Ni lazima tujuwe elimu za viongozi wetu wa kiroho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lazima tujuwe elimu za viongozi wetu wa kiroho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Matola, Mar 23, 2011.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Wakuu amani kwenu,
  Nimelazimika kuileta hoja hii kwenu, kwani siku hizi viongozi wetu wa kiroho wamekuwa wakizungumzia mambo ya kisiasa kwa niaba ya waumini wao na ukiwa ndio kama msimamo wa madhehebu yao, sasa basi ni haki yao kimsingi kufanya hivyo, lakini mimi ningependa sasa na sisi tusiwe kama mazuzu kuwasikiliza tu bila kuhoji, sasa ningependekeza njia nzuri kwanza tuanze kujuwa na elimu zao za kidunia ni za kiwango gani? ili wawe na huo uhalali wa kuzungumzia mambo mazito ya nchi na kuacha ya dini.
  Leo ningependa mwenye CV za mufti mkuu wa waislamu Issa Bin Simba na Askofu mkuu wa wakatoliki Mhadhama Kardinary Polycaply Pengo atuwekee hapa CV za hawa viongozi wetu hawa wawili ili tujuwe upeo wao kidunia.
  N:B. Asitokee mwehu wa kusema thread hii eti ni ya udini, hapa ni JF where we dare to talk openly. hakuna mkuu nchi hii zaidi ya JAKAYA KIKWETE, lakini hapa anajadiliwa na anachambuliwa in n out.
  Karibuni nimefunguwa mjadala.
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nafikiri huku ni kufilisika kiakili.

  Mambo ya kiimani yana mahusiano gani na mambo ya shule yako. Mfano Babu kule Loliondo ana madegree mangapi mpaka kupata watu mbalimbali kupata kikombe chake.

  Kifupi wao wamechaguliwa na waumini wao na wataaminika tu kwa waumini wao waliowachagua. Huwezi jadili CV za watu hapa.

  Vile vile wangappi wana CV nzuri lakini wanaongoza kwa kutema pumba.

  Heshimu sana imani za watu
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  wale wale! hivi hapa tunazungumzia imani au cv za hawa viongozi? kama una hoja kaa pembeni wacha watu wenye data wazimwage hapa jamvini tuanze kujuwa upeo wa hawa watu. Hakuna mtu asiyejadiliwa nchi hii, hakuna mtu mkuu nchi hii zaidi ya Jakaya Kikwete, lakini anajadiliwa, na kama wasingetaka kujadiliwa wangekuwa wanaishia kuhubili injili na koran tukufu tu, lakini kama wanakuja kwenye majukwaa ya siasa lazima tujuwe upeo wao katika elimu dunia. sisi hatuhoji sheikh amesoma juzu ngapi, wala pengo amekariri vitabu vingapi vya biblia kichwani mwake, hapa tunahoji vidatu.
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,157
  Trophy Points: 280
  Ya Mungu Mpe Mungu Na Ya Kaisari Mpe Kaisari. Mtakuja ambiwa Msipige kura Mkaafiki.

  kwenye dini fanyeni ya dini na kwenye siasa fanyeni siasa kwa faida yenu.

  Ukiona unaonewa ni ruksa yako kudai ila kwa amani lakini unaemdai akikupuuza tafuta nji za kumshitaki hata kwa wanainchi.

  Kukaa chini na kutatua ndio imekuwa chanzo cha watu kuhamasisha maandamano kwani serikali haina mwenyewe, hakuna wa kusikiliza wananchi.

  Wakisikia maandamano ndio wanaanza kustuka tena kwa kuyakemea bila kutafuta njia za kusaidia wadai wao ni dharau hizi, Maandamano yakija TUTAANDAMANA HADI MNG'OKE MBU NYIE(kazi ya mbu ni kunyonya), kama hamtaki tuandamane leteni maisha bora tu sie hatuta andamana. shida ikowapi ukataze bila kutoa mbadala. hufai kuwa kiongozi hata watoto wanafahamu zuri na baya iweje wewe huoni. au umetumwa. kama walichakachua ukapewa uongozi nenda tena arabuni uone mambo yamebadilika. hakuna tena unafiki wa kukumbatia serikali chafu. NAMSHAURI SHEIKH MKUU AACHANE NA SERIKALI CHAFU ITAMCHAFUA NA ITATUCHAFUA WOTE. Imetupindisha na sie tushapinda. dawa ya jeuri ni Kusudi.
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja ya mtoa mada. Tabia ya waumini kuwaweka viongozi vipusa wasiojua A wala C imepitwa na wakati kwa dunia ya leo. Hata kama ni kiongozi wa kiroho lazima aende shule. Sasa ona tunavyopata ukakasi wa matamko ya viongozi wakuu wa kiroho yasiyo na mbele wala nyuma! Lazima tuhimize elimu ili kuondokana na kauli za kijingajinga za viongozi wanaojua kusoma na kuandika tu.
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Kwa kuonesha mfano, CDM wamemchagua mgombe mwenza darasa la saba.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Usinivurugie thread yangu, mambo yenu ya CCM na CHADEMA tafutaneni huko kwenye thread nyingine. hapa ni MUFTI SIMBA CV & ASKOFU PENGO CV.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukweli unaumaaaaaaaaaaaaaaa
   
 9. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Saigon angalizo...unaotaka CV zao ni viongozi wa watu of whom kuna watakaoghadhibika as well as kufurahi...sijui umejiandaaje na hili! Lakini kadiri nijuavyo hata wasingekua viongozi wa dini Busara haziletwi na elimu wala umri wa mtu! Ni common sense tu ya mtu! Kwamba unajua una ushawishi kijamii na kutoa tamko/maneno yanayoweza kuchanganya watu ni kosa sawa na makosa mengine tu! Na km itaonekana inafaa mtoa maneno atalazimika kutoa ufafanuzi bila kujali nafasi yake kwa wakati huo!
   
 10. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  pengo

  born 1944
  ordained 1971
  doctorate in moral theology from Pontifical Lateran Univ. - Rome 1977
   
 11. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  CV YA PENGO HII HAPA KWA UCHACHE.
  Name:
  H.E. Polycarp Card. PENGO
  Position:
  Archbishop of Dar-es-Salaam
  Age:
  66 (Born Saturday, August 05, 1944)
  From:
  Tanzania
  Cardinal since:
  Saturday, February 21, 1998
  Title:
  Cardinal Priest of Nostra Signora de La Salette

  Cardinal Polycarp Pengo, Archbishop of Dar-es-Salaam (Tanzania), was born on 5 August 1944 in the parish of Mwazye, diocese of Sumbawanga in Tanzania.

  From 1959 to 1964 he did his higher secondary schooling at the minor seminary in Kaengesa. In 1965 he entered the major seminary in Kipalalpala for three years of philosophy (1965-67) and four years of theology (1968-71).

  He was ordained a priest in the diocese of Sumbawanga on 20 June 1971 and for two years - from June 1971 to July 1973 - he was Secretary to the Bishop.

  From 1973 to 1977, he studied moral theology in Rome at the Pontifical Lateran University (Academy of St Alphonsus), obtaining a doctorate. After his studies, he returned to Tanzania and taught moral theology at the major seminary in Kipalalpala for nine months in 1977. He then was made the first Rector of the major seminary in Segerea, a position which he held from 1978 to 1983.

  Pope John Paul II named him Bishop of Nachingwea on 11 November 1983 and ordained him on 6 January 1984 on the Feast of the Epiphany in St Peter’s Basilica. He took possession of the diocese on 19 February 1984.

  On 17 October 1986 he was named Bishop of the new diocese of Tunduru-Masasi and he was installed there on 12 February 1987.

  Named Coadjutor Archbishop of Dar-es-Salaam on 22 January 1990, he took possession of the Archdiocese on 22 July 1992 following the resignation of Cardinal Laurean Rugambwa.

  On Sunday 2 September 1990, on the occasion of the Apostolic Visit of John Paul II to Tanzania, the then Coadjutor Archbishop of Dar-es-Salaam, addressed to the Pope the words of homage at the beginning of the meeting with clergy and religious in St. Peter’s Church in Dar-es-Salaam. In introducing the Church in Tanzania to the Pope, he underlined in particular the fidelity to, the love of and the passion for the task of evangelization.

  On 12 April 1984 he spoke at the Fourth General Congregation of the Special Assembly of the Synod of Bishops for Africa. The theme of his speech was, "The Deepening of Christian Faith in Daily Life".

  Created and proclaimed Cardinal by John Paul II in the consistory of 21 February 1998. Titular church Our Lady of La Salette.

  (Source:Catholic-Pages.com | Cardinals of the Catholic Church: Biography of Cardinal Pengo)


  YA SIMBA NAITAFUTA NIKIIPATA NTAWEKA HAPA IJADILIWE PIA aliyeipat atayari aweke
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mpaka sasa hivi ni bla bla tu hakuna aliyeweka CV.
  Ninavyojua mimi Mufti Simba ni darasa la saba kwa elimu dunia.
  Amesoma sana elimu ya dini.
  Kuhusu Pengo sina uhakika lakini najua kuwa na Elimu dunia ni moja ya vigezo vya kuwa kadinali.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280

  Nakuunga mkono kwa asilimia 100% ulichokisema, lakini maana ya mada hii nimegunduwa ni kweli hawa viongozi wa kiroho wanasikilizwa na kuheshimiwa, sasa wanapoongelea mambbo ya kiutawala ni lazima tujuwe elimu zao ambazo ndio kitakuwa kigenzo cha uwezo wa kuchanganuwa mambo, kwa sababu mimi naamini mtu asiye na busara lakini ana eilimu ni afadhali kuliko asiye na vyote viwili.
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilijua huo ndio mwelekea wako sababu kubwa Pengo ni Chadema damu na yupo ku suport na kuifadhili chadema iingie madarakani ili yeye na Papa waweze kuiongoza nchi kwa remote control.

  Tumegundua na hatudanganyikiiiiiiiiiiiiii.

  Vipi babu kule Loliondo ana degree ngapi mpaka kuvuta watu wengi kiasi kile?
   
 15. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Kama mchungaji Mtikila ameweza kubeba yote bila kuleta mtafaruku kwenye moja wapo kwa maana ya kuchanganya mambo nashauri(sielekezi) kwamba yafaa sasa anayedhani ana mbavu nene avae joho la siasa apande kwenye majukwaa ya siasa,na propaganda,kejeli na matusi ya kwenye majukwaa ya siasa ayaache huko huko wakati akipanda kwenye mimbara /kuongoza waumini ya dini yake!
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Labda Saigon ungejaribu kuainisha sifa/kazi za kiongozi yeyote katika kikundi, halafu ukaendelea na mada hii ingekuwa rahisi kwa watu kukuelewa.
  Kwa mtizamo wangu elimu dunia na uongozi vinaenda pamoja japokuwa katika thoery yeyote kuna exceptions.
  Hao wanaosemekama wana madegree halafu hakuna desired results wangekuwa hawajasoma katika tungekuwa tunaongelea maajabu ya dunia, ingekuwa ni wabovu infinite times zaidi ya hapo walipo. Ukitaka kujua elimu dunia na dini vinahusiana hudhuria siku moja viwanja vya manseze-bakhresa usikie kinachihubiriwa. Tena si waislam wala wakristu wote hukusanyika pale.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Umuhimu wa elimu dunia ni kama huu, hawa ni watoto zetu siku hizi wanafundishwa haya, sasa hatuhitaji viongozi saa saba usiku.
  : LATEST FROM NURSERY SCHOOL;
  A-Apple, B-Bluetooth, C-Chat, D-Download, E-Email, F-Facebook, G-Google, H-hp, I-iPHONE, J-Java, K-Kingston, L-Laptop, M-Messenger, N-Nero, O-Orkut, P-Picassa,Q-Quick Heal, R-Ram, S-Server, T-Twitter, U-USB, V-Vista, W-WiFi, X-Xp, Y-Youtube, Z-Zorpia
   
 18. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hii hoja'

  Ningependa pia CV ya Mwingira na Kakobe
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sijui hata kosa langu nini hapo?
  Miye nimeweka wazi tu kiwango cha elimu ya mufti, kama nimesema uongo mufti sio darasa la saba basi nikosoe.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Nadhani ili kurahisisha zoezi hili na kulifanya liwe na ufanisi, naomba mwenye website ya BAKWATA atuwekee hapa na mwenye website ya CCCT baraza la maaskofu atuwekee hapa ili tuingie wenyewe kupata hizi CVs.
   
Loading...