Ni lazima mawaziri kuwa wabunge?

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
80
Kuna hiki kitu kinanisumbua sana akilini mwangu hususan ukizingatia ya kuwa tunajitahidi sana kuikosoa, kuirekebisha na kuishauri serikali yetu, serikali ifanyayo mambo kana kwamba haiwajibiki kwa mtu, ila kila baada ya miaka mitano hurudi kwa wananchi wake na kuwaahidi mambo lukuki. Na wananchi jinsi walivyo na huruma na kusamehe kwa wepesi, huwachagua tena kwa matarajio ya kuwa “pengine this time watabadilika”.
Tatizo nililonalo mimi ni mfumo mzima wa serikali yetu kwa hivi sasa. Serikali kuwa na mkono kwenye kutunga sheria, “Mawaziri ambao ni wabunge”. Mimi hili naona halijatulia, kwani tuna imani kama bunge ndilo litakalokuwa na jukumu la kuiweka serikali ‘in check’, sasa kama ikiwa wabunge wenyewe ndio serikali, nani atakayemfunga paka kengele?
Hii ndio ipelekeayo visa vyote vya Kiwira, Richmond, EPA, na vinginevyo vingi tu ambavyo havijavuja bado. Kama serikali isingekuwa na mkono bungeni, hii ingewafanya angalau kidogo kuwa na discipline katika mambo yake kwani inajua kutakuwa na oversight ya bunge. Lakini leo hii muhemishimiwa Waziri anajua fika dili lake la wizara litapita kiulaini bungeni kwani wajumbe wa kamati ya bunge ni constituency neighbors, washkaji wanajirusha pamoja kwenye vikao vya bunge, sasa watafanya nini.
Wabunge wawe wabunge kuwatumikia straight wananchi, na mawaziri wawatumikie wananchi for the pleasure of the President. Sasa waziri asaini mkataba hotelini nje ya nchi, ajue ana la kujibu bungeni.
Or may be haya ni mawazo yangu tu, kuna ufanisi mkubwa sana kwa system tuliyonayo, mimi siuoni tu.
 
Hili tumelirithi kutoka kwa watawala wetu, Waingereza. Kwa kuwa Wabunge wetu wanaoteuliwa kuwa mawaziri "WANAFAIDIKA" sana na mfumo huu, kwa sasa huwezi kuwaambia kitu. Waziri kama wa MiundoMbinu humwambii kitu kuhusu "ndoa" yake batili na mameneja wa TANROADS wa Mikoa; Waziri wa Maji na Wakurugenzi wake wa Mamlaka za Maji Mijini ndio kabisaaa; Waziri wa Kazi na NSSF yake....n.k. Huu ndio UFISADI mwingine ambao hauvumi sana ingawa jamaa wanapeana mamilioni, wanajengeana majumba, wanasomesheana watoto...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom