Ni lini CHADEMA mtarudisha listi ya mafisadi kwenye tovuti ya chama?

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
TANGU chadema walipompokea lowasa walifuta list of shame kwenye website YAO kitu ambacho wananchi walikitafsiri kama kupoteza falsafa ya kukemea ufisadi na kubaki na nguvu ya soda tu,

Nauliza ni lini hiyo list ya majambazi mtairudisha kwenye website yenu?
 
Hii mada itakuwa na wachangiaji wachache, kwani mleta mada kaupiga mkuki penyewe kabisa, yaani moyoni. Usafi wa wanasiasa, uhalali wao mbele ya jamii, ni vitu vilivyokuwa na nguvu sana enzi za mwalimu Nyerere. Baada ya hapo siasa imepoteza kabisa heshima, huwezi kumsema mtu leo maana hujui kesho fedha zake zitakuwa na nguvu kiasi gani. Unayemkejeli leo hii, kesho anakuwa bosi wako halafu unaanza kufanya kazi nzito ya kumsafisha, tena majukwaani, sehemu ambayo uliitumia kumdhalilisha.

Wanasiasa wa kizazi cha sasa wameshapoteza uhalali mbele ya wanajamii, uongo umekuwa mwingi, hivyo wanajikuta wanapoteza muda mwingi katika kujaribu kuuhalalisha ili ugeuke kuwa ukweli. Cha kusikitisha zaidi ni kuona kuwa tabia hii ya ulaghai katika jamii inaambatana na ukosefu wa uzalendo kwa taifa. Yule yule anayewalaghai wananchi wake hashindwi kuiuza nchi yake, hashindwi kuihujumu nchi yake. Tanzania inao maadui wa ndani na wa nje, wale maadui wa ndani, ndani ya muda wowote ule wanaweza kuwa washirika wa wale wa nje. Kazi ipo, tena pevu.
 
Hii Nguvu manayotumia hapa, mngeielekeza kwenye kumshauri Rais wenu Magufuli, awashughulikie wezi wa ESCROW ambao wengine tayari wameshajipenyeza bungeni na kupewa uenyekiti wa bunge!
 
KUMBE WALE VIJANA MAARUFU KWA JINA LA LUMUMBA BUKU 7 WALIKUWA 46....ha ha ha JK bhana...

..Nimecheka mpaka mbavu
zimeniuna. Kumbe zile tetesi kuwa kuna kundi LA Lumumba buku 7 ni ukweli kabisa baada ya mwenyekiti wao kuwasifia mkutanoni Singida na kusema wakumbukwe kwani walikuwa 46 na wamekuwa wakifanya kazi shift 3 kwa siku bila kulala.
Kasema vijana hao wana hali mbaya kimaisha hivyo kakiomba chama chake kiwakumbuke kwani walifanya kazi kubwa sana kugeuza mambo.
 
Badilisha kichwa cha Habari kilipaswa kuwa hivi :
Ni lini Serikali ya Ccm itawapeleka

Watuhumiwa wrote wa Ufisadi waliowahitajwa Na Katibu wa Chadema Dr Willbriad. Slaa
Wakiwemo

Mkapa
Kikwete
Lowassa
Magufuli
Chenge

Na wengine wengi wa Escrow ,EPA, Kagoda ,

Kuwepo au kutokuwepo bila kuhimiza hatua za kimahakama

kuthibitisha mbele ya sheria haisaidii !!
 
Badilisha kichwa cha Habari kilipaswa kuwa hivi :
Ni lini Serikali ya Ccm awamu hii ya tano itawapeleka

Watuhumiwa wote wa Ufisadi waliowahitajwa Na Katibu wa Chadema Dr Wilbroad. Slaa
Wakiwemo

Mkapa
Kikwete
Lowassa
Magufuli
Chenge

Na wengine wengi wa Escrow ,EPA, Kagoda ,

Kuwepo au kutokuwepo kwenye tovuti ya chadema bila kuhimiza hatua za kimahakama wakajiteteee

kuthibitisha mbele ya sheria haisaidii !!
 
TANGU chadema walipompokea lowasa walifuta list of shame kwenye website YAO kitu ambacho wananchi walikitafsiri kama kupoteza falsafa ya kukemea ufisadi na kubaki na nguvu ya soda tu,

Nauliza ni lini hiyo list ya majambazi mtairudisha kwenye website yenu?
Umepiga ikulu.
 
Lowassa amesema alihama ccm kwa kuitwa gamba na fisadi, sasa chondechonde msimuite fisadi atahama huyooo
 
Hii Nguvu manayotumia hapa, mngeielekeza kwenye kumshauri Rais wenu Magufuli, awashughulikie wezi wa ESCROW ambao wengine tayari wameshajipenyeza bungeni na kupewa uenyekiti wa bunge!

Vipi Richmond baba LA ufisadi
 
Lowassa amesema alihama ccm kwa kuitwa gamba na fisadi, sasa chondechonde msimuite fisadi atahama huyooo

Huo uongo akawambie malofa sio sisi wenye akili timamu ,chadema walimuita fisadi takriban miaka saba hakuama iweje aondoke baada ya kukatwa jina then asema ni baada ya kumuita gamba,
 
Mkuu yule ni mkuu wa Manyumbu
 
Mafisadi waliisha toka Lowasa aende chadema.Kwani umesikia wanazungumzia Tena ufisadi?
 
Hivi FISADI anaweza kuishi nje ya CCM?

Ni sawa na samaki kuishi nje ya maji! Je inawezekana?
 
TANGU chadema walipompokea lowasa walifuta list of shame kwenye website YAO kitu ambacho wananchi walikitafsiri kama kupoteza falsafa ya kukemea ufisadi na kubaki na nguvu ya soda tu,

Nauliza ni lini hiyo list ya majambazi mtairudisha kwenye website yenu?
kipaumbele sasa cdm ni kuindoa ccm madarakani kwa nguvu ya mafisadi.
 
KUMBE WALE VIJANA MAARUFU KWA JINA LA LUMUMBA BUKU 7 WALIKUWA 46....ha ha ha JK bhana...

..Nimecheka mpaka mbavu
zimeniuna. Kumbe zile tetesi kuwa kuna kundi LA Lumumba buku 7 ni ukweli kabisa baada ya mwenyekiti wao kuwasifia mkutanoni Singida na kusema wakumbukwe kwani walikuwa 46 na wamekuwa wakifanya kazi shift 3 kwa siku bila kulala.
Kasema vijana hao wana hali mbaya kimaisha hivyo kakiomba chama chake kiwakumbuke kwani walifanya kazi kubwa sana kugeuza mambo.
Kweli ni wachache ukilinganisha na 189 wa CDM.
 
Back
Top Bottom