Ni lini CRDB mtaanza kukopesha tena?

cheeter

JF-Expert Member
Apr 19, 2011
475
155
Tangu zoezi la watumishi hewa lianze CRDB nao wamezuia kukopesha watumishi wa serikali na hata wafanyabiashara. Mwenye majibu basi atujuze ni lini CRDB bank wataruhusu watu wakope. On other hand, nimemsikia Charles Kimei kuwa CRDB wana mpango wa kuongeza branches 11 nchi nzima.
 
katika dunia ya biashara,jambo kubwa sana ni kutabirika kwa hali ya nchi kisiasa,kisheria na kiuchumi.

Kama hali ya usalama wa ajira ya mtumishi ni hatihati,hakuna benki utakuwa tayari kutoa pesa yake kumkopesha mtu ambaye haijulikani kesho ataendelea kuwa mtumishi!

Benki zinafatilia matamko ya kila siku majukwaani kufukuzana.

Benki zinafuatilia hali ya kiuchumi mtaani,hazisikilizi kauli ya wanasiasa kwamba hali ni nzuri.

Benki zinafuatilia kauli kwamba "pesa zitaendelea kukauka mfukoni" sasa wewe unataka ukopeshwe,utalipaje wakati umeahidiwa kutopata pesa ya marejesho
 
Wajiunge kwenye SACCOS za mashirika ya kiserikali ili wakope tu humo..... huku dalili siyo nzuri@cheeter
 
Tangu zoezi la watumishi hewa lianze CRDB nao wamezuia kukopesha watumishi wa serikali na hata wafanyabiashara. Mwenye majibu basi atujuze ni lini CRDB bank wataruhusu watu wakope. On other hand, nimemsikia Charles Kimei kuwa CRDB wana mpango wa kuongeza branches 11 nchi nzima.
ni lini mara ya mwisho umekwenda CRDB bank?
 
Nipo na jamaa wangu wa crdb wamepewa taarifa kuwa mikopo binafsi inaanza mwezi wa kwanza mwakani..
 
Tangu zoezi la watumishi hewa lianze CRDB nao wamezuia kukopesha watumishi wa serikali na hata wafanyabiashara. Mwenye majibu basi atujuze ni lini CRDB bank wataruhusu watu wakope. On other hand, nimemsikia Charles Kimei kuwa CRDB wana mpango wa kuongeza branches 11 nchi nzima.
Ni muhimu kwanza ujiulize unakopesheka? Maanake hata wakianza kesho na wewe hukopesheki ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom