuwa Cameroon wametuacha sana kwenye suala la viwanja vya kisasa.

Viwanja vyao viko vizuri ni level za Ulaya.

Je, sisi tunakwama wapi na naamini hata kwenye suala la maendeleo tupo mbele ya Cameroon.

Kwa kwetu kidogo uwanja una uafadhali ni Uwanja Mkapa pale Dar es Salaam labda na wa uhuru kidogo lakini viwanja vya mikoani ni vina hali mbaya kabisa.

Kwa hali tuliyopo tunapaswa kuwa na viwanja vya kisasa walau hata 4 vya kubeba watu kuanzia elfu 40.
 
Ni suala tu la Serikali na chama chake cha ccm, kuvirudisha viwanja vyote ilivyo vikwapua kwa njia za wizi! Mfano kiwanja cha Sokoine Mbeya, Samora Iringa, Nelson Mandele Rukwa, Mkwakwani Tanga, Jamhuri Morogoro, Ali Hassan Mwinyi Tabora, na vinginevyo vingi!

Na baada ya kuvirejesha, viwanja hivi vingekabidiwa kwa Halmashauri zetu za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji kwa ajili ya kuvisimamia, lakini pia kuviendeleza na kuviboresha! Hakika baada ya miaka 10 mbele, tungeweza kuendesha mashindano ya aina yoyote yale.

NB: Hongereni Azam kwa kuweka yale mabango ya matangazo ya ki electronics kwenye uwanja wenu wa Azam Complex Chamazi! Hakika mkiweka na TV live wakati mechi inaendelea, basi mtakuwa mmetisha sana.


Na hii iwe changamoto kwa Vilabu kongwe vya Simba na Yanga ambavyo miaka yote vinaendeshwa kwa ujanja ujanja tu! Huku vikiwa na idadi kubwa ya mashabiki na mafanikio lukuki, ukilinganisha na hiyo Azam Fc
 
Back
Top Bottom