LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 15,791
- 23,056
Ni muda sasa tangu zoezi LA kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma lifanyike.Wananchi hawaoni mrejesho wa hilo zoezi.
Majibu yanatakiwa yawe ni watumishi wangapi wamekutwa na vyeti feki na wangapi wamekutwa wanatumia vyeti orijino lakini si vyao ni vya watu wengine.
NECTA inapotaka wananchi wawataje watu wenye vyeti feki au wanaotumia vyeti vya watu wengine kwa mini itupie wananchi jukumu lake la kuhakiki vyeti? Wao ndiyo wanavijua vyeti halisi.
Pia ni ngumu kumtaja mtu anayetumia cheti halisi ambacho si chake. Mamlaka zenye nguvu ndizo zinapaswa kujiridhisha zenyewe na elimu za watumishi wao.
Zoezi la kuhakiki vyeti ni gumu na lina utata hasa kwa watumishi waliotumia vyeti vya watu wengine kupata kozi na ajira.
Pana shughuli pevu sana hapa kama itatakiwa kuchimbua historia ya mtumishi tangu akiwa ngazi za chini za elimu,na hapo ndiyo pazuri pa kuanzia kumfahamu mtumishi alikotokea na mtiririko wake was elimu.
Ukaguzi wa vyeti uanzie na elimu ya msingi huko ndiko kuna ukweli wa kumfahamu mtu halisi na vyeti vyake.