Ni lini matangazo ya TBC yatakua na ubora unaoendana na hadhi ya Taifa

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,993
3,684
Wadau,

Naandika hapa nikiwa nafuatilia hotuba ya viongozi wa kitaifa wa Tz na India kupitia chombo chetu adhimu cha TBC1 TV.

Kinachonisikitisha ni hii sauti ya TBC ambayo haijatulia , sasa sijui ni vifaa navyotumia au ni huko wanakorushia,hii imejitokeza mara nyingi unapoangalia "live broadcasting" kupitia TBC.

Nadhani kuna tatizo mahali,wahusika boresheni basi au mmesahau hii ni Tv ya Taifa na inaendeshwa kwa kodi/paye zetu,
 
Bora wangetumia hata camera za Iphone
kuliko walizonazo
Output yao inaboa sana
 
Matangazo ya TBC ni bora kuliko channel nyingine zote ndo maana ukishindwa kulipia king'amuzi cha startimes channel zote zinakatwa isipokuwa TBC 1!
 
Matangazo ya TBC ni bora kuliko channel nyingine zote ndo maana ukishindwa kulipia king'amuzi cha startimes channel zote zinakatwa isipokuwa TBC 1!
Mkuu huo ni ubora au upatikanaji?

"Quality vs affordability & availability"!

Kwa ufahamu wangu ubora hupimwa kwa parameters nyingi! Mojawapo ni hiyo output yao ikoje.
 
Kama ni upatikanaji je kitu kibaya ambacho watu hawana haja nacho kinaweza kupatikana kwa wingi namna hiyo?
Mkuu elewa kwa mapana point..kutokua na ubora kiasi flani bado haimaanishi ni mbaya,pia hakuna anayesema hawana haja nayo!

Be constructive!
 
TBC ni mzigo inafaa kutumbuliwa, habari ni chache majadiliano ni mengi ubora wa picha na sauti ni duni wala haufanani na jina lake kama chombo cha Taifa la tz
 
TBC hamna kitu hata kidogo ,mpaka nakaa chni najiulza hvi Tumerogwa n nn cc Tanzania?
Yaani kwnza Camera za ovyo, picha zmefifia kama ukiangalia kwenye flat screen , animations zao pumba tupu,mchanganya picha haeleweki, yani mavi matupu ,waige mfano wa KBC ya Kenya au Clouds
 
Back
Top Bottom