Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni utaratibu kwa mtu anayemaliza muda wake kukabidhi Ofisi kwa mrithi wake. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa katika mfumo wa uongozi na utawala wa ngazi yoyote ile.
Ni dhahiri sasa mamlaka ya CHADEMA katika Manispaa ya Kinondoni imezikwa rasmi na sasa CCM imerejea kwa kishindo. Hata hivyo, naiona kwikwi na mgagasiko uliomkumba Meya aliyemaliza muda wake, Boniface Jacob. Sina hakika kama aliandaa Handing Notes. Sina hakika kama Bendera za CHADEMA zilishaondokewa kwenye Ofisi yake. Sina hakika kama zile nyaraka za siri kuhusu mambo kadhaa ya kiuongozi alishaziteketeza.
Pamoja na mgagasiko na kwikwi hizo, ni wajibu wake kukabidhi ofisi mapema iwezekanavyo ili Hapa Kazi Tu ianze mara moja. Kwa vile wafuasi wake wapo hapa, ni vema wakamfikishia ujumbe huu na kumkumbusha jukumu lake la msingi la kukabidhi ofisi.
Nimalizie kwa kusema kuwa huenda Boniface Jacob akaingia kwenye kumbukumbu ya kihistoria ya nchi yetu kwa kuwa Meya aliyekaa madarakani kwa muda mfupi zaidi.