Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,088
- 33,576
Kwa mujibu wa Katiba yetu, Rais wa Tanzania anapoapishwa uahidi "kulinda na kuitetea" Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Maana ya kuilinda ni dhidi ya mtu, watu, ama kundi jingine. Kwa maneno mengine kiapo hakimlazimishi Rais kujilinda yeye binafsi kuvunja katiba.
Rais wetu huilinda Katiba yetu dhidi ya watu wengine, jee yeye ni nani anayemlinda dhidi ya uvunjaji wa Katiba yetu? Usiseme Bunge wala Mahakama zetu kama zilivyo hivi sasa, kwani kwa muundo wa Katiba yetu hii dhaifu na iliyojaa viraka, vyombo hivyo viwili haviwezi kutunishiana Misuli linapokuja suala la maslahi binafsi ya Rais katika uvunjwaji wa Katiba.
Kwa mtazamo wangu ni vizuri sasa kikaongezwa kipengere ama maneno ya kumtaka Rais kuitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania katika kiapo siku ya kuapishwa kwa Rais. Hii itamlazimsha Rais Kumlazimisha kutii Katiba kwani akienda kinyume cha hata mtu wa kawaida tu anaweza kwenda Mahakamani kulalamika kwamba Rais ameshindwa kuitii Katiba.
John Pombe Magufuli akila Kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania