Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Siku zote ukiona wabaya wako wanapiga sana kelele kukutaka uache kufaanya jambo fulani basi wewe fanya hima kukamilisha jambo hilo kwani siku zote mpinzani wako hapendi kukuona unafanikiwa. Ni lini Simba ama Yanga amekuwa na huruma kwa mwenzake? Kufanya vibaya kwa timu moja ni furaha kwa upande mwingine. Vivyo hivyo katika politics. Mafanikio ya chama tawala na serikali yake ni kifo cha upinzani. Haitakuja kutokea chama cha upinzani kikaishauri vizuri chama tawala. Siku zote upinzani unavizia chama tawala kifanye makosa ili wawe na ajenda kwenye jamii.
Suala na sukari kwa sasa limekuwa ajenda kuu kwa upinzani baada ya ajenda zilizopita kutofanikiwa. CHADEMA wameshindwa kutumia utumbuaji majipu kujipatia umaarufu wa kisiasa na badala yake wameshuhudia Rais Magufuli na serikali yake wakijizolea umaarufu na uungwaji mkono kwenye jamii. CHADEMA na UKAWA wameshindwa kufanikiwa kwenye ajenda yao ya Rais kutosafiri nje ya nchi na badala yake wameshuhudia wananchi wengi wakipongeza hatua hiyo kwani imeokoa fedha nyingi. CHADEMA wameshindwa kufanikiwa kwenye ajenda yao ya kulaumu uamuzi wa serikali kufuta sherehe za uhuru na badala yake fedha hizo zitumike kujenga barabara ya MWENGE - MOROCCO. Wananchi wanaotumia barabara hiyo wamekuwa mashuhuda kwa jinsi ujenzi wa barabara hiyo unavyorahisisha usafiri.
Suala na sukari nalo litapita tu. Upinzani unajua kuwa soko la sukari lilihodhiwa na wafanyabiashara wachache wasiozidi 10 ambao ndio wananunua sukari yote ya ndani na inayoingizwa toka nje ya nchi. kuendelea kuacha soko hili katika mikono ya mabepari hao ni kuhatarisha usalama wa nchi kwani uamuzi wowote watakaofanya unaweza kusababisha serikali kuyumba na hatimaye kuanguka. Hapa nampongeza Dr Slaa kwa jinsi alivyolieleza jambo hili.
Nawashauri wapinzani. Endeleeni kujenga vyama vyenu, muwe na viongozi shupavu na Imara kama akina Magufuli, muwe na sera nzuri na wakati wa uchaguzi muandae Ilani nzuri za uchaguzi ili ziwashawishi wananchi wawachague. Mnachokifanya sasa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Rais Magufuli anajua nini anakifanya. Wapinzani tulieni ili Ngosha aendelee kukamua kwa manufaa ya wananchi. Nawashauri wabunge wa CHADEMA subirini mwaka ambao Fisadi atakuja kuwa Rais ndipo mumshauri hayo mnayoshauri. CCM ina Ilani yake na ina viongozi na washauri makini. Haina haja ya kupokea ushauri wenu ambao kwa hakika una malengo mabaya.